Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Wewe njoo ujaribu hiyo number 4 huku UK uone kama hukuishia jela. Wenye nchi yao wameshaamka na wanaujua ujanja huu ndani nje. Siku hizi kuoa huku sio process rahisi kabisa.
Mkuu kwahiyo badala ya namba nne nini kifanyike? Tueleze ndicho tunachohitaji...

Hii ni kwaajili ya wengine si mimi maana kwa umri na nilipofika pananitosha.
 
Mkuu kwahiyo badala ya namba nne nini kifanyike? Tueleze ndicho tunachohitaji...

Hii ni kwaajili ya wengine si mimi maana kwa umri na nilipofika pananitosha.

Kwa sasa mimi sina ushauri kwa sababu mimi kwanza niko huku miaka mingi sana na sikujiripua, nilikuja kwa aina ya visa ambayo kwa sasa imefutwa, nilifanya kazi katika kampuni moja kwa miaka miwili na kwa bahati nzuri na kupendezewa na uzoefu wangu na uchapaji wangu wa kazi kampuni yangu iliniombea kuongezewa muda wa kuendelea kufanya kazi nao na nikakubaliwa. niliongezewa miaka 2 na niliombewa kuongezewa muda mara tatu na zote kukubaliwa na ghafla tu nikajikuta nimeshafanya kazi huku kwa miaka kumi na nikaweza kuomba indefinite leave, visa ambayo ndio niliyo nayo hadi sasa. Kama nilivyosema nimekuja huku zamani, wakati ule ilikuwa ni rahisi sana mwanafunzi kijana kutoka common wealth country kupata visa ya work experience na ilikuwa rahisi mno kuweza kuongezewa muda endapo kampuni ufanyayo kazi wakikupenda na kukuombea muda zaidi wa kukaa wakisisistiza ni namna gani wananufaika na utendaji wako wa kazi. Kwa ufupi nilibahatika kupata nafasi katika kampuni nzuri tu.

Kwa vile nimefanya kazi miaka mingi huku ndio nikasema kuwa ujanja wa ndoa za uongo ushagundulikana na watu wengi tu wamejikuta jela. Wapo wanaofanikiwa lakini ni wachache na siwashauri kufata njia hii.
 
Yote ya yote wabongo muda mwingine tunawakatisha waliopo mbele kutusaidia. Unakuta unamsaidia mtu mwisho wa siku anakuibia au anafanya mambo ya kishenzi mbele na wewe mwenyeji wake unabakia kulaumiwa . Huu ni upuuzi ni kuwaharibia wengine wanaohitaji misaada kama hiyo. <br /><br />Ila wito wangu. Kwa walio mbele binadamu wanatofautiana. Kosa la mmoja lisiwe la kufanya ushindwe kusaidia kiumbe kingine chenye roho ya ubinadamu kisicho na hatia. Naamini kuna ambao wanasaidiwa na wanafanya vizuri. All in all nikuwa makini tu hasa kwenye kumjua unamsaidia ikiwezekana uwe na baadhi ya docs zake.
Yeah, mkuu. Wanajua mtu ukifika ughaibuni hela uNaokota tu, sasa pale anavyo ona ndiyo sivyo ana amua kuaribu, unarudi kutoka kazini utakuta chumba kimesafishwa. Na ulaya ya sasa tofauti na yazamani, hali ya kiuchumi imebadirika duniani kote, kwa hiyo tunaenda kutafuta maisha, tuwe na negative mind, inaweza kutujenga kisaikolojia, pindipo pale mambo yanapoenda kinyume na matarajio.
 
Hahhahahahaha.... watu wamekata tamaa mno... hii hatari sana mkuu... hispania watu wanapungua wanaitaji ongezeko la watu watu ni mtaji ni rasilimari wewe una sema watabaki wazee (hahahahhahahaha....)
Binafsi uzi huu nauunga mkono 100% Lakin pamoja na hayo bado kuna changamoto nyingi kufikia hatua ya kuondoka nchini, kuna mambo mengi ambayo niya msingi hasa upande wa Serikali yetu tukufu hasa upande wa Idara ya uhamiaji. Tz yetu mtu kupata the tu cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki ya Mzawa mpaka jasho likutoke, na ikiwezekana na rushwa juu utoe. Ukienda Migiration ili kuanza mchakato wa passport utahenya vibaya,

Kupata card ya chanjo ya homa ya manjano mpaka utahenya.

