Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Britanica alikutenda nini? Mimi sihitaji pesa yoyote nakupa ramani tu...

Kuhusu cheti cha kuzaliwa cha mzazi kisikutishe... Pale uhamiaji hutoa hati za kiapo cha baba au mama, ukienda kuna wanasheria wanakusainia kwa elfu 10 tu ambapo utapatiwa affidavit then utaambatanisha. (muhimu uwe na taarifa kamili za baba au mama)
Huyo britanicca.ni kirusi.
 
hii ni shule mkuu, big up.
Dada unajua ktk East Africa au Africa nzima Watanganyika ndio wamekuwa watu waoga sana kutoka nje na hii wamezeshwa toka enzi ya J.K Nyerere yani wameaminishwa Tanzania na mikoa yake ndio sehemu pekee kuishi na kutafutia maisha ndio maana mpaka leo ukiomba passport lazima huwe na sababu dah hv ni kweli passport ndio kitambulisho cha kimataifa kinachomtambulisha mtu lakini kwenu kukipata mpaka eti ueleze sababu kwa nini unakitaka


Then kila ukimuuliza mtanganyika atakwambia anataka kwenda nchi ambayo kila siku anaisikia na kuiona kwenye BBC,CNN wakati kufika huko ni lazima uwe na vigezo na nchi hzo siku hz wanafunga mipaka kwa wahamiaji leo sijui kujilipua hakuna nafasi tena ukikamatwa tu ni safari hapo hapo ulipo sasa kama utaweza ukiona gari la LAPD au NYPD au POLICE ukajificha kwa miaka yote sawa lakini siku wakikukamata tu unarudi home kwenu bila hata kubeba sindano uje nayo home kuwaonyesha
 
Utaratibu tuliuharibu wenyewe...miaka ya 2000 passport haikuwa kazi ngumu kuipata...now imekuwa ngumu sababu ya wahindi..wasomali na watu wengine ambao sio watanzania kwa faida ambazo Tanzanian passport holder tunaingia entry..wakawa wanapewa passport zetu kama NJUGU...now ni SAWA TU kuwepo na udhibiti wa passport..ni vyema passport kuwe na udhibiti...MGUMU
Tunaumia sisi.tunaotaka kutoka kutafuta kakaa.
 
Izzo tupe mchakato wa kupata kazi za kujitolea,hata mashambani...watu tuelekee huko mana Tanzania tunapoteza Muda,kila unachopata serikali inachukua
Mkuu nimecheka sana hapo uliposema kila unachopata serikali inachukua [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndugu wana JF
Kwa muda mrefu kumekuwa na masuala mbalimbali yahusuyo kujilipua (kwenda nje ya nchi) ambayo watu wanauliza mmoja mmoja kwa lemgo la kutaka msaada na ushauri namna ya kufika na jinsi ya kuanza maisha huko nje.

Kutokana na kutoa msaada kwa wengi (binafsi) kwa kutumia njia binafsi nimeona nifungue uzi huu ili kuweka mambo yote wazi kwa kadiri itakavyowezekana na kualika wengine pia waweze kutoka maoni yao.

Ndugu zangu nchi yetu ya Tanzania ki uwezo bado ni changa, fursa za kutoka ni chache na hata changamoto ni nyingi. Huko kwa wenzetu fursa ni nyingi ndio maana imekuwa chanzo cha kuvuta wahamiaji wengi sana toka mataifa masikini.

Nchi masikini wenzetu huko mbele raia wao wamejaa haswa kutokana na moyo wa kusaidiana na kuvutana.

Nimeamua nilete hoja hii kama ambavyo wenzetu hufanya huko Nairaland ya Nigeria ili kila mtu mwenye ujuzi au ufahamu juu ya namna ya kutoka (kujilipua) atoe msaada kwa wengine kwenda huko... si lazima wewe binafsi usaidie mtu binafsi NO, hata mbinu tu za jinsi ya kufika huko.

Kabla sijaingia kwenye kiini cha mada naomba nitoe faida na changamoto za kujilipua.

FAIDA
1. Fursa nzuri za kiuchumi na kujiinua hasa ukiwa na malengo.. Wakuu binafsi nimeishi Marekani kwa miaka nane. moja ya faida nilizopata huko ni kujiinua kiuchumi.... binafsi wakati naenda kusoma huko nilijiwekea malengo ya kujenga ghorofa nyumbani, kufungua mashine za kusaga na kukoboa nafaka pamoja na kumiliki fuso za mizigo...

kipato cha mfanyakazi wa kule ni kikubwa mno kushinda hata cha baadhi ya maboss wetu hapa... hivyo nilijitahidi nilipokuwa kule malengo yangu yaimie... ni kweli baada ya muda huo nilifanikiwa kutimiza yote.

2. Huduma nzuri za afya, Elimu, Sheria, miundombinu.

CHANGAMOTO
1. changamoto kubwa kwa kuwa kule ni upweke (ku feel home mara kwa mara japo wakati mwingine ukizoea hutoweka)

2. Xenophobia hii ni kwa baadhi ya nchi tu sio zote.

USHAURI WA WAPI UENDE NA NAMNA GANI UENDE
Kwa wale wahitaji wa masuala ya maisha kujijenga na kuchuma nashauri nchi hizi, USA, UK, NORDIC COUNTRIES, NA WESTERN EUROPE COUNTRIES. kwa Afrika nashauri SA.

