Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Nimefight Sana kuingia uk, usa tangu 2009 nimefail, nimejaribu njia zote mpaka 2012 nikaenda burundi kujaribu kuondokea kule kama mrundi niingie belgium then nizame uk but nkafail...mwaka jana nimerusha kete yangu usa niingie kwa program ya mast nipate j1 visa nimetoswa nayo nshajikatia tamaa but uzi huu unataka niamsha tena nianze michakato..kuna mtanzania flan alijifanya kunisaidia niingie kwa bibi ye yupo coventry uk akaniliza pound 1300... wabongo wengine njaa kali majuu
 
Ok Mkuu
Ila sijaamini bado kuwa Italy fursa kuu ni ngada

Ni ngada kaka,wabongo wote % kubwa waliko italy ni ganda tu,ila kama uko smart kuna biashara za nguo viatu labda hizo uchukue huko ukauze bongo lkn ajira brother watu wanakimbia huko kila siku hakuna ajiri na mtu ni citizen kabisa lkn no job uchumi umeyumba sana Italy kama grace tu
 

Lithuania inapakana na Poland na poland inapakana na Ujerumani,Isitoshe Poland ipo Muungano wa Ulaya.
Toka hapo mbele kwambele .

Au pale Estonia anachukua ferry Tallin to Helsinki , ni kama dar to zenj.
 

Nimeshtuka sana!
Kuna ndugu zangu kule wamekaa zaidi ya 20 years nahofia wasijeishia jela kwa mtaji huo
 

Acha kukatisha tamaa watu aisee,ukiwa na uraia wa nchi moja ya Ulaya,unaweza fanya kazi nchi yoyote ya ulaya,me na mwanangu Ana uraia wa kireno na kWa sasa anapiga kazi france bila tatizo lolote,tena anatumia uraia wake wa ureno
 
mkuu tumia njia ya kujitolea,pitia workaway.info...hii njia ni guarantee maana humpi mtu pesa mkononi..
 
Nataka kweda south Afrika kusoma Radiography kwa alie South afrika anipm au mnisaidie jamani sina mwanga kabisaaa
 
Acha kukatisha tamaa watu aisee,ukiwa na uraia wa nchi moja ya Ulaya,unaweza fanya kazi nchi yoyote ya ulaya,me na mwanangu Ana uraia wa kireno na kWa sasa anapiga kazi france bila tatizo lolote,tena anatumia uraia wake wa ureno

Sawa ila mimi naongea kitu ambacho nakijua hata mimi ni raia wa sweden lkn nafanya kazi Norway,Je unajua ni proces zipi unafuata ili upate number ya kulipia TAX? Mie siongei mambo ya vijiweni wala sina haja ya kumtisha mtu yoyote, kwa taarifa yako Europe kila nchi ina sheria zake na hata nchi kama sweden japo iko kwenye European union lakin hata hiyo euro haitumiki hapa.watu wengi wakiwa ulaya tatizo hawasemi ukweli ili watu wajue mzee
 

Pale ni mchanganyiko wa Asia kaka,kuna wa Pakistan pale,kuna wa Afghanistan,wa hindi,wa China,etc na kuna weusi wengi tu ambao walienda kupigana vita kipindi kile cha ukoloni na france ambao inasemekana asili yao ni Senegal,sema asilimia kubwa wanawake wao ni wazuri sanaa na bei nafuu sana kuwapata,kWa mfano unaweza ukapata mwanamke mzuri kWa buku 10 ya kibongo,buku ni nyingi sana pale,walimu tu wanalipwa elfu 25 kWa mwez ambayo ni sawa na euro 10,kile kisiwa maskini sana lakin inaweza ikawa njia pia ya kuingia reunions na kuanzia maisha hapo,ukipata permit ya reunions unaingia france bila visa,nauli yako tu
 
