Lethergo
JF-Expert Member
- Aug 7, 2023
- 6,534
- 11,421
Wakuu,
Leo acha nizungumze na wazazi, wazazi mtanisamehe kwa nitakachokizungumzia hapa leo hii ila naomba mnielewe. Naombeni muda wenu walau kwa dakika kadhaa someni hiki ninachowaasa kitawasaidi nyinyi na watoto wenu.
Kuna katabia nimekabaini katika baadhi ya familia sio zote hususani hizi familia zinazochipukia nasema kusema familia changa. Ndoa ina mwaka mmoja au miwili au miaka mitatu. Familia labda imebahatika kua na watoto wawili au watatu wadogo, tuseme wenye umri wa miaka kati ya 3/4/5/6 mpaka 7.
Kumekua na kajitabia ka wazazi kufanyia mapenzi mbele ya watoto wakihisi labda watoto hawawezi kuona au labda hawawezi kuelewa nini kinachofanyika mbele yao. Hiki ninachosema nimeshuhudia sehemu kikifanyika. Lile jambo kusema ukweli sikulipenda hata kidogo kuona wazazi wakipenzika mbele ya watoto sio vizuri na haijengi afya ya akili ya watoto.
Hivi mzazi unapofanya mapenzi mbele ya mtoto wako unamfundisha nini mtoto? Sawa ana umri mdogo kwa hio ndio uamue kufanya mapenzi na mwenzio mbele yake? Mbaya zaidi chumba kipo mnacholala chumba chenu kipo l lakini cha ajabu mtoto yupo sebleni mnamwekea movie au katuni kisha nyinyi mnajivuta kochi la pembeni mnaanza kufanya mapenzi, mtoto akigeuza shingo anawaona mnachokifanya, mnafikiri mtoto km huyo anajifunza nini kwenu nyinyi wazazi?
Wewe mzazi nakuuliza wewe unawaza nini unapofanya mapenzi mbele ya mtoto wako? Huo ni ukatiri kwa watoto suala la kufanya mapenzi mbele ya mtoto sio suala jema kabisa nalikemea, sawa basi mmemwekea movie au katuni nendeni mkafanyie mambo yenu chumbani kwenu huko km faragha kwani ni lazima mfanyie sebleni mbele ya watoto? Mnajivuta kochi la nyuma mmejibanza mnaanza kufanya mambo kwani chumbani kuna umbali gani mzazi?
Watoto wanapoenda mashuleni wakianza kufanya mlichokua mnakifanya mbele zao huku wakijichukua video mnaanza kuwasema vibaya lakini kumbe chanzo kimeanzia nyumbani alipotokea hilo jambo amekua akiliona kwake ni la kawaida maana amekua akimuona baba na mama wakifanya hivyo.
Nimeshuhudia sehemu hili jambo likifanyika na sikulipenda wala kufurahishwa nalo hata kidogo ingawa sikupenda kuwaambia wahusika kua mnachokifanya sio kizuei maana ni kawaida yao kufanya hivyo ila hakitengenezi picha nzuri kwa watoto.
Kwa sababu watoto wana kawaida ya kufanya marudio au marejeo ya kile walichokiona au wanaweza kwenda kusema kwa watu kwamba nimeonaa baba na mama wanafanya hivi na hivi au akajaribu kufanya na mtoto mwenzie. Na hio akifanya na mtoto mwenzie inakua ni kwa siri sana wanachokifanya hiki nimekisshuhudia kikifanyika watoto wakifanyiana sababu mtoto mmoja amekua akiona wazazi wake wanachofanya anaenda kufanya na mtoto mwenzie wakiwa chumbani wamejifunika blanket kumbe wanafanya michezo ya ajabu kabisa na ni watoto.
Sasa bora hio mtoto amefanya na mtoto mwenzie hajafanya na mtu mzima, je mtoto akitamani kufanyiwa na mtu mzima nyinyi wazazi mtaweka wapi sura zenu au mtasema mtoto amejifunzia wakati amekua akiwashuhudia mnachofanya?
Sikatazi wazazi kuzuia watoto wa kike na wa kiume kuchangamana ila kwa watoto ambao wanaona wazazi wao wanachofanya kuna wakati wanaenda kufanya marudio ya kile walichokiona.
Hili nimelishuhudia likifanyika na sikupenda maana watoto wanafanya kile wanachoona sasa ukiangalia watoto ni wa umri mdogo inakuaje wazazi wanaruhusu jambo km hili litokee?
Mzazi una mtoto wa kike na kuna jirani ana mtoto wa kiume, unaruhusu watoto hawa wawe wanatembeleana na kucheza pamoja sawa, mmoja wa watoto hawa amekua akiwaona wazazi wake wakipenzika mbele yake. Baada ya hapo anamfuata mwenzie wa jitani ambae hucheza nae mara kwa mara michezo ya watoto na kumwambia kwamba amepata mchezo mpya ambao ameuona mama na baba yake wakiucheza, mwenzie bila kujua anamwambia haya tucheze.
Wazazi mtanisamehe kwa hiki ninachokisema hapa ila hiki ninachokisema nimekishuhudia kwa macho kikifanyika, ilifika wakati watoto wakaanza kucheza wazi wazi wakidhani kwamba lile ni jambo la kawaida hata wao wanaweza kufanya na wazazi baada ya kuona hivyo wakachukua hatua ya kuwaadhibu pasina kujua kwamba ni wao ndio waliowafundisha kufanya hivyo.
Wazazi nawasihi sana mnaoishi na watoto hakikisheni hamfanyi mapenzi mbele ya watoto wakiwa wanawatazama sababu mnawaharibu watoto hususani watoto wadogo wenye miaka 3/4/5 mpaka 7 mkifanya hivyo mnawaharibu kisaikolojia, iwe kwa kushikana shikana au kubusiana busiana au kuvuana vuana na kufanyiziana mambo yenu mbele ya watoto mkihisi kwamba ni watoto tu hakuna wanalolielewa mnakosea watoto wanaelewa kwa haraka sana na wana uwezo wa kudurufu kile ulichofanya maradufu kuliko wewe.
Wazazi km wewe ni mzazi na una hio kawaida ya kufanya hayo mapenzi mbele ya watoto ukihisi ni usasa acha kabisa unamuharibu huyo mtoto, wewe mzazi huwezi kwani kwenda faragha hadi ufanyie mambo yako mbele ya mtoto? Huoni km unamuharibu huyo mtoto kwa kufanyia mambo yako ya chumbani mbele yake?
Wazazi muache huo sio uzungu bali ndio mwanzo wa mmonyoko wa maadili kwa watoto wako maana mtoto atasema nimeona baba anafanya na mama na mimi ngoja nifanye huoni unamuharibu huyo mtoto?.
Wazazi muache hio tabia ya kufanyia mapenzi yenu sebleni mbele ya watoto mnawaharibu.
Nimechoka hata kuandika niishie hapa tu ila wazazi acheni kufanya hivyo mbele ya watoto.