Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Hahaha, nimefurahi khs uyo kinega
 
Hata mm natarajia kwenda kuishi japan. Thou inabidi nioe kule mke wa kijapani. By mwez wa 4 naondoka. Nabeba mikuyati yangu ya kutosha naanza maisha ya kijapani
Hongera sana mkuu, tutakua twakutana angani Inshaallah
 


Mkuu ubarikiwe sana aisee, Tunakuombea Mungu akujalie Afya na Amani

Jana ubalozi wa Italy/Malta mpaka mlinzi ananiuliza unakuja lini kuchukua visa! Nimekukukumbuka mkuu Malter the Best.
Mkuu naomba nikurudishe nyuma kidogo. incase nataka jeshi sweden, 1. je ni kweri ndio tunaowekwa frontline kwenye mission za hatari? 2. usajiri wa kuingia jeshi sweden moja kwa moja pamoja navigezo vyake vipoje 3. value ya mtu mweusi inafanana na ya mswiden. for me napenda jeshi, naomba nisaidie Mkuu, nina fear of unknown.
 
Mkuu hio web ya visa ya Malta ktk Italy embassy nimeingia nimekuta ki italiano kitupu ko sielewi

Embassy of Italy
P.O. Box 2106 - Lugalo Road, 316 - Upangas - Dar es Salaam
Tel. +255 22 2115935/36 - 2123010/11
Commercial Office - Tel / Fax +255 22 2117369
Emergency telephone: +255754 777 701 (emergency calls and after hours)
hours: Monday to Friday: from 08.00 to 15.10 - Wednesday: 08:00 to 16:10
certified Mail:
amb.daressalaam@cert.esteri.it
amb.daressalaam.cons@cert.esteri.it
amb.daressalaam. pass@cert.esteri.it

Ambassador
Roberto Mengoni
Email: segr.dar@esteri.it
Int. 102

chief hii ni full package ya contact zao, in case umekwama kwa website just call them on Hot line. likini mimi iko poa na nipo naifanyia kazi muda huu.
 
Safi sana mkuu, vipi ume apply visa ya aina gani kwenda malta? Umeshapigiwa simu kuwa umefanikiwa?
 
Asante kwa update mkuu Izzo,
Mungu akubariki zaidi na zaidi
 
Safi sana mkuu, vipi ume apply visa ya aina gani kwenda malta? Umeshapigiwa simu kuwa umefanikiwa?

Chief nipo initial stage sana, so nasoma masharti kwa kina, then nitakapokwama niwapigie ubalozi wanipatie ufafanuzi. mkuu by kesho ntakua vizuri mkuu.
 
Chief nipo initial stage sana, so nasoma masharti kwa kina, then nitakapokwama niwapigie ubalozi wanipatie ufafanuzi. mkuu by kesho ntakua vizuri mkuu.
Okay nilifikiri umeshafanya application.
 
Kwani maua nje yanauzwaje? Mi nnavyofaham kuna jamaa mmoja alikuwa anayakata vijiti kama vya inchi nne hivi then anavipack kulingana na aina tofauti tofaut ya maua,
Fursa hii mkuu ndio na mm nauliza mwenye kuielewa uzuri na ambaye alisha wahi kuifanya basi tuone jinsi gani twaweza fanya kwa pamoja na kama soko pia lipo basi hii fursa nzuri kwa kweli...
 
TANGAZO KWA UMMA

Ijumaa, 10 Machi 2017 13:23
TANGAZO KWA UMMA


NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SAYANSI NA HISABATI WALIOHITIMU MWAKA 2014/2015 KURUDI NYUMA.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia wahitimu wote wa Stashahada na Shahada ya Ualimu katika masomo ya Sayansi na Hisabati wa mwaka 2014/ 15 na miaka ya nyuma, kuwa bado kuna nafasi za ajira, hivyo, wenye sifa watume maombi yao.

Wahitimu walioomba wakati Wizara ilipotangaza nafasi za ajira mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 wasiombe tena kwa kuwa mchakato wa ajira kwa wale wenye sifa unaendelea. Wahitimu walioajiriwa Serikalini wasiombe.

Nyaraka zinazotakiwa kuwasilishwa ni hizi zifuatazo:-

  • Elimu ya sekondari (Kidato cha Nne na Sita);
  • Taaluma ya Ualimu (Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu -PGDE);
  • ‘Academic Trascript’ ya Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu-PGDE);
  • Cheti cha Kuzaliwa;
  • Wasifu (CV) unaoonesha majina matatu. Mwombaji ambaye vyeti vyake vya Elimu na Taaluma havina jina la tatu, akamilishe taratibu za kisheria za kuongeza jina la tatu na kuwasilisha kiapo stahiki pamoja na maombi yake.
UTARATIBU WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-

  1. Mwombaji anatakiwa ‘ku-scan’ vyeti/nyaraka halisi – (Kidato cha 4, 6, Stashahada, Stashahada ya Uzamili na Shahada) na siyo kivuli (photocopy) na kuhifadhi katika ‘File’ moja la ‘pdf’. File lipewe majina matatu ya mwombaji kuanzia la kwanza, kati na la mwisho ndipo litumwe.
  2. Mwombaji atumie anuani ya barua pepe yake mwenyewe na siyo ya mtu mwingine kutuma nyaraka zake.
TANBIHI:

  1. Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 30 Machi, 2017.
  2. Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji zitumwe mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu.
  3. Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika ajira.
  4. Wahitimu ambao waliomba awali mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 na nyaraka zao ziliwasilishwa kikamilifu na kupokelewa, majina yao yamewekwa kwenye tovuti ya Wizara www.moe.go.tz. Hao wasiwasilishe nyaraka hizo tena.
  5. Tangazo hili haliwahusu wahitimu waliofaulu mtihani mwaka wa masomo 2015/16 baada ya kurudia masomo waliyoshindwa mwaka 2014/15.
  6. Nyaraka zote ziwasilishwe kwa barua pepe ifuatayo: apa@moe.go.tz
IMETOLEWA NA

Tarish M.K.
KATIBU MKUU
10/03/2017
 
Website gani?
wengine nawapata Instagram ila huyu anaenikubari zaidi nmekutana nae facebook tu na tulianza kama friends end of the day tukawa couples tangu mwaka jana mapaka sasa ila wa Tennessee Nina miaka nae minne na nmekula pesa sana vidollar mia mia kawaida sana kunitumia
 
Hahaha... kwanini usiwe na vision nao ndefu mkuu kuliko kuendelea kula kula vipesa vya uji. Jichange uwapange ukapate residential permission.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…