Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 441
- 1,065
- Thread starter
- #21
Wewe ndo unasema ni mtetezi wa haki za binadamu na unapendekeza badala ya mwanafunzi kupewa "adhabu" apewe "kazi"?Kazi ni nyingi shuleni unaweza kumpa adhabu ya kufanya usafi eneo fulani kwa siku ama zaidi ya siku moja kulingana na ukubwa wa kosa.
Kumwagilia maua maji na kutunza bustani ni miongoni mwa adhabu ambazo mwanafunzi ataona ni kubwa zaidi na atajiepusha na kutenda makosa akihofia kufanya kazi hizo.
Adhabu za viboko ni urithi wa kipumbavu tulioachiwa na wakoloni na sisi tukaendelea kufanyiana Waafrika wakati hao walioiasisi wala hawaitumii kwao.
Afrika ni laana wakati mwingine maana hatuna muda wa kujiuliza na kutafakari badala yake ni kuiga tu vitu tulivyokuta tunafanyiwa na wakoloni. Too pathetic.
Kwanza kabisa unatakiwa ujue kutofautisha "adhabu" na "kazi". Kumwagilia maua, kutunza bustani, kufanya usafi si adhabu bali ni shughuli ambazo inabidi watoto wafundishwe kuzipenda na kuzithamini
Kazi kama hizo zikigeuzwa kuwa adhabu maana yake ni kuwajenga kisaikolojia watoto waamini wanaofanya kazi hizo wanaadhibiwa kwa makosa fulani fulani. Ukiwa naakili timamu utanielewa nachokisema hapa
Adhabu kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili ni "mateso anayopata mtu kwa lengo la kumrekebisha kutokana na makosa aliyofanya". Tuwazoeshe watoto kuwa kufanya usafi ni mateso? Kutunza bustani ni mateso?
Nabaki kuishauri serikali kupitia wizara ya elimu kufanya tathimini upya ya adhabu ya viboko itakayopelekea kufuta adhabu hiyo shuleni lakini pamoja na ushauri huo sioni kama kutunza bustani, kufanya usafi ni mbadala wake