Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Mkuu hujanipata vizuri, yaani hii form najaza ndo ya kuomba hiyo visa pamoja na residence permit...
Mkuu hapo ni vizuri uangalie mifano ya kujaza hizo forms au waulize ubalozi husika kuhusu hicho kipengele.
Samahani mkuu
 
Kama kuna mtu ana uzoefu na USA,kuna ndugu yangu anataka kwenda kusoma degree ya kwanza je course ipi inalipa kwa USA,ingawa yeye alitaka kusoma Marketing,
 
Jamani kuna mtu yeyote anayejua taratibu za kupata short term training canada au japan na kukubalika kupata resident permit
 
Jamani kuna mtu yeyote anayejua taratibu za kupata short term training canada au japan na kukubalika kupata resident permit
Kanada ni rahisi kupata PR kama umesoma huko. Lazima uwe na Bachelor's ili uombe PR viza.

Japan, scholarship binafsi zinaanzia doctorate level isipokuwa maofisa wa serikali.

Short term training in which field? Be specific, please. Your major? Work experience?

Toa info zaidi ili ueleweke.
 
Mkuu, mwaka huu nimeomba scholarship kwenda kusoma Australia, China na UK
Niombeeni nifanikiwe ,nijilipue huko, nafanya kaxi ila haina maslahi na wategemezi lukuki, bora nitokomee huko kwanza

Wewe na mimi hatupishani. Kadegree kangu kamoja tu wategemezi kibao siishi kwa raha mjini kila saa simu za kuombwa hela tu. Nimeomba scholarship Norway China na Sweden. Zikigoma naenda kujisomesha. Mwaka jana nilipata chuo ila nikawa nategemea mpaka scholarship....sasa mwaka huu nikikosa scholarship naenda kujisomesha mwenyewe nauza ki mark x changu kisha naunganisha na mpunga mwingine huyoooo China kujisomesha nikifika huko mambo itajipa tu. Kuna jamaa yangu kaenda mwaka juzi kwa kujisimesha kajilipia ada semester ya kwanza tu ya pili akapata scholarship na sasa muda ambao hayupo darasani anafundisha vitoto vya kichinia Kiingereza anapiga mpunga wake safi wa kama mabank teller watanne kwa hapa Dar. Kaka tuondoke tupotee kama miaka mitano hivi kisha ndo turudi maana ndugu wa hapa bongo hatutaendelea
 
Mimi nataka kwenda Denmark. Naomba jinsi ya kuingia na fursa zilizopo huko zisizohitaji elimu.yaani nguvu kazi.

Nimekaa Denmark kama taxi driver miaka minne. Kule ukipata chance ya kwenda we nenda kafanye kazi za kufunga mabox au kusafisha kiwanda kimoja cha nguo kipo Hedeslev unapiga laki tatu kwa siku japo kodi ya nchi ile ni kubwa 47% lakini bado unabaki kama na kilo mbili hivi. Ila uwe sio mzembe mzembe wale wanapiga kazi fasta fasta na unakuwa monitored na mashine. Ukiwashiwa red tu kesho hawakupi kazi na pia uwe on time. Sasa jiulize kwa mwezi ukipiga si una m zako zaidi ya 20? Halafu baada ha muda unafunga ndoa na mwanamke yeyote kisha maisha bwerere....asikudanganye mtu watu weusi mademu wa kizungu wanatupenda sema hawatakagi kusema tu in public na wengi ni ndoto yao one day to bed with an African man....ndio maana kaka zao na baba zak wanatuchukia ila ukweli ndio huo black is beautiful.

Jinsi kuingia---tafuta rafiki yeyote aliyoko huko (ila awe wa kiume---akiwa wa kike hupati visa pale Norwegian embassy watakuzingua tena kama ukikuta siku hiyo anayekuinterview ni yule chalii mswahili utachukia ubalozi huo, bora yule bibi aliyeolewa na mswahili mwenzetu miaka kibao iliyopita)
Huyo rafiki hata kwa fb unaweza ukampata tu angalia tu fb watu wa Denmark has wenye last name zinaishia "SEN" kisha jifanya urafiki hata umkaribishe bongo then mnakuwa marafiki anakualika huko kwao. ONYO usianze na shobo kuwatafuta hao marafiki----wazungu hawapendi shobo kabla hamjazoeana wanataka distance kidogo-----so act sitaki nataka na usisifie sana nchi yao sifia sana bongo na usionekane unataka saaaaana kwenda kwao.
 
Wewe na mimi hatupishani. Kadegree kangu kamoja tu wategemezi kibao siishi kwa raha mjini kila saa simu za kuombwa hela tu. Nimeomba scholarship Norway China na Sweden. Zikigoma naenda kujisomesha. Mwaka jana nilipata chuo ila nikawa nategemea mpaka scholarship....sasa mwaka huu nikikosa scholarship naenda kujisomesha mwenyewe nauza ki mark x changu kisha naunganisha na mpunga mwingine huyoooo China kujisomesha nikifika huko mambo itajipa tu. Kuna jamaa yangu kaenda mwaka juzi kwa kujisimesha kajilipia ada semester ya kwanza tu ya pili akapata scholarship na sasa muda ambao hayupo darasani anafundisha vitoto vya kichinia Kiingereza anapiga mpunga wake safi wa kama mabank teller watanne kwa hapa Dar. Kaka tuondoke tupotee kama miaka mitano hivi kisha ndo turudi maana ndugu wa hapa bongo hatutaendelea
Yaaani unavyoongea utadhani unaona harakati zangu, inafika sehemu unakomaa sura kwa kuwaza.
hebu mkuu weka sawa hiyo ya China au Japan ada zao shilling ngapi za kibongo ili tuanze kukomaa kuzitafuta.
 
