Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Mkuu inategemea unataka kwenda inchi gani kujilipua...zipo inchi zipo ulaya lakini utatamani ubaki Africa..sasa wewe nidokeze unataka uende inchi gani?

Acha uvivu ndugu yangu, kuna wakenya na wanigeria wenzako wanakwambia wakitua tu nchi yoyote ya ulaya wamewin tayari!! Haya niambie ni nchi gani ulaya kati ya alizotaja Lusungo ni sawa na Africa?? Acha watu wakatafute maisha nchi yenyewe hii Ngosha kakaba mpaka penalty na huku akisema waloshikwa wafungwe au wanyongwe tu, sasa kupi bora??
 
Halafu German ni super power Nchi za Umoja wa Ulaya. Yeye ndiye aliyebeba mzigo wote wa Euro Curency,
maana wakati hii Euro inaanza fedha yake ndiyo ilikuwa na thamani sana.
Kweli mkuu..na hata hyo euro y.. INASHUKA thamani sababu ya inchi kama Greece.. Na zinginezo masikini....kwnza hawa watu wanapenda sana raha kuliko kazi...wewe umeona wapi ofisi zinafungwa SAA saba wafanyakazi wanakwenda KULALA MAJUMBANI mwao halafu wanarudi tena ofisini SAA Tisa..wanatoka SAA kumi na moja... Greece ndy utaratibu wao wa kufanya kazi... Ile INCHI....inawabebesha wenzie mzigo wa madeni.tu
 
Mkuu wewe ushakaa ULAYA? nianzie hapo kwnza...halafu nikupe sifa za hao Nigerians na wakenya..huko majuu...
 
mulemule kumbe afya ndio dili ee ngoja nami nitasogea huko mkuu tujumuike wote nisaidie tu barua ya mwaliko niwe kama mgeni wako nikija nakuachia fungu kidogo natafuta njia yangu nami yakutokea by the way nami ni health personal.
Safi, hiki ndo tunachotaka....
 
Eti mkuu mtu unaweza kuwa considered kuwa ww ni expat wa madini kwakuwa a diploma holder from Tanzania kwenye nchi ulizozitaja hapo juu, au paka uwe na kiwango gani cha elimu ndo utakuwa considered kuwa expert???
 


Haha, mkuu Richard umenifurahisha hapo pa kuwa mweusi kama M Sudan ili upate uraia. Wengine wanadharau sana hiyo rangi kumbe inaweza kuwa the best kwa uhamiaji...lol

Lakini hili suala la refugees limekuwa pia gumu sasa worldwide, it's not that easy anymore. Hayo mashinikizo yanayowekwa sasa against refugees, from Brexit, to America first, to...God knows chaguzi zijazo za France and German kama zina muelekeo huo pia. It's mayhem.

Baadhi ya nchi kibano kwa wanaojilipua/wakimbizi pia kimekuwa kikali sana, na haijalishi ni mkimbizi wa vita, njaa au majanga ya dunia.
I don't think it was this strict before, lakini siku hizi naona watu wanavalishwa bracelets wakati cases zinaendelea, and once they're under the radar, they're not at peace.
Immigration officers walikuwa wanawa visit at least once per week, lakini sasa naona kuna watu wanatakiwa kupiga simu ku report every single day. Na uki miss kihama. Imagine huyo ni mkimbizi na familia, na huko alikotoka ni kihama pia.
 
Mkuu wapi nawwza kuishi nakupata kazi European country na Asian country na kuna urahisi wa kupata visa?
Mkuu mimi na wewe ni wamoja sote tunachukua maujanja hapa..

Siwezi kikwambia right place ni wapi kwenye assurance ya fursa, wewe cha msingi fanya kukusanya taarifa mbali kutoka kwa watu wenye uzoefu na hizi mambo kwanzia humu JF hadi huko mtaani, tena kama una machalii wako walioko mbele unapotaka kwenda ni poa sana ukiwa nao intouch au kama huna tafuta rafiki yeyote mtandaoni wa huko utapo taka kwenda na mtengenze mzoea hili upate kufahamu vingi kupitia yeye ila tu hakikisha awe loyal tena nakushauri tafuta rafiki msichana.


Mimi hiii piga,garagaza,chinja,ua,zika lakini lazima ikanyage Dubai kwa kina El Maamoud Salhel Jabir.
 
Ina maana blacks wanaweza aminika jeshini huko mbele mkuu? Mfano Norway wanaweza kukuchukua black?


Sina uhakika na Norway, but why not mkuu so long as una nguvu zako?
Kuna weusi, wa Africa, in some of the best militaries in the world.
 
Duuh.... Kwa huu ushuuda basi ile sehemu hapafai kuishi hata kima.
 
Duuh.... Kwa huu ushuuda basi ile sehemu hapafai kuishi hata kima.
Mkuu nimeshuhudia mwenyewe au itafute Madagascar na utamaduni wao ktk Google uta niamini mkuu...Mara ya mwisho kufika pale ni 2014...na ajabu ingine ukitoka airport unalipa airport fee kama dola 30 hivi...labda waitoe juzi...ww umeona wapi mambo hayo..kulipa pesa ya gharama za airport...
 