Jinsi gani utaenda namna ni nyingi.... naorodhesha baadhi hapo chini...
1. kwenda kimasomo ambapo unaweza tafuta sponsors then ukapata scolarship itayokuwezesha kupata visa na kujilipua huko baada ya masomo...

2. Kutafuta mwenzi wa nje ambaye atakualika huko kisha mtaoana na kukuwezesha kupata resident permit na baadae uraia.

3. Kuhamisha mataji na biashara njia hii unakubaliwa popote alimradi uwe na biashara halali,

4. kwenda kwa shughuli za utamaduni

Wenzetu wakenya na wanigeria wameunda mfumo wa kualikana wao kwa wao, kwamba mtu anakutumia barua ya mwaliko, then unakwenda ukifika huko anakutafutia mtu mnaoana kisheria tu ili upate karatasi kisha kila mtu anasika hamsini zake....

Wapendwa mambo ni mengi siwezi andika yote ndio maana nimeanziasha uzi huu tutaendelea kujuzana kwa kairi michango ya watu itakavyokuwa na maswali yatayojitokeza.

Nawakaribisha wafuatao: BAK kui Isanga family Sky Eclat


Matola MziziMkavu Copenhagen DN Ng'wamapalala Pascal Mayalla Nyani Ngabu rev kishoka Bavaria FaizaFoxy farkhina MfalmewaKiha mwandende Slim5

Na wote wenye maujuazi au mauzoefu ya huko mbele... karibuni tusaidiane tujenge taifa letu... Tuwasaidie vijana wakasake fursa.
Mkuu tafadhali niPM mkuu umeniguza kwene malengo yango nadhani utanisaidia sana Mkuu japo Majina uloyataja ni Magumu kama NG'WANAPAGI, NG"WAMAPALALA Majina ya home kabisa iyo ila Magumu sana Mkuu...
 
Kuna baharia mmoja miaka ya 2000 alikuwa anaitwa msakanyoka
Alichukua hela yetu ya ada kwa minajili anaenda kututengenezea passport
Kumbe feki

Aha ah kweli safari kafiri
Never forget unaona kabisa rafiki yako tena mko safari moja, maskani yenu moja

Wanamchomoa pasport Inapigwa x Unarudi ulikotoka hapo ni ranokwabane
 
Mkuu ninakumbuka wa-Somali walikua wanaingia passport wanaflash kwenye choo cha ndege wakifika Heathrow, baada ya hapo wakifika kwenye immigration desk wanajilipua hawana passport. Mashirika ya ndege nayo yalianza kuriport vyoo kuziba. It was a big scandal na zote zinakutwa ni passport za Tanzania.
Hiyo sasa wamedhibiti kwa kiasi kikubwa sana ndy maana wanatumia njia ya MAJINI. now kila shirika LA ndege wana AIRLINE SECURITY.. kuna jamaa lazima ukutane nae kwnza akuhoji.. Akaguwe passport na viza na hata mualiko wako.ndy URUHUSIWE KWENDA KWENYE boarding PASS DESK. .nakumbuka nilipotoka AFRICA hapo VIA Nairobi. Jamaa wa Emirates airline security alinisumbuwa sana...ila nilifanikiwa kuruka. Ila kuna msomali mmoja with Kenyan passport holder walimzuia kuruka. Rout yangu ilikuwa NAIROBI..DUBAI...ROME....yule msomali ni NAIROBI.. DUBAI..TURKY..na alikuwa hana viza ya Turkey.. Wao wanaingia ENTRY PALE ...tulimwacha pale ..hawakumruhusu KURUKA. Msomali akifika TURKEY tu ndy safari ya SHENGENA countries zinaanza..hapo..na jamaa wanajuwa hivyo.
 
Mkuu hivi Ukipata Rafiki wa Denmark sio wabaguzi kusema anaweza aka kuharika then akaanza kukunyanyasa?????
Mkuuu ndugu yangu ukiwa mtu mweusi neno ubaguzi au kubaguliwa kuchulia ni kama sehemu yako tu trust me hakuna sehemu duniani ambayo mtu mweusi yuko safe dhidi ya ubaguzi zaid ya Africa japo napo si 100% kwani wapo wanabaguliwa hata ndani ya Africa mfano wahindi , wachina na makaburu SA so ilo lisikupe tabu

Nchi nying za Ulaya wabaguzi sana sana ni wazee na watoto wadogo na mara nying ni wale wanaokaa mashambani lakini mijini ubaguzi umepungua kwa kiasi kikubwa sana
 
Mkuuu ndugu yangu ukiwa mtu mweusi neno ubaguzi au kubaguliwa kuchulia ni kama sehemu yako tu trust me hakuna sehemu duniani ambayo mtu mweusi yuko safe dhidi ya ubaguzi zaid ya Africa japo napo si 100% kwani wapo wanabaguliwa hata ndani ya Africa mfano wahindi , wachina na makaburu SA so ilo lisikupe tatu

Nchi nying za Ulaya wabaguzi sana sana ni wazee na watoto wadogo na mara nying ni wale wanaokaa mashambani lakini mijini ubaguzi umepungua kwa kiasi kikubwa sana
Huo ubaguzi ndiyo unakufanya uwe na malengo, cha kwanza ni sala, sali sana Mungu akusaidie, pili pata elimu yao maana huwezi kuondoka na gunia la pesa na tatu kumbuka kuboresha hali yako ya nyumbani hata ukirudi uwe na pa kuanzia.
 
Back
Top Bottom