Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

kaeni nyumbani muijenge nchi yenu. nyie mnaikimbia wakenya,wazimbabwe,wamalawi ,wazambia,wachina na mataifa kibao wanaingia.
 
Kwa kuanzia tu mi naona nataka nitoke na hii ya kupata Mwenza hebu funguka njia ya kuweza kupata weza pengine kama kuna sites online nijilipue kwa njia hio
 
Njia rahisi ni kupitia Nairobi Kenya coz Dar hawana embacy Ila visa yao ni very easy kuipata.

Kwa Afrika Malta wana ofisi za ubalozi katika nchi za South Afrika (Durban na Cape Town), Egypt (Alexandria na Suez), Nigeria (Lagos) na Tunisia. (Tunis)
 
Kama ni kenya si wakupe ndogo ile karatasi na picha juu. Ila ndo hivyo kaka tafuta namna ujianfikie hiyo invitation letter mwenyewe, ingia net sample kibao,
tatizo mihuli ndio shida mkuu halafu kuna jamaa aliandikaga humu kwamba sasa hivi mipakani hawatoi zile temporary passport kama zamani.
 
Sio lzm kwenda nje, Tz kuna hela za kufa mtu we became millionaires by being here

How did you do that ?

Mimi nimeanza na kuchoma chips hapa Kwamtogole na nina kamgahawa kadogo, lakini hali ni tete sana.

Tupe uzoefu wako, ulitokaje?
 
Waliofika zamani huko wakt uchumi uko vizuri nao wako vizuri,ila kwa hii miaka 5 hali mbaya kaka
Duu...yaani ndy kuwa VIZURI kule?hao ndugu zako wapo ofisini?au mitaani?hyo zamani mwaka gani?mm nimekaa 2013 ...2014....mdomo huo ufute....kwahyo wale wapo VIZURI kuliko bongo?au ndugu yako alikuletea kiatu na pesa basi unajuwa anafanya kazi ofisini? Au unajuwa alipo kuna maisha mazuri?MKUU pabaya pale.....nenda ukajionee...usione ndugu yako kanitumia pch ya sehemu Fulani Fulani.....
 
Sio brittanicca huyu kweli ...
Mi nimeapa sintokaa nitapeliwe kamwe.
Mtu anakuja humu anajifanya anajua sana maisha ya nje ama anajua kwenda njia za kufanya kwenda nje ya nchi...ili avutie watu ukiingia kingi unaachwa kwenye mataaa kama yale ya ubungo...
 
Moja ya Comment bora kabisa
 
ndoto zangu nikwenda US hata ushamba boy au kuzoa taka me ntaanza nao ntawezaje kufika huko mkuu
 
Moja ya Comment bora kabisa
Mkuu, bongo mtu anakubania bila kisa bila sababu, yaani hapendi tu kuona unafanikiwa, si bora kungekuwa na jambo akikubania wewe anapata yeye, hamna, anakubania akijua hunufaiki chochote. Wapo vijana wengi sana wamekwama kwa kubaniwa kwa staili kama hiyo.

Unakuta mtu amepata admission, wakati wakuomba scholarship unatakiwa upate barua ya employer kuthibitisha amekubali uende ukalr nondo, hr gani kwa bongo atakuandikia hiyo barua? Huipati miaka 200.

Mm najiandikia mwenyewe employer statement, logo ya kampuni ninayo, contacts naweka zangu mwenyewe (nina namba kama nne hivi, huku nakuwekea voda hapa nakuwekea airtel). Michakato inaenda. Ukizubaa tu bongo umeliwa. Majitu yana roho mbaya kama kitugani sijui
 
Mkuu we mbayaaaπŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚.Mimi mwenyewe siku hizi naandaa kila kitu nikifika pale namsomesha HR anisainie tu, ukisubiri akuandikie barua utakesha.
 
Mkuu we mbayaaaπŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚.Mimi mwenyewe siku hizi naandaa kila kitu nikifika pale namsomesha HR anisainie tu, ukisubiri akuandikie barua utakesha.
Huyo wako ana nafuu, wengine wakijua unataka kusepa tena kwenda mbele kujiendeleza anapata uoga na kinyingo. Hatakiwi kujua akijua anakutengenezea zengwe manake anajua ukiwa nje ya system ngumu kutafuta ugali na kufight haya mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…