Huu uzi ni mzuri maana utasaidia wenzetu pia kimawazo na kifikra pia,mtu anaweza kujua wapi pa kuanzia Kama akitaka kusafiri,sema me naanza na hapo kwenye faida ulizopata,ni kweli faida ni nyingi sana ukitofautisha na bongo,lakin kaka sijaelewa kitu,umesema umeishi miaka 8 na umeweza kujenga ghorofa bongo na mashine,sasa me najiuliza mbona miaka 8 midogo sana??uliwezaje??au ulikuwa hauli vizuri??ulikuwa unajibana sana au ulikuwa unaishi nje ya mji(maana huko ndo kila kitu kinakuwaga poa,tofauti capital city au capital ya uchumi)???
Swali langu la 2,Kujilipua,sijaelewa kidogo hapo,unazungumzia kujilipua kWa aina gani??maana zipo nyingi sana,mfano kuna kujilipua kwa kujipa uraia wa nchi zenye vita ili kuomba hifadhi(mfano wa nchi,Somalia(watoto wa kinzanzibar wanajilipua sana na kujipa uraia wa kisomali,Eritrea,Africa ya Kati,Sudan n.k),au kujilipua pia kWa kuchana passport kWa ajili ya kuomba hifadhi Kama mtu ambaye hana uraia wa nchi yeyote ile,hiyo ni mifano tu na kuna wengine wanaweza ongezea,sasa kaka wewe unazungumzia ipi hapo??maana kutafuta mke mzungu kuoa na kupata karatasi,hiyo siyo kujilipua(mawazo yangu).
Kingine kwenye changamoto,naweza ongezea hali ya hewa maana sisi wengi tushazoea joto au jua kWa mwaka mzima lakin wenzetu kuna baridi sana baadhi ya miezi na kuna joto kWa miezi 4 tu katika mwaka,changamoto nyingine inaweza ikawa karatasi mfano Europe kila unachokifanya inabidi ufanye photocopy,unabaki na original unatoa copy na katika kila kitu utakachofanya na wakati kwetu siyo hivyo,wengine wanaweza ongezea.
La mwisho naweza ongezea pia hapo jinsi ya kwenda,unaweza pia kwenda nchi yeyote ya Europe kWa kisingizio cha kutaka kusoma lugha yao,kWa mfano ujeruman,unaweza ukatafuta chuo au center yoyote ambayo hipo ujeruman ambayo inajulikana na serikali ya ujeruman na ambayo inaweza kukualika kWa ajili ya masomo ya lugha yao ya Dutch,hao jamaa wakishakubali uwa wanakutumia barua ambayo inaonyesha ushajiandikisha katika chuo chao kWa ajili ya kwenda kusomea lugha,hiyo barua wanatuma pia ubalozi wa ujeruman Dar,so ukienda pale wanaweza kukupa visa ya kusoma,inaweza ikawa ya mwaka na ukawa unaruhusiwa kufanya kazi labda kWa masaa 20 kwa week(kihalali)na kuweza pia kufanya kazi masaa mengi zaidi ya hayo,ukapata sana mpunga lakini isiwe kazi ya kihalali,nikimaanisha black work(watu walioishi Ulaya na USA wanaelewa naongelea nini),baada ya hiyo visa unaweza omba card ya kuendelea kusoma kWa mwaka wa pili au unaweza mpata mtu mwenye uraia au resident permit akakuoa na maisha yakaendelea au ukapata kazi ya kudumu na ukaweza badilisha status kutoka kwenye uwanafunzi na kuwa na status Kama mfanyakaz,hapa wanaweza kukupa kabisa resident permit ukaweza kuvuta na ndugu zako wengine kupitia mgongo wako.
Jingine unaweza tafuta mtu mwenye uraia wa Ulaya au USA ukaongea naye,ukampa pesa mnafunga ndoa ya uongo,yeye anasimamia kila kitu mpaka unapata permit yako halafu anafanya divorce lakin anakuacha na permit yako,nafikiri wengine watakuja kuongezea,sema kaka naomba unijibu hilo swali langu hapo juu kuhusu kujilipua.
Shukrani sana[emoji1317]
 
Mkuu mbona hujaitumia mali hiyo.... Maana ukiwa na passport South Africa unakwenda kama tandika tuuu... Ni nauli yako
Mkuu ukaona upataje hapa gheto kabisa nlipolala(tandika) hehe
Hivi mkuu huko SA kuna fursa za aina zipi za kazi na ni miji gani mizuri kufikia? Ila si nliskia huko SA wanapiga wahamiaji, wewe hujaliskia?
Naiota sana japan na thailand ili nikifika huko niwe nafanya biadhara ya spare za magari(ukoo wetu umejikita sana kwenye magari na spare) na bidhaa za kitechnologia niwe nazisafirisha bongo ndo niko hapa nafikiria nitafikaje huko ikiwa ujuz nlionao ni wa computer science japo nataman niende nchi yoyote nzuri kutafuta maisha lakini hizo ndo first priority
Na vipi kuhusu turkey naona haijazungumziwa hata kidogo au walowah kufika huko ni wachache ndo maana taarifa zake hazijakua displayed hapa

Kwa kuongezea tu jana nliskia kwenye habari kuwa kampuni za denmark zinatafuta wafanyakazi yani kuna uhaba wa waajiriwa
 
Huko unakokwenda pia kuna matumizi, tena kama ni hizi kazi za unskilled labour utajikuta wewe ni mtu wa hand to mouth. Kinachoumiza sana ni kodi ya nyumba, watu wengi inabidi wafanye kazi mbili ili kupata pesa ya ziada.

Umesahau kuhusu cotisation za mshahara kWa mwezi,hapa utegemea na mshahara unaolipwa,sometimes unakuta mtu unakatwa mpaka 700€ kila mwez(hii kWa Ulaya),hapo bado haujalipa nyumba na bills zake,na haujalipa tax za makazi etc
 

Nafikiri hii system ni kwa ulaya nzima,maana nimeishi Berlin,Paris na Barcelona,flats zao zipo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…