Lakini pia changamoto nyingine ni mtu kupata Nauli kamili ya kukufikisha mahari unako taka kwenda.
Binafsi ninacho elewa wakirahisisha hayo mambo ya juu, naona Tanzania inaweza kubaki na wazee tu,
Sasa nchi gani hii isiyo toa ajira, Mali asili ni nyingi lakini hatujui wala hatuoni uthamani wake, Vyeo vya juu wanapeana wao kwa wao

HAKI YA MUNGU MIMI SIKU NIKIONDOKA NDO BASI TENA. BORA NIKAFIE KWA FARAO KULIKO KANANI AMBAKO SIJAWAHI FIKA.
 
kama ni wanafunzi ni rahisi sana kupata na wale wanao omba offer letter online pia una pata as an attachment ya kuomba si zani kama kuna ugumu kama utaomba kwa academic issues ila kwa mambo mengine ni mlolongo wa serikali za mitaa kwenye kitu kidogo au kama ni mfanyakazi wa kanisa pia ni rahisi kupata... jambo la msingi kupata hii pass ni kuwa na sababu wao wanachotaka ni sababu na unaweza chukua ile form na ukawa unaijaza taratibu upatapo nafasi huku ukiwa unatafuta viambatanishi vyake... naimani unafanikiwa katika hilo... sababu zipo ndio maaana hata ukisoma kwenye mada pale juu wanasema wakenya na nigeria huwa wanatumiana barua za mualiko hii ina msaidia kupata visa na pass pia na huku kwetu inaitajika pia uwezi ruhusiwa kwenda nchi ya watu ukawe mzururaji....
Mkuu ni kweli... Uhamiaji hawatoi passport bila reason.... Nafikiri tungebadili huu utaratibu tuwe kama wenzetu ambao passport kwao ni haki ya msingi na unaweza miliki tu.
 
Wangefanya hivyo.siku nyingi ningekuwa sauzi.walinipa form zao zile.zina maswali hatari.zikazichoma moto.
ungetafuta mtu akusaidie usikate tamaa mapema... mimi nilianza tafuta nikiwa sekondari nilishindwa vigezo vingi nikajaribu tena nikashindwa mara ya tatu rafiki yangu alitoka likizo UDSM nami nimetoka likizo nikamwambia kuhusiana na pass akanieleza utalatibu mpaka yeye alivyofanikiwa na mimi nikiwa mwaka wa mwisho nikafanya vile so ikawa namaliza chuo na pigiwa simu kuchukua mzigo wangu....
 
  • Thanks
Reactions: kpi
Kwl mkuu...miaka hiyo ya 90 ilikuwa Tanzanian passport holder unaringa tu.. UK....SCANDINAVIAN.. countries.... Tunaingia tu entry..wakawa wanakuja wasomali na wahindi hata Nigerians wanapewa passport wanaingia ..tu.ulaya...kibaya zaidi Nigerians wanabebea MADAWA... na wahindi na wasomali wakifika tu Airport wanaongoza REFUGEES DESK...wanasema mm ni msomali au muhindi. nimenunuwa passport Tanzania...naomba UKIMBIZI....ndy chanzo cha wazungu kukasirika...tukaekewa VIKWAZO CHA VIZA...inchi hizo...nina maana yote ni sababu ya PASSPORT kuwa ZINATOKA kama NJUGU
Nyerere alitupa kaeshima kidogo kipindi hicho tukaonekana na sisi tuna dharau kumbe tuna hitaji....
 
Kuna mtu nimeona anaulizia Agent, kuna mzee namfahamu kapeleka jirani zangu wengu uswizi na ndie najaribu kujipanga anipeleke. Ila bajeti yake ni $4000. Km yupo agent mnamjua ambaye ni cheap kiasi naomba tupeane connections
 
Kama anakufanyia na mpango wa long stay visa kabisa nenda hiyo hela ni ndogo but kama ni kwenda tu mengine ujijue mwenyewe hiyo hela kubwa usimpe.
 
Wekeni contacts za hao watu ili watu waweze kuwasiliana nao wenyewe na wajiridhishe pia
 
  • Thanks
Reactions: Qj_

Uswisi tuu, au nchi yoyote? leta info zaid
 
Yeah, mkuu. Wanajua mtu ukifika ughaibuni hela uNaokota tu, sasa pale anavyo ona ndiyo sivyo ana amua kuaribu, unarudi kutoka kazini utakuta chumba kimesafishwa. Na ulaya ya sasa tofauti na yazamani, hali ya kiuchumi imebadirika duniani kote, kwa hiyo tunaenda kutafuta maisha, tuwe na negative mind, inaweza kutujenga kisaikolojia, pindipo pale mambo yanapoenda kinyume na matarajio.

najua yooooooote hayo, saikolojia yangu ya huu ubongo nimeshautrain kutochukulia vitu rahisi rahisi, i did not expect hayo uliyoyasema.
 
Kama anakufanyia na mpango wa long stay visa kabisa nenda hiyo hela ni ndogo but kama ni kwenda tu mengine ujijue mwenyewe hiyo hela kubwa usimpe.
Ukifika baada ya muda unajisalimisha polisi unaomba hifadhi ya ukimbizi
 
Wekeni contacts za hao watu ili watu waweze kuwasiliana nao wenyewe na wajiridhishe pia
Brother nadhani tahitaji ruhusa yake, ila kapeleka watu zaidi ya kumi naowafahamu na wameshaishi huko km miaka kumi sasa
 
  • Thanks
Reactions: Qj_
Alipiga mbizi na mkopo.... hatari
Njoo basi inbox tuongee.

Kuna jamaa yupo korea. Alichukua mkopo ofisini kwake akapotea ila alipofika ikabidi ajirudi aombe msamaha akaulipa
 
Back
Top Bottom