Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Kweli mamtoni ni mamtoni tu.......kama una malengo na una nidhamu...hakika lazima utoboe iwapo utamtanguliza Mwenyezi Mungu.
utabadilika kuanzia muonekano mpako roho...lazima utakuwa na roho nzuri ya utulivu manake upo mbali na wachawi na washirikina,🙂🙂
 
Shukran sana kaka nakuunga mkono ikiwezekana naomba tuongee inbox 📞
 
Ingia deep kidogo .. toa sababau za kwanini tusio wazungu?
 
mkuu salaam.

Mkuu kitaaluma ni IT, kwa maana bachelor degree nimefanya Computer Science, ila pia ni am holding professional certifications mfno CISA, CISM n.k, na kwa sasa nafanya kazi taasisi kubwa tu ya serikali, lakini nimekuwa na ndoto kubwa sana hasa kwa kipindi hchi na hamu ya kuja kujaribu maisha nje ya nchi, kama ikikupendeza mkuu naomba msaada hata kuni connect au kunipa abc vzr niondoke bongo..ila pia kama uwezekano wa kuajilika kirahisi ili nikiondoka nisianze kuteseka sana. mwisho pia kama kuna platform zinatoa michongo inayopatiana kirahisi. nitashukuru sana.
 
Kitu cha kwanza kama una jamaa au rafiki asiye mchoyo ni rahisi kukupa michongo na maisha jinsi yalivyo huko majuu bila janjajanja ila kitu cha muhimu doc zote ziwe sawa zisipishane, mpunga ni jambo muhimu sana aisee katika mambo ya kwenda mbele
UZI TAYARI....👍
 
Mimi nataka niende Scandinavian Countries au Canada. Kama kuna mtu ana connection anijuze.

 
Website zipo nyingi ila Cha kwanza kufika huko
 
Kwa wale watu mnaopenda kwenda nje ngoja niwawekee link ya jamaa fulani hivi yupo Ubelgiji nadhani huwa anafundisha njia mbalimbali za kufuata ili kusafiri kwenda kwenye nchi mbalimbali.
Lengo la jamaa yeye ni kuwafundisha watu wafunguke njia za kujisafirisha wenyewe bila kutumia MaAgent au bila kumlipa hela mtu yeyote maana kuna watu wengi wanapigwa sana hela zao kwa sababu ya kutoelewa process.

View: https://vt.tiktok.com/ZS6nc7FUS/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…