Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ujinga ni kuishi kinadharia anaetoa gharama za maisha na kuonyesha ugumu wa mtu kukabili izo garama kwa pound 250/week ni mpumbavu na anapaswa kupuuzwa.

Cha muhimu kushinda yote ni uwe na uwezo wa kuwasiliana hapa namaanisha angalau ujue English.

Yeyote mwenye nauli please tafuta host nimechek mf . USA kuna hostels maeneo mbali mbali na bei zao kwa mwezi ni kuanzia dola 500+ then chakula unajitegemea.

Sijui nisemeje ila kwa ufupi huwezi kufanikiwa kimiujiza lazima ujitoe, tafuteni nauli kupata host is not a big deal naweza kuwatafutia host kwenye mtandao watu watakaohitaji kwenda Korea kusini na japani. Hivi vitu vinawezekana jiamini hii Dunia ni yetu sote
 
Upo sahihi mkuu.

Ila unapotaka kufanya jambo chukua kila aina ya ushauri hata usipoutumia utakuwa shield au ngao pale mambo yanapokuwa mabaya.

Risk ndiyo kila kitu mengine baadae.
 
Naongelea uingereza nimekupa data, njooni mujaribu, Korea ya kusini nina mashaka.wafilipino wako karibu sana na hapo Lkn wanaenda uarabuni kufanya kazi.uarabuni ni zaidi ya kilomita 6000 hapo Korea kusini si zaidi km 2000.uarabuni wafilipino wanalipwa si zaid us dollar 500 kwa mwezi kwa nn wasiende hapo karibu?
 
South Korea kuna jamaa anasoma Seoul university anapasifia saana anasema earning per day ni kama 48000 won ambayo ni kama 95elf ya kibongo. Sema unatakiwa ufanye kazi kweli kweli.

Nwei : Nashukuru maana kila mmoja anatoa ushuhuda kwa jinsi anavyoshuhudia maisha ndani kwake.
 
Mbona poa tu
 
Hata Macedonia tunaenda tuu
 
Safi sana mkuu na hongera, ila usiwahi sana kumwambia khs reward, hiyo normally ni matokeo ya hospitality yako mkuu,
Asante
 
Asante kwa courage mkuu,
 

MziziMkavu
Uhamiaji Au kujilipua kamwe hakutwa pitwa Na wakati.Kubadilisha mazingira Au kutoka nje ya box NI faida kubwa Kwa Watu Na Jamii.
Ukienda nje ya nchi utapata Elimu Na pesa Kwa kufanya kazi.Ukirudi Tanzania utaanza kuviona vitu ambavyo Ulikuwa huvioni wala kuvifikiria.
Hizo fursa ambazo ziko Tanzania utaziona baada ya kutoka kwenye BOX.
 
Mkuu Karibu sana Ulaya uje ujionee Mwenyewe usingojee mpaka uambiwe njoo uje ubebe Maboksi na kuwa Mtumwa wa Wazungu.

 

Mkuu Okyoma unayo sema mengi NI kweli Ila hizo roho mbaya zinapandikizwa Na wachache.
Mfano unamsaidia mtu kila kitu akisha pata kazi tu wewe hauna maana Lakini sio wote.
Mkuu mimi nilisaidiwa kwenda kusoma USA.
Kwenye geto yetu tulikuwa Watu 7 tulikuwa tunasaidiana kwa kila kitu Lakini mmoja wetu akaanzisha fitna tuka muaka kati tulivyo maliza mwenyeji wetu akamfumuza mfitini.
Sasa kama unapata mtu kama huyo kweli unaweza kumsaidia mtu mwingine? Lakini huyo mwenyeji wetu bado anasaidia watu mpaka Leo hii Ukiwa Na roho ya kusaidia hauwezi kubadilika Na hao wako wengi tu.
 
Mkuu Karibu sana Ulaya uje ujionee Mwenyewe usingojee mpaka uambiwe njoo uje ubebe Maboksi na kuwa Mtumwa wa Wazungu.

View attachment 485814
Nimecheka sana ile POST yako ati ULAYA hakufai ilhali wewe ungali umeng'ang'ania huko... wengi wametoka kwa kuja Ulaya kutafuta maisha....

Mkuu wape njia wana nao waje wasake LIFE!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…