Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

mm naitaji kwenda Iceland , Malta au Sweden, nipeni contact niweze kupata Barua ya mwaliko tu, mambo mengine yote nitasimamia mwenyewe bila wasi wasi wowote maana nimejipanga vyakutosha .
Tatizo ni hilo tu, Barua ya mwaliko.
Mkuu iceland mbali kote huko?
 
Wakuu kuna mtu yuko USA ni raia anataka kutuma barua ya mwaliko TZ but hajui aanzie wapi, ni anaandika email tu na kutuma??? au lazima apititie US embassy ya kule ???? na ni vitu gani anaambatanisha??? Nisaidieni hapo.
 
Barua ya mwaliko inaandikwa kiofisi yani inaonesha address yake na yako, tarehe, kichwa cha habari, pia mwishoni kuna kuwa na sahihi ya mtumaji na muhuri kama ni taasis ama shirika na inaelezea madhumini ya safari yako. anaaweza ku google ili aiandike kwa ufasaha zaidi.

Unaweza ukatumiwa kwenye email then uka print out, lakini sijui kama hii inakubalika kila balozi.

Unaweza ukatumia iyo barua kwa njia ya posta itachukua wiki 2-3 -4 ama anatumia express ambayo ni ndani ya siku 2-3 .
 
Mkuu asnte kwa maelekezo mazuri kwa hio anaingia google anajaza kama form online ?? au anaandika tu kwa email ???
 
Wakuu kuna mtu yuko USA ni raia anataka kutuma barua ya mwaliko TZ but hajui aanzie wapi, ni anaandika email tu na kutuma??? au lazima apititie US embassy ya kule ???? na ni vitu gani anaambatanisha??? Nisaidieni hapo.

Huu NI Mfano wa barua kutuka Kwa mtumaji
Jina kamili
1234 S. Main Street
Los Angeles,CA 90019
Cell phone 213.555.1212
E-mail xyzzy@gmail.com


April 04 2017
Consular section
Embassy of United States of America
Dar-es-Salaam,Tanzania

I,jina kamili la mtumaji,cordial extend my invitation to Mr (Mutasha John Doe) to visit (jina la mji anao ishi) mfano Los Angles,California this Spring of 2017.
I am resident of the state of California and an American citizen.I reside at the address above

I am a co-founder of xyzzy Inc.As financial officer based in Hollywood California and a member of Tanzanian community in greater Los Angles.

The invitation will be for four months.Mr.Mutasha John Doe will purchase his round trip to Los Angles and I (jina la mtumaji)
will cover all of his financial responsibilities when he will be staying with my family.

I am looking forward showing him Hollywood,Universal studios,Disneyland and many other attractions in California.

Here is pertinent travel information for Mr Mutasha
Tanzanian Citizen
Passport No A...........
Date issue 12 Feb 2017
Name Mutasha John Doe

Sincerely
Mtumaji jina kamili

Mtumaji atandika barua kama hiyo Halafu anakutumia kwenye barua Pepe.(E mail)
Halafu Wewe unajiandikisha kwenye tovuti ya US embassy( non immigrant visa application (DS-160) itakugharimu $70 ambayo hurudishiwi kama ukinyimwa visa.
Ukiitwa Na ubalozi Kwa mahojiano ndio unapeleka hiyo barua,akounti za banki,Au udhamini wowote kuonyesha kwamba ukienda USA hautarudi Tanzania.
Kila la heri
 
Asante sana mkuu, ila hapo kwny akaunti ya bank inatakiwa iwe na salio kiasi gani ???? au mtu wa kunidhamini inatakiwa mwny vigezo gani ????
 
Hakika umeleta chakula kizuri sana, barikiwa mkuu
 
Asante sana mkuu, ila hapo kwny akaunti ya bank inatakiwa iwe na salio kiasi gani ???? au mtu wa kunidhamini inatakiwa mwny vigezo gani ????

Mutasha
Banki akaunti isikutishe sana.Wako watu wengi wenye mifuko mireeeefu bank lakini visa hawapati.Muhimu uoneshe vigezo kwamba unayo sababu ya kurudi Tanzania.Mfano biashara zako(mashamba,nyumba za kupangisha) Mke, familia( ndugu wa damu).
Mdhamini wako hapa Tanzania atakufanyia
(Mazingaombwe) ili uwe Na vigezo vyote.
Nadhani umenielewa hapo.Jihadhari na wadhamini usio wajuwa.
 
Tunashukuru sana kwa mrejesho mzuri lakini tunaomba wenye ujuzi wa kuingia kwenye Balozi mbalimbali mtupe ujuzi ni vitu gani muhimu ukiwa navyo inakuwia rahisi kupata visa na maanisha ukiwa tayari na barua ya mwaliko.
 
 
Tunashukuru sana kwa mrejesho mzuri lakini tunaomba wenye ujuzi wa kuingia kwenye Balozi mbalimbali mtupe ujuzi ni vitu gani muhimu ukiwa navyo inakuwia rahisi kupata visa na maanisha ukiwa tayari na barua ya mwaliko.

