Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Kweli mamtoni ni mamtoni tu.......kama una malengo na una nidhamu...hakika lazima utoboe iwapo utamtanguliza Mwenyezi Mungu.
utabadilika kuanzia muonekano mpako roho...lazima utakuwa na roho nzuri ya utulivu manake upo mbali na wachawi na washirikina,🙂🙂
 
Binafsi uzi huu nauunga mkono 100% Lakin pamoja na hayo bado kuna changamoto nyingi kufikia hatua ya kuondoka nchini, kuna mambo mengi ambayo niya msingi hasa upande wa Serikali yetu tukufu hasa upande wa Idara ya uhamiaji.

Tz yetu mtu kupata the tu cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki ya Mzawa mpaka jasho likutoke, na ikiwezekana na rushwa juu utoe. Ukienda Migiration ili kuanza mchakato wa passport utahenya vibaya.

Kupata card ya chanjo ya homa ya manjano mpaka utahenya.

Lakini pia changamoto nyingine ni mtu kupata Nauli kamili ya kukufikisha mahari unako taka kwenda. Binafsi ninacho elewa wakirahisisha hayo mambo ya juu, naona Tanzania inaweza kubaki na wazee tu.

Sasa nchi gani hii isiyo toa ajira, Mali asili ni nyingi lakini hatujui wala hatuoni uthamani wake, Vyeo vya juu wanapeana wao kwa wao

HAKI YA MUNGU MIMI SIKU NIKIONDOKA NDO BASI TENA. BORA NIKAFIE KWA FARAO KULIKO KANANI AMBAKO SIJAWAHI FIKA.
Shukran sana kaka nakuunga mkono ikiwezekana naomba tuongee inbox 📞
 
All the best, ukifanikiwa usioe mzungu, iko hivi ndoa ya mzungu mwanamke na mwafrika (mwanaume) hazidumu ni mateso lakin ndoa ya mwafrica mwanamke na mzungu (mwanamke) ni raha mseleleko.

Kaka zetu walio oa wazungu ndo wana majibu hiki nilichokwambia.wachache sana wana furaha.

Rafiki yangu yupo US katoka kunipigia muda sio mrefu anajuta kuoa mzungu pamoja na pesa alizo nazo bado hana furaha. Anakuja tz kutafuta mwanamke hata kama hajasoma.

N.b wadada walioshindwana na kaka zetu bongo tafuta mzungu hutojuta.
Ingia deep kidogo .. toa sababau za kwanini tusio wazungu?
 
karibuni Basel (uswizi)...ila huku ukitaka kula nchi uwe umepiga shule...niko swiss tropical inst....

....ulaya imekua chungu sana kwa waosha vyombo na wazamiaji....maana sharia za nchi za ulaya zimekua tight sana ...maana wana monitor terrorism....maana kumejaa waarabu ulaya....

.....sasa hivi ukitaka kuula....nenda shule tu....ili ukubalike kokote....

....Btw.....home is always better.....singewashauri watu wawe na mtizamo wa kukimbilia ng'ambo....kwani bado kuna ubaguzi mkubwa wa kimfumo(institutional racism).....kwa hiyo ni bora nyumbani TZ....ni bora kubanana nyumbani kuliko ng'ambo....

..madada zetu wengi wanaishia kupiga umalaya ng'ambo...na wanapigwa hadi nyuma...kisa eti maisha bora!!kuuza utu sababu ya maisha bora!!....ama kuoshea wazungu vyoo!!...no please....
mkuu salaam.

Mkuu kitaaluma ni IT, kwa maana bachelor degree nimefanya Computer Science, ila pia ni am holding professional certifications mfno CISA, CISM n.k, na kwa sasa nafanya kazi taasisi kubwa tu ya serikali, lakini nimekuwa na ndoto kubwa sana hasa kwa kipindi hchi na hamu ya kuja kujaribu maisha nje ya nchi, kama ikikupendeza mkuu naomba msaada hata kuni connect au kunipa abc vzr niondoke bongo..ila pia kama uwezekano wa kuajilika kirahisi ili nikiondoka nisianze kuteseka sana. mwisho pia kama kuna platform zinatoa michongo inayopatiana kirahisi. nitashukuru sana.
 
Kitu cha kwanza kama una jamaa au rafiki asiye mchoyo ni rahisi kukupa michongo na maisha jinsi yalivyo huko majuu bila janjajanja ila kitu cha muhimu doc zote ziwe sawa zisipishane, mpunga ni jambo muhimu sana aisee katika mambo ya kwenda mbele
UZI TAYARI....👍
 
Mimi nataka niende Scandinavian Countries au Canada. Kama kuna mtu ana connection anijuze.

 
Mimi nataka niende Scandinavian Countries au Canada. Kama kuna mtu ana connection anijuze.

Website zipo nyingi ila Cha kwanza kufika huko
 
Kwa wale watu mnaopenda kwenda nje ngoja niwawekee link ya jamaa fulani hivi yupo Ubelgiji nadhani huwa anafundisha njia mbalimbali za kufuata ili kusafiri kwenda kwenye nchi mbalimbali.
Lengo la jamaa yeye ni kuwafundisha watu wafunguke njia za kujisafirisha wenyewe bila kutumia MaAgent au bila kumlipa hela mtu yeyote maana kuna watu wengi wanapigwa sana hela zao kwa sababu ya kutoelewa process.

View: https://vt.tiktok.com/ZS6nc7FUS/
 
Back
Top Bottom