Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Mkuu izzo ningeomba ufafanue kuhusu suala la mchakato wa hao vijana wanaokwenda nchi mbalimbali kwaajili ya kutalii na kujifunza tamaduni,
je, kuna website maalumu ya kuwasiliana nao?(hii inaconsist kama watahitaji kuwatumia picha yako na mahali unaishi ili wajiridhishe)
Vilevile umesema kunauwezekano wa kuwaleta hata 30 kwa mwaka, je huwa wanakuja group au jopo la hao vijana wote kwa mkupuo, au kila mtu anasafiri kivyake?( hapa nataka nifahamu wakifika nchi husika kama watakuwa na tabia za kuwasiliana na kutambuana kwa ujumla)
Naomba ufafanue hayo kwanza na kama kuna vitu vya kuongezea basi itakuwa mwake
 
Nitumie fursa hii nyingine ambayo ni adhimu sana kukushukuru mkuu izo namuomba Mungu afungue baraka juu yako kwa upendo wako kwetu Cc ndugu zako
 
Kujibu swali lako kwa ufupi kwani hapa tumekuwa na Mission na Vision Mission ni kwenda kusaidia ndugu zetu Watanganyika kuja kutafuta maisha nje ya JPM empire so starting point ni nchi ya Malta tukaanza na Option number 1 now ni option number 2


Kujibu swali lako kama nilivyosema nimekuwa na ushirikiano na taasisi za vijana katika nchi hzo yani Nonproft org ambazo wao wanafanya kitu kinaitwa culture exchange ambapo wanachukua vijana kwenda sehemu mbalimbali duniani kwenda kujifunza tamaduni na lugha za nchi mbalimbali duniani lakini hawajawai kuja Tanganyika so ninauwezo wa kuongea nao na kuwashawishi juu ya kuleta vijana Tanganyika lakini vigezo ni vile nilivyovitaja

Wanakuja kwa mafungu mafungu kwani wengine wanakwenda nchi nyingine so wanaweza kuja 5 then wakaja tena 6 lakini kwa mwaka wanaweza fika 20-30 huku Tanganyika lazima kuwepo na mtu ambae atawapokea na kuwapeleka kwa hao host kila host mgeni mmoja mmoja sema sasa project hii inachangamoto kama nilivyosema kwenye bandiko hapo juu
 
britanicca huyu jamaa anaogopeka kama ukoma ameliza watu wengi saana hapoa jamii forum kuna uzi alianzisha kwa kusaidia watu kama agent...
hivyo basi kama huyu jamaa mwenye namba +12136666803 anaukaribu na mtu anayeitwa britanicca ambaye ndio mwenye ID hizi tatu anatumia DR RWEYENDERA na Katelelo naona kampani yake si salama ndio maana hata ukiangalia watu wanaofanikiwa niwachache wengi walirudishwa hivyo basi ni kuchagua moja ila huyu agent nina walaakini naye.
 
Tuweke malta kwenye plan aseeh.

Sema nimevutiwa na visa ya uchumba. izzo nafikir anapaswa kunifikiria juu ya hili.

Halafu Adams ngoja kesho nikamwone yule jamaa wa host nione anamwelekeo gani
Mcheki mkuu utanipa mrejesho..
 
Mkuu itabidi nikifika Tanganyika niwasiliane na wewe kuhusu hili la kuwapokea hao vijana
 
Sio kweli mpk ufuate utaratibu wao,na mtu ukipata residence hapa sweden huwezi kutamani kuhamia Denmark maana upatikanaji wa kazi Kati ya Denmark na sweden hapa ni easy mkuu
Mkuu expertise gani wanahitajika sanaaa huko??
 
Hata nilivykua Dubai nilikua najitambulisha kama mkenya, maana kule wakenya wanawafahamu sijui walikua wanawauzia chai/kahawa Dubai miaka hiyo, so at least wanaelewa ila wengi ukiwatajia Tanzania hawaelewi
Umesaliti nchi mkuu
 
Mkuu tunashukuru kwa michango yako aise maana bongo imekua chenga sana aise ngoja nizidi kufuatilia huu uzi kuna maaarifa nayapata kutoka hapa.
 
Mkuu fani gani ya elimu inahitajika sanaaa huko, yaani hata kesho mtu akija anapata kazi
 
Wabongo wa majuu hamna upendo mnajigawa...!,Uongo hauna miguu skendo zina mabawa...!
 
Mkuu umeandika vyema sanaaa, napenda kuuliza mpaka nifike hapo Malta niandae sh ngap.
 
Ndo leo naona jf mtu analilia atongozewe demu daaah! jf raha sana mkuu izzo ukimtongozea na mimi nakudai..πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…