Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

africa mashariki unaenda wanakupa karatasi ya muda kukupa kubwa ni ngumu sababu una safiri east africa ambayo kuna pass ndogo inatumika... na hii kuipata haizidi wiki wiki mbili ukitimiza vigezo...
Dah mkuu embu nielekeze hayo maujanja yako ili kesho morning tu nitie maguu migration coz nasafari ya kenya halafu migration wanizingua tu.
 
kwasisi wenye elimu ndogo mnatusaidiaje au sisi ndio tubaki hapa kuwalindia nyumba jamani,tukifika huko tutajiongeza tu maana hapa kwetu ndio hivyo mpaka tuibe vyeti wengine uwezo huo hatuna tupeni basi mbinu za kuvuka hapa
 
Bado Hauna TIN na unaitajika ukalipe kodi mkuu kwa biashara unayoifanya....
How did you do that ?

Mimi nimeanza na kuchoma chips hapa Kwamtogole na nina kamgahawa kadogo, lakini hali ni tete sana.

Tupe uzoefu wako, ulitokaje?
 
Alaf passport. Nilipoona masuala ya cheti cha kuzaliwa cha mzazi.hapo ndo nilichoka.sasa tunafanyaje kuipata.ya 50,000.ila naomba usiwe kama britanicca tu. 😀 😀 😀 😀 😀 😀
Aah mkuu mbona jambo rahis sna unaenda kula kiapo tu maakaman nakumbuk ile karatas ni 2000 tu pamoja na stamp
 
Hivi kwa mfano umefanikiwa kwenda na umejilpua je siku umeamua kurudi nyumbani na hapa pia utasumbuliwaaa au la
 
hahaha, mkuu nimecheka sana😀😀😀
kwasisi wenye elimu ndogo mnatusaidiaje au sisi ndio tubaki hapa kuwalindia nyumba jamani,tukifika huko tutajiongeza tu maana hapa kwetu ndio hivyo mpaka tuibe vyeti wengine uwezo huo hatuna tupeni basi mbinu za kuvuka hapa
 
anaenda mzazi kula kiapo au unaweza kuenda hata mwenyewe bila mzazi.
Kma yupo vizur uende nae ila kama hayupo just wewe unataka kukamilisha requirement tu so unaweza kuongea na wahusika wakakufanyia urahis kwan hakuna kikubwa ni karatas tu ya kiapo na mhuri na stamp kwisha kaz
 
Kma yupo vizur uende nae ila kama hayupo just wewe unataka kukamilisha requirement tu so unaweza kuongea na wahusika wakakufanyia urahis kwan hakuna kikubwa ni karatas tu ya kiapo na mhuri na stamp kwisha kaz
asante sana hapa uminionesha njia mkuu.
 
Ndugu zangu jana nilitoa list ya balozi ambazo unaweza kuomba visa ya Malta kwani nchi ya Malta ina balozi chache sana kwa nchi za Africa balozi zipo Africa ya kaskazini so wanachofanya kuna balozi ambazo unaweza kuomba visa ya Malta kwa Tanzania ni balozi ya Italy ndio unaweza pata visa ya Malta njia ya kwenda Malta ni tatu kusoma,kutalii,kutembea hii inahusisha kufanya kazi kwa kujitolea ambapo yule unayefikia kwake anakutumia barua ya mwaliko

Kama unakwenda kwa ajili ya kufanya kazi ya kujitolea mara nying ni kazi za mikono ambazo unatakiwa kuwa unazijua ni
1 ufundi wa mbao au saidia fundi
2 kuchunga na kuangalia wanyama {mifugo}
3 kupika hii ni kwa wanawake
4 kutunza watoto hii ni kwa wanawake
5 kutunza bustani hii ni kwa wote