Najua kuna wabongo wanasoma south afrikaaa nisaidieni jamanii nijapange kivipi kipesaaaa applications na mambo mengine ya msingi japo kiufupiiii utanipaaa mwangaaaaaa msaaada tafadhariii mwakani mwezi wa kwanza mungu akijalia niwe hukoo
 
ha
Ahsante mkuu kwa kuni tag. Ebu nipe uzoefu kuhusu jamaica yaweza kuwa rahsi pia. Kama unauzoefu. Kuna dada wa kijamaica kaniganda kama kupe na anakomaa niende huko
hahaha, mavumbini πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Najua kuna wabongo wanasoma south afrikaaa nisaidieni jamanii nijapange kivipi kipesaaaa applications na mambo mengine ya msingi japo kiufupiiii utanipaaa mwangaaaaaa msaaada tafadhariii mwakani mwezi wa kwanza mungu akijalia niwe hukoo

Falcon Mombasa
 
Lithuania inapakana na Poland na poland inapakana na Ujerumani,Isitoshe Poland ipo Muungano wa Ulaya.
Toka hapo mbele kwambele .

Au pale Estonia anachukua ferry Tallin to Helsinki , ni kama dar to zenj.

Sawa unachukua crusing ship boat za kula raha huko ndani ni jehanamu lkn sasa kutoka humo ukanyange ardhi ya helsink mzee mbinde wala sio tallin tallink na kuna vikingline pia security ni kubwa kutokana na issue za ugaidi jamaa wako makini.ni bora utafute tourist visa kwa nchi amabayo unataka kwenda ukifika huko ndio unazama mazima sasa mpk kieleweke lkn border to border utahagaika saana
 

Me siongei mambo ya kijiweni ndugu yangu,Scandinavian kidogo kuna sheria haziingiliani na Europe angalau pia wapo umoja wa ulaya na ndo mana hawatumii euro kama nchi zingine,wao Kama wamejitenga,lakin ukiwa na uraia wa ulaya wa nchi zinazotumia euro unaweza ingia nchi yeyote ya ulaya inayotumia euro na ukafanya kazi bila masharti yoyote yale,kWa mfano ukiwa una uraia wa ureno,Italy,hispania,ufaransa,ujeruman,belgium,uholanzi etc,hawa wanafanya kazi pamoja(umoja wa ulaya).
 
Kuhusu kuingia Jeshi lazima uwe na permit hata ya mda mfupi(mwaka 1)Kama hauna hauwezi ingia ndugu zangu,na hauingii jeshi kabisa,hapana unaingia jeshi la wageni ambao mnakuwa wengi sana na wengine kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Africa,Asia pia na Europe wanakuwaga wachache,lakini pia ni kweli unakuwa na mkataba wa miaka 5 baada ya hapo unaomba uraia wanakupa bila tatizo lolote na kazi unakuwa hauangaiki,unapata kiraisi sana maana wanakuwa wanakuamini na unakuwa na vyeti ambavyo umesomea ulivyokuwa katika Hilo jeshi la wageni,kumbukeni hili jeshi pia ndo wale migambo wanaotangulizwa mbele wakati wa vita na wanapelekwa kwenye nchi zenye vita Kama Iraq,Syria,Libya, n.k,so usipokufa katika huo mkataba wako wa miaka 5 ndo umeyatoa maisha sema wengi wanakufaga,wengi wakimaliza hiyo miaka 5 wanakuwa vilema na madhara mengi sana,lakin maisha pia ni Risk,ukiamua umeamua Lakin hauwezi ingia katika Hilo jeshi Kama hauna Permit hata ya mda mfupi(mwaka 1).
 

Kaka hujui unachokisema mie Nina mshikaji wangu ana uraia wa italy lkn kazi imeshidikana sweden,pia upatikanaji wa kazi hapa ulaya sio kama bongo ujue kwanza hiyo kuna agency ya serikali kila nchi amabyao inashughulika na kukutafutia kazi wewe mkazi wako radhi wakulipe hela hata kama huna kazi wkt wanakutafutia kazi na hata wanaweza kumwambia mwajirj akupe kazi akulipe 20%tu ya mshahara na 80% wanakulipa wao.sasa,kuhusu kutumia euro hiyo sio hoja italy wanatumia euro je mtu amaweza kutoka italy akafanya German?je unajua kila nchi hapa ulaya wana lugha yao?mzee mie niko ulaya huu mwaka 24 kabla ya hapa nimekaa saana German,Italy,Finland na huko kote nilikua natafuta maisha najua sheria za hawa jamaa sikia tu story za vijiwen siku ukifika ndio utajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…