Mashindano ya kimataifa ndio imeanza, tafuteni scout wa kuwatafutia wachezaji wazuri zaidi watakaowasaidia hapo Yanga katika mashindano ya kimataifa.
Huu ujinga wa kuleta mchezaji toka Uingereza anakuja kulipwa hela nyingi na kuja kukaa benchi....... ni hela ambazo zingetosha kabisa kumuajiri scout wa kutafuta vipaji vitakavyoisadia Yanga kipiga hatua nyingi mbele.
Na huu ujinga mwingine wa kutujazia Wakongo ambao viwango vyao vinazidiwa na wachezaji wengi tu wa Kitanzania muuache vilevile tafuta scout afanye kazi hiyo.
Na huu ujinga wa kumsajili mchezaji baada ya kumuona akicheza mechi moja au mbili na akacheza vizuri, mkakurupuka na kumsajili vilevile muuache, tafuta scout afanye hiyo kazi ya kumfatilia zaidi huyo mchezaji.....
Maana inawezekana hata hapo baada ya kucheza na Al Hilal mshaanza na maongezi na baadhi ya wachezaji wao.
Nimemaliza
Sent from my SM-A135F using
JamiiForums mobile app