Napendekeza kama kazi ya kujitolea ukafanye kijijini au kwenye miji midogo faida yake ni
1Kwanza utajua Lugha zaid ya moja yani lugha ya wenyeji
2 unakuwa unaply low profile{kwani watu ni wachache na wengi ni wazee ambao mala nying hawana mpango na mtu}
3 Ni vyepesi kupata mdhamini wa kukuombea uraia endapo utakaa mwaka mmoja
4 Wengi kule ni wazee so mzee siku zote wanaaminika sana kwa serikali na taasisi zake so kama akikuombea uraia process zako zitakuwa fupi tofauti na akikuombea kijana

Vijiji na miji ya Valletta,Mdina, Zabbar,Cospciua na st paul"s bay

Wale wakina John kisomo kule scholarship nyingi ni kwa level ya masters na PhD ambazo nying ni za serikali BT ninazo scholarship za Sweden,Canada,Denmark , Australia ,Austria ,Germany , Finland, NZ lakini nying ni Masters na PhD lakini mission yetu ni Malta so tunajikita kwenye Malta

Note ; ni uhakika kama ukifanikiwa kukaa ndani ya MALTA mwaka mmoja kupata uraia ni vyepesi na ukifata process zote utafanikiwa lakini pia Mungu ni wa kumuomba kwa kila jambo pia

Kama utafanikiwa nchi za kwenda kwa ulaya ni za Scandinavian country na Ujerumani,Canada, USA kwa sasa hakuna free visa kwa nchi za ulaya mpaka pale watakavyobalisha Luxembourg nchi ambazo usiende kwani ni kimeo ni Italy,Spain, Ufaransa kwani kazi hakuna na maisha ni magumu UK wamejitoa EU so sidhani kama kuna free visa


kuhusu jeshi nilishazungumzia labda kama kuna swali naweza ulizwa

Kumbuka jeshi la wenzetu mafunzo si magumu sana kama huku kwetu najua wengi wanaweza ogopa kutokana na mafuzo huku ni kukomoana kule ni kufundishana majeshi ya wenzetu wamewekeza kwenye technology si katika nguvu za mwili mambo ya kuvunja matofali au kuvuta gari kwa meno hakuna labda uwe kwenye vikosi maalumu kama special force na commando wenzetu siku hizi ni kubonyeza botton tu vinatoka vitu mpaka sijui mkutane mpigane mieleka siku hz hakuna room hiyo siku hiz zinatumwa spy UAV{Unmanned aerial vehicle} inapiga picha jion pilot mmoja au wawili wanachukua chombo aidha fighter jet au bomber ambazo hazionekani kwenye rada na kwenda kudrop madude then baada ya masa 6 au 10 wamerudi huku uko walipo kwenda wakiacha vilio tu na kazi ya ambulance kwa ajili ya kubeba majeruhi au maiti na fire kwa ajili ya kuzima moto

Pia kwa wenzetu jeshi ndipo vitu bora vinapatikana kuanzia elimu bora na huduma bora za afya kwani viongozi wote wa serikali wakiumwa utaskia wamepelekwa kwenye hospital za kijeshi wanasema kitu chochote bora duniani kinapatikana jeshini kwa wale wanaotaka kuomba kazi moja kwa moja unaweza pita hapa www.maltajobport.com

mwenye swali aulize bt no pm kwani sito jibu msg ya mtu yeyote

kirikou1 kweupee Hary Jay Ndata Prishaz WiseLady Mrike wembeee talentboy Dr.adams faida Daby Tombstone Piledrive Padri Mcharo Shyshii lucley kui tagamwa binti kiziwi dangadunguri Tembo2 lusungo kweupee pius1021 Prof cognition Agogo Jr Chakochangu soul provider Mrike
https://www.google.com/url?sa=t&rct...sg=AFQjCNH9Pvbb83aZc4r_XxpdH36SWqh9aA&cad=rja
 
asan
asante sana mkuu ku tagging, bado nina interest ya Malta. vipi airfare Dar to Malta?
 
Bro, sasa njia za kupata nafasi ya kuvolunteer?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…