Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Wakuu huku ktk hili jukwaa inawezekana nikampata mtu ambaye yuko Msumbiji au anayejua namna ya kupata uraia. Kwani ni kama wiki mbili zilizopita nikiwa natoka Moshi kuna Mzee tulikuwa tunapiga stori za maisha kwa ujumla ananiambia raia wa kule sio watu wa kujishghulisha. Yeye anasema alitoka huko miaka kumi na mbili iliyopita. Msaada wenu kwangu utanisaidia sana
 
Maputo ndo sehemu salama kule ni kireno hasa, fulsa za biashara zipo pia wao wanapenda sana dawa za asili miti shamba kama wamasai wanavyouza. Kuna dada yupo humu Jf anaishi huko nadhani anaweza kueleza vizuri.
 
Changamoto ya hizi nchi zisizotumia Kiingereza ni kuelewa lugha yao kwenye website zao hapo hua naumiza kichwa sana
 
Wakuu naombeni ushauri, Nina rafiki yupo USA tulikutana. online tuna miezi miwili sasa, je akinitumia mwaliko pale US embassy watanipa visa? au inatakiwa urafiki uwe wa mda mrefu ?? angalau miezi mingapi??? Nisaidieni. wakuu.
 
Nashukuru Wakuu. Yule Mzee kazi nyingine aliyonielekeza biashara ya Mgahawa kwani raia wa huko huwa hawapikagi pia swala mapishi hawako vizuri. Na kikubwa kwangu natakakuju namna ya kupata uraia ili nikishaingia kule nianze kuangaikia kwani naamini nikiupata uraia nirahisi kuwekeza ktk hizo biashara.
 
Mkuu hayo maswali yako yamejibiwa katika huu uzi
Tafadhali soma vizuri
 
Changamoto ya hizi nchi zisizotumia Kiingereza ni kuelewa lugha yao kwenye website zao hapo hua naumiza kichwa sana

Hizi nchi huwa wanaweka lugha ya kiingereza katika tovuti zao maana zinasomwa na watu wa mataifa mbalimbali..

Ukiangalia juu upande wa kulia utaona bendera za nchi husika na ile ya Uingereza ikimaanisha kuna lugha ya kiingereza.

Unachofanya unagonga hapo na lugha inabadilishwa kutoka hiyo ya kigeni na kuwa ya kiingereza.
 
Changamoto ya hizi nchi zisizotumia Kiingereza ni kuelewa lugha yao kwenye website zao hapo hua naumiza kichwa sana
1. Hii tovuti ni ya Kiingereza.
2. Unaweza kusoma kwa lugha ya Kiingereza kwa baadhi ya masomo.

3. Kuna vyuo vinavyotumia Kiingereza peke yake Ujerumani, Norway na hata Japan.

Ukiwa na uwezo, the sky is the limit.
 
Hiyo nimepitia na imekaa vizuri kilugha, nimejaribu kwa vyuo vingine imegoma hata kutranslate

ubarkiwe mkuu
 
Wandugu Mimi nina shahada ya kilimo, nafanya kazi serikalini, nina miaka 3 kazini
Naomba kupewa link ya kusoma vyuo vya nje masters ya kilimo katika vyuo ambavyo hawahitaji mitihani ya English, maana mimi sijafanya hiyo mitihani.
 
Ingia hapa Swedish Institute Study Scholarships Application zinafunguliwa mwezi December, kwa mwaka huu tayari wameshatoa majina ya waliopata scholarship. Hizi ni za Sweden
 
Wandugu Mimi nina shahada ya kilimo, nafanya kazi serikalini, nina miaka 3 kazini
Naomba kupewa link ya kusoma vyuo vya nje masters ya kilimo katika vyuo ambavyo hawahitaji mitihani ya English, maana mimi sijafanya hiyo mitihani.
Kuna vitu vya muhimu uviandae Kabla ya muda wa kuomba kufika
1. Hakikisha una passport maana itahitajika wakati wa kutuma maombi
2. Kama hujafanya mitihani ya kiiengereza (IELTS/TOEFL) basi walau kidato cha nne uwe umefaulu English kwa kiwango cha B.
3. Wanataka watu wenye potential za kuwa viongozi, kwa hiyo hakikisha kwa namna moja uwe unajishughulisha na kazi zinazogusa jamii.
4. Uwe na watu watakaokuandikia recommendation letter (sio lazima walimu waliokufundisha)
5. Andaa Swedish Kronor 900(Hii ni kama 100USD) kwa ajili ya kulipia admission
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…