Kifaa kinachotumika ni fimbo ambayo bila kutarajia inaweza kusababisha jeraha hasa ikipasuka na kipande cha fimbo kuchana sehemu ya mkono au bila kutarajia fimbo ikagusa sehemu ya kidole kikavimba hasa kwa wenye ngozi laini
Ikumbukwe kuwa, mtoto akishakuwa na jeraha au uvimbe ni vigumu jamii kuelewa kwasababu wao "focus" yao itakuwa kwenye jeraha au uvimbe hata kama alichapwa fimbo moja tu!
Kitu kingine kinachonishawishi kushauri tamko la kufuta hii adhabu ni pale linapotokea tatizo kwa mwanafunzi kuumizwa, hakuna anayekumbuka kuangalia dhamira ya Mwalimu iliyomsukuma kutoa adhabu aliyotoa
Kuna watu nimeona wameshauri kuwa adhabu mbadala kama kumwagilia maua, kufyeka, kulima, kufanya usafi, nk zitolewe kwa wanafunzi wanaofanya makosa. Hawa wamesahau kuwa hizi shughuli hazipaswi kupandikizwa vichwani kwa watoto kama adhabu badala yake wanatakiwa kujengewa mazingira ya kupenda shughuli za mikono kwani mbeleni zinaweza kuwa msaada kwao
Adhabu ni tendo analofanyiwa mtu kumuonywa kufanya jambo baya. Kwa maana nyingine tendo hilo lazima liwe la kuumiza au kumnyima mtu uhuru au haki fulani kwasababu amevunja sheria. Tukiwazoesha watoto kuwa kumwagilia maua ni kazi za wenye makosa tutakuwa tunatengeneza jamii ya aina gani?
Kuna shule moja mtoto alipoteza maisha kwa kuangukiwa na jiwe wakati wanachimba kifusi, wahusika wa shule ile waliyopitia wanayajua. Kuna shule watoto walikutwa wanazimbu chemba za choo zilizoziba (kwa matumizi yao mabaya), bado ilionekana walimu wamekosea
Mbaya zaidi anayependekeza watoto wapewe adhabu za kumwagilia maua au kufanya usafi anajiita "mtetezi wa haki za binadamu". Yaani kwake kufanya usafi anataka iwe adhabu isiwe kazi ya kawaida na ya kuwajenga watoto wapende kufanya usafi
Mimi nadhani adhabu ndogo ndogo zinawezakuwa kama kupigishwa magoti bila kujali kwa muda gani kulingana na kosa, kukalishwa chini, kunyimwa fursa zinazopatikana shuleni kama kufungiwa kushiriki michezo (kama ni mwanamichezo), kuzuiliwa kushiriki masomo kwa kipindi fulani (suspension), na wenye makosa makubwa kufukuzwa shule kama ilivyo kwa sasa
Nashauri adhabu ya fimbo ifutwe lakini mbadala wake haiwezi kuwa shughuli za mikono kwasababu "adhabu" ni tendo la kumuonya mtu hivyo tendo hilo lazima liwe lisilo la kawaida