Ushauri kwa Wizara ya Kilimo-Fursa zinazotakiwa kufunguliwa ni za mazao ya biashara sio chakula

Ushauri kwa Wizara ya Kilimo-Fursa zinazotakiwa kufunguliwa ni za mazao ya biashara sio chakula

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Salamu!
Mada inajieleza,
Fursa zinazotakiwa kufunguliwa na ambazo nitaziona kama kipimo cha wizara ni zile za mazao ya biashara mfano pamba,kahawa,mwani na mazao ya wanyama kama ngozi ,pembe na kwato.

Nadhani nimeeleweka!
 
Mkuu elezea zaidi,serikali ifanyaje hapo

Ova
 
Labda huko mikoa mingine. Kagera ukutwe unauza hiyo kahawa kwa Waganda utapewa kesi ya uhujumu uchumi.
 
Mkuu elezea zaidi,serikali ifanyaje hapo

Ova
Ifungulie fursa ya mazao ya biashara kama vile ngano,kahawa,miti n.k
mfano tunatakiwa kutafuta fursa ya kusafirisha mkaa nchi za ulaya hususani majira ya baridi.
 
fafanua zaidi mkuu
Ni kwamba kahawa ya Kagera na baadhi ya maeneo ya Kigoma ina sifa za organic maana madawa na mbolea za viwandani havitumiki. Baada ya Waganda kuliona kila mwaka huwa wanatoa ofa kubwa kuliko ya vyama vya ushirika. Kutokana na kwamba kuna mirija ndani ya vyama vya ushirika basi hakuna kiongozi wa serikali anayependa kahawa iuzwe Uganda. Ukikamatwa kahawa yako inaitwa magendo unashtakiwa na Jamhuri. Mleta mada ana hoja lakini nahisi hata kwenye korosho ni hivyohivyo.
 
Ifungulie fursa ya mazao ya biashara kama vile ngano,kahawa,miti n.k
mfano tunatakiwa kutafuta fursa ya kusafirisha mkaa nchi za ulaya hususani majira ya baridi.
Wazo zuri,tatizo nchi hii kuna kundi fulani wao tu ndiyo wanataka waendele kuwepo na wao tu ndiyo wawe matajiri
Seeikali ndiyo linajukumu la kufungua fursa ...tunataka kuona mabilionea wengi wa kitz wanatokana na kilimo
Siyo kila kukicha unaambiwa mabilionea sijui ni wakata mauno tu

Ova
 
Salamu!
Mada inajieleza,
Fursa zinazotakiwa kufunguliwa na ambazo nitaziona kama kipimo cha wizara ni zile za mazao ya biashara mfano pamba,kahawa,mwani na mazao ya wanyama kama ngozi ,pembe na kwato.

Nadhani nimeeleweka!
Mkuu ongezea na bangi pia

Ova
 
Back
Top Bottom