Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Check hii website inaitwa After school Africa kuna scholarships, intenships mbalimbali na various opportunities for African students
 
Nmepata mchongo wa kwenda japan na mwenyeji wangu kaniambia fursa za kazi kibao na nkifika natafutiwa mwanamke tunafunga ndoa napata kikaratas maisha mengine yataendela. Kwa mwenye uzoefu na inchi hiyo ningependa kujua mengi
Mh angalia Japan, usije ukaenda kujifunga.
 
tuonesheni wengine njia mkuu... hata kama ipo syria
Inategemea nchi gani unataka kwenda Ila Kwa Europe njia rahisi ni
unaweza kuapply viza ya Spain au Portugal (tourist visa)kupata kwake unaambatanisha barua ya kuonyesha kama umeajiriwa (unaweza ipata popote), hotel booking online incase haina invitation letter(booking ni bure), booking ya ticket ya ndege #bure#, ukipata unaweza safiri nchi zote za ulaya (Schengen) kasoro U.K
so unaweza amua kubaki au kwenda nchi nyingine unayotaka
Incase hujafanikiwa kupata visa pia kuna njia ya Georgia hii nchi haina visa na Tanzania unaweza ingia then ukachukua train mpaka Romania ambako ni karibu na Italy ukapiga mchongo wa kuingia italy ili uweze kwenda Germany or France or Swiss nk.
 
Huu uzi umesonga sana.

Kheri ya mwaka mpya wadau.

-Kaveli-
 
Watafutaji pia ingieni jukwaa la travel nairaland kule wana sticky nyingii za jinsi ya kujilipua namna ya kukabiliana na vikwazo vya kupata visa yaani wanajukwaa la travel lipo detailed sana kuanzia vyuo na nchi mbalimbali kama ijulikanavyo wale jamaa wapo kila kona. Waliopo nje wanatoa experience zao. Ushauri tu kwa yule anaetaka kweli kusonga huko.
 
shukrani mkuu kwa hizi taarifa ulizo ziacha.... zitabaki kuwa kumbukumbuku kwa muda mrefu... kukiwa na maswali zaidi, msaada wako kwa ufafanuzi una itajika...
 
Mkuu lusungo nitumie mwaliko basi na mimi nijilipue!! Shule ishaisha huku!
 
ngoja tuchimbe na huko.... sema tatizo la maraia wengi wa bongo... sio poa... hawataki kutoa njia, hawataki kuwa elekeza wenzao...

kuna video nili post jinsi wasyria wanavyo saidiana kuingia nchi za EU na wanavyo saidiana kupata passp' kwa wasio wasyria... na mambo kbao...

juzi kati nilipanda ndinga ya kutoka kampala kuja bongo... kulikuwa na madogo wa kiganda wana shuka SA... baada ya kumaliza skul na ajira home hamna... nika wauliza mmeaga home, wakanijibu yeah tumeaga, mna simu wakajibu hatuna tuna namba za simu za kuwa siliana na kaka yetu tukifika harare... na marafiki wengine... maana wame tuaidi kututafutia ajira huko ndio maana tuliweza kuondoka kwa kuaga...

walikuwa wana zinguana na ma utingo kwa kuwa hawajui swahili, wao ni kiganda na kizungu... kuna muda ina bidi kuwa saidia wanapo itaji msaada na ufafanuzi toka kwa wenye basi... walisafiri hivyo kwa purukushani, chakula chao ni mkate na maji na soda, maziwa kidogo...

hapa ndipo nilipo gundua dhana ya msafiri kafiri...!

nchi za africa waamiaji ni wengi sana tuna tafuta maisha bora na mambo mengine mengi... ndio maana una ona kila siku watu wana safiri kutoka eneo moja kwenda lingine iwe ndani au nje ya nchi... kwa sababu mbalimbali...

tusivunjane moyo... tusaidizane kupeana njia... na misaada mingine kama ina wezekana... lakini tatizo kubwa la wa tz ni kukatishana tamaaa na kujifanya wanajua hata kama hawajui... lengo ni kutaka kukatisha wengine tamaa...

pia wengi wao ni waoga, uoga wao wana jaribu kuupeleka kwa wengine na kusemaa au kuzani hwawezi kufanya jambo na kufanikiwa... ina sikitisha sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…