Mwenye uelewa hizi visa za ubaharia tuambizane humu naona wengi ni za kusoma.

hizi visa unaweza kuipata kama unasema meli yako iko Usa kumbe ni tofauti, wazanzibar wengi wameondoka kwa mchongo huu.
 
Asante sana mkuu tokyo mimi ni graduate wa education in science na napenda kuishi canada nimejaribu kuomba vyuo lakini gharama naona ni kubwa sana na scholsrship siqualify kwa sababu GPA yangu ni 3.4 lower second hivyo nimeoba option ni kupata training fupi hasa ya vocational jobs ambayo itaniwezesha kupata kazi canada au jyhapan au scandnavian countries ili nikisettle nisome medicine au nursing au lab science nikiwa nimepata uraia au permanent residence please naomba yeyote mwenye information anisaidie
 
Mkuu, kubadilisha major sio rahisi kwa njia yako. Kwanza itabidi uanze upya na itakugharimu pesa nyingi hata kama utakuwa raia wao.

Kama huna uwezo wa kulipa fee, nakushauri uombe kusoma Ujerumani au Norway. Huko chuo ni bure kwa wageni, unalipa malezi tu na GPA yako inakuruhusu.

Sifahamu njia nyingine ya kukusaidia.
 
Mkuu Malinyi,

Hiki ni moja ya chuo bora huko Berlin, Ujerumani. Fee yao ni Euro 120 hivi lakini pia kuna utaratibu wa kuweka fedha katika ubalozi wa Ujerumani kama Euro 7000.

Angalia tovuti ya chuo. Kinaitwa Technical University of Munich.

Application and Acceptance - TUM

Fahamu kuwa utahitaji kuonyesha na kufungua a/c ya Euro 7000 ubalozi wa Ujerumani, Tanzania. Hii ni gharama ya maisha kwa mwaka Ujerumani.
 
Ninashukuru sana kwa uzi huu, nimeona wengi hawana uchoyo na suala hili. Ni dhahiri kuwa watazania wengi tumekosa fulsa mbalix2 kwa kutozijua zilipo, na wanaozijua hawazitoa bayana. Shukran kwa waelekezaji, ombi langu, wengi tunataka kusoma nje ya tz yetu, lakini uchumi unadumaza sana ndoto hizi na nimehangaika sana na scholarship ya masters ya elimu, au inayoendana hii lakini lakini sjaona mwanga bado, ndgu zangu walio nje tusaidie hata kwa ushauri wa kina. Mungu awabariki walioleta uzi na wachangiaji wote.
 
Mkuu mm sijibu PM kama nilivyosema toka mwanzo kuhusu Chuo
Ni Chuo kizuri lakini si best hiki unasoma free lakini ukitaka cheti baada ya kumaliza courses inakutaka utumie hela kwa ajili ya shipping ya cheti lakini cheti chake si cha thamani sana Kwani kila kitu unafanya ww so uwezekano wa kucheat ni mkubwa sana kwani baada ya course unatakiwa kufanya mtihani na unatakiwa u score 70% out of 100 % lakini bado nabaki pale pale uwezekano wa kucheat ni mkubwa sana
kwani bado mitihani inakuwa pale pale yani unaifanyia kwenye computer then kama utashindwa kuscore 70% unaweza kurudia tena kufanya tena mtihani tena ambao unakuwa the same so credibility ni ndogo sana

Chuo ninachozungumzia mm ni kama hvyo hyo na mtihani ni kama hvyo hvyo lakini mtihani wa mwisho unakwenda kufanyia ubalozini au kwenye centre watakayokuchagulia wao so uwezekano wa kucheat unakuwa hakuna chuo hiko unalipia lakini kuna technique ya kusoma bure 100% free
Salam Kaka Izzo. Naomba kukukumbusha kuhusu vile vyuo vya kusoma usalama wa afya kazini OSH. Pia kuhusu jambo nilikujulisha awali.
 
Yaaani unavyoongea utadhani unaona harakati zangu, inafika sehemu unakomaa sura kwa kuwaza.
hebu mkuu weka sawa hiyo ya China au Japan ada zao shilling ngapi za kibongo ili tuanze kukomaa kuzitafuta.
Yaani nimependa ushauri wako shukurani mkuu ; lakini pia naomba nikuhulize kuhusu na upande wa Wakina dada kazi huko siko vp kama unafahamu
 
nimependa huu mjadala kiukweli naamini mdogo mdogo tutabadilisha hiii mitazamo tunayosakamwa nayo ya kutopendana na kuonyeshana channel barikiweni sana wenye positive vibes
 
Back
Top Bottom