Kitu Cha kwanza usiwe na wasi wasi.Vaa vizuri
Sio suti Na tai:usivae mashati ya maua maua na dengirizi(jeans) usivae kofia,mlegezo Au T-shirt tumia dawa ya kwapa na ya mdomo USAFI NI LAZIMA.
Kila ubalozi una sheria zake ingia kwenye tovuti zao wataoredhesha vitu vinavyo hitajika.
Ukiwa kwenye mahojiano Na mwakilishi wa ubalozi husika 1) eye contact (tizama machoni)
Ukitizama chini maana yake NI muongo Au unaficha kitu.Fanya Mazoezi ya kutizama mtu usoni Kabla hujaenda.2) usiseme kitu kama hujaulizwa.Jibu maswali tu:Kama haujayaelewa
TAFADHALI mwambie hujaelewa swali.Hata kama unajuwa usijifanye unajuwa.Vilevile kama lugha inaangaisha wapo wakalimani wa Kiswahili hata wanao kuhoji wanajuwa Kiswahili usiogope kuomba mkalimani.Hapa unaonyesha uzalendo wako sio kwa nia mbaya.
3) Muhimu sanaaaaa lazima ujuwe umeandika nini kwenye application yako.Maana maswali yote yanatoka kwenye hiyo application.
Utaulizwa jina lako kamili,Ulizaliwa wapi kila kitu
Ulicho jaza.Ukifauli maswali hayo.Unanafasi nzuri ya kupata visa.
 
Tunashukuru sana kwa mrejesho mzuri lakini tunaomba wenye ujuzi wa kuingia kwenye Balozi mbalimbali mtupe ujuzi ni vitu gani muhimu ukiwa navyo inakuwia rahisi kupata visa na maanisha ukiwa tayari na barua ya mwaliko.

Mkuu fokofu
Swali lako Kuhusu Japan.MwanaJf
Tokyo40 anaweza kukujibu vizuri.
Vilevile amejibu maswali mengi kwenye huu uzi
Kuhusu Japan.
Kila la kheri
 
Mkuu asante kwa mrejesho mzuri na vipi kuhusu flight tiketi naiakata mapema ili siku ya interview niende nayo kama kiambatanishi ???? au naikata baada ya kupata visa ????
 
Mkuu asante kwa mrejesho mzuri na vipi kuhusu flight tiketi naiakata mapema ili siku ya interview niende nayo kama kiambatanishi ???? au naikata baada ya kupata visa ????

Usikate tiketi mpaka umeweka visa mkononi.
Visa kawaida ni ya miezi 6 mpaka 12
 
Usikate tiketi mpaka umeweka visa mkononi.
Visa kawaida ni ya miezi 6 mpaka 12
Ok sasa kabla kunipa visa hawataniuliza tiketi ??? Pia baada ya kupata visa lazima niondoke ile ile iliyotajwa kwny mwaliko??? au naweza kuondoka mda wowote naotaka mm ???
 
Ok sasa kabla kunipa visa hawataniuliza tiketi ??? Pia baada ya kupata visa lazima niondoke ile ile iliyotajwa kwny mwaliko??? au naweza kuondoka mda wowote naotaka mm ???

Mutasha
Ukinunua tiketi Kabla ya kupata visa ni hasara kwako.Kwenye tovuti ya ubalozi wa Merekani
Wameeleza wazi kwamba usinunue tiketi mpaka upate visa.Sijui utaratibu wa mabalozi wa nchi zingine.Kama nilivyo kueleza hapo awali:visa ni ya miezi 6 mpaka 12 unaweza kuondoka wakati wowote.Mfano umepata visa mwezi wa May 20 2017 utapanga kuondoka June 21 2017 tiketi yako itakuwa rahisi $300
www.cheapoair.com
Muhimu unajitayarisha Na kupata visa kwanza halafu mambo ya tiketi NI ya mwisho.
 
Nashukuru sana mkuu kwa maelezo yako hakika nimejifunza mengi, tutazidi kupeana mirejesho kadri siku zinavyokwenda, nilichogundua bado wa Tanzania wengi tuna mengi ya kujifunza na nina amini hakuna kinachoshindikana kama unatimiza vigezo vyote vinavyohitajika ili mtu kuweza kupata visa ya kwenda nchi husika.
... Nimefuatilia sana huu uzi tangu mwanzo tatizo nililoliona ni watu wachache sana wenye ujuzi wa ng'ambo wamejitokeza kutuletea mrejesho nawapongeza sana siwezi kuwataja wote kwa majina wengi wenye ujuzi wa mambo ya ng'ambo wamejificha na wengine wanajaribu kutoa mirejesho ya kufikirika ambayo kiuhalisia haiwezekani wenzetu huko hawafanyi mambo ya kubahatisha wala hawana mkatomkato kama huku bongo wala hamna mambo ya kujuana.
 

Mkuu fokofu
Muhimu katika maisha NI kushukuru ulicho nacho Na kukifanyia kazi ili kikusaidie.
Hili jukwaa kama ulivyo eleza umelisoma lote.
Wachangiaji wengi wameweza kutufungua macho Na mambo mengi tuliyo kuwa hatuyajui.
Wahenga wa majuu walisema "If you get a lemon [emoji522] make a lemonade"
 
Reactions: SDG
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…