Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bila Lowasa upinzani ungepata wabunge zaidi na heshima yao ingebaki palepale, sasa hivi unashangilia wabunge ambao wote walikuja kuunga mkono juhudi
Ungewapata wapi ambao wasingeunga mkono juhudi? Je, akina Halima Mdee, Ester Bulaya, Yule mBabati anaeingizia watu chupa kwenye makalioni, Waiara, Silinde na wengine waliounga juhudi, hawakupo Chadema kabla ya ujio wa Lowassa?
 

1. "Jasiri" ni neno la kiswahili lililo na maana moja tu ambayo hata mtoto mdogo ambaye hajaanza shule anaijua.

2. Ila nifanye je kama nimeulizwa swali hata kama la kitoto?

3. Ninakuwekea hapa "post yangu #6" ipo kwenye uzi huu kukuonyesha kuwa jasiri ni yupi, kuwa si mara ya kwanza kulitumia hata kwenye uzi huu huu, kukuonyesha hakuna kipya:



4. Bado maana yake kamili imeelezwa kwenye uzi huu niliokupa:

Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

5. Hapo #4, ninakuwekea hapa utangulizi wa uzi huo kujiridhisha uliuona:



6. Kwamba pamoja na post yangu #6 (kwenye uzi huu), pia hapo: #5 na hivyo #4 yote, bado hukuweza kujua ni ujasiri upi naoungelea?

7. Unayasoma wapi "mabunduki au fujo" unazoongelea wewe?

8. Hapo #7, nimekuwa nikikukumbusha mara zote kutonihusisha na lolote lisilotokea kwangu.

9. Linihusu nini vipi nilisiloliandika mimi?

10. Niko wazi kujadili hoja kwa hoja lakini si kujadili misamiati ya kiswahili au kuwekeana maneno mdomoni.
 
Marekebisho kidogo, hawakumpokea Lowassa na kumpa uenyekiti, bali walimpa nafasi ya kugombea urais. Jambo lile halikuwa sahihi. Hilo la kwamba ccm walimkata wakijua ataenda cdm na kupokelewa Sina hakika nalo, ila nijuavyo ni kuwa Lowassa hakupewa nafasi bure bila kutoa hela.
 

1. Kwamba uniongoze wewe kusoma ninapo kushutumu wewe kuedit kihuni?

2. Umeongezea aya nzima kihuni baada ya kuwa nimekujibu hoja zako zote na hilo kwako ni sawa?

3. Tafadhali tambua silichukulii suala hili la ku edit kinyemela yaliyopita (kwenye mambo nyeti) kuwa ni dogo au la kupuuza:

Namkubali sana Wakili msomi Mwabukusi lakini...

4. Kwenye post hiyo hapo #3 niliwahi kugundua "malicit isiyokubalika JF kuhusiana na hii ya ku edit kinyemela vilivyopita: "Kwamba 'malice' hiyo ilikuwa ya kufanana na hii iliyo mhusu huyo Huihui2 , kama ilivyo hapo ambayo ni vyema mkurugenzi Maxence Melo na hata Moderator wakafahamu. kuwa kuna mambo muhimu ya kujitathmini "seriously" wao kama "provider."

5. Hapo #4 niliamini bila shaka bwana Mshana Jr aliweza kunisoma vyema: "Kwamba tunaandika kwa umakini, weledi na nia njema ambapo privacy, anonymity na integrity yetu katika kila hali haviwezi kupuuzwa." Si tu, huwa tunarejea kuandika tulivyoandika "integrity" ya tulivyoandika juzi, jana, asubuhi, au mwaka jana nk. Yaani kuona kama vingalipo kama tulivyoviacha? Kwamba hakuna maruhani au mkono wa mtu siyo?

6 Hapo #3, #4 na #5 ninao ushahidi wa baadhi ya post zangu za siku nyingi nyuma kupotea. Yaani kufutwa na hivyo kuweza (hata) kubadilishwa pasipokuwa na uhalali wowote na nisiowajua.

7. Ninaiweka hapa sehemu ya kughafikishwa huko kutokea #3:


"Unapaona hapo kwenye maujanja ya kufuta kinyemela posts za nyuma za watu?" Yalinikuta kwenye uzi huo pia.

8. Siasa uchwara za humu JF ninazijua na si nia yàngu kupotezeana muda na yeyote au kupakana matope kihuni.

9. Si kila mtu anavinjari huku akiwa na nia ovu yaani "ulterior motives."

10. Ama kwa hakika nimefadhaika.
 
Ila wewe dah unanifanya nicheke sana...

Sijui kwanini unasema nimeongeza aya nzima kihuni, huo uhuni unatoka wapi jamaa kama aya niliyoongeza haifanani na ile ya awali?

Kwani nabanwa na sheria gani hapa JF kuongeza aya moja baada ya ku type aya nyingine? hebu nipe hiyo sheria kama ipo.

Sijaona sababu yoyote kwako kuwataja wengine kwenye jambo linalonihusu mimi, mimi nimefanya kile nilichofanya bila kuvunja sheria yoyote ya JF, mawazo yako tu ndio yanakufanya uwe mkali kwa jambo dogo.

Unatakiwa kujibu aya zote kama nilivyoandika, bila kujali kama aya moja ilitangulia nyingine ikafuata, kuzunguka hapo kwangu ni dalili ya mtu aliyezidiwa hoja, sasa anatafuta mlango wa kutokea, nothing else.

Wacha ujanja janja wako!. Huo ugunduzi wako mimi sihusiki chochote, usilazimishe kuingia kwenye kichwa changu ujione unajua nia yangu, hiyo ni ramli tu kwangu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 

1. Kule nimekupa mfano ambapo maandiko yangu ya nyuma, yamefutwa na wasiojulikana kinyemela.

"Kwamba kumbe mtu anaweza kuedit posts zangu za juzi kuwa zisomeke Leo kama atakavyo."

2. Moja kwa moja hilo si halali, ni wazi kuwa ni uhuni kuhalalisha malengo fulani maovu.

3. La kwako si tofauti sana na hayo hapo juu.

4. Hapo #3, kwamba tumejibizana tukatoka kwenye post au mada husika; ninakuja kujua vipi ulikwenda kinyemela (wiki baadaye) kuongeza au kuondoa aya zingine kukufaa wewe utakavyo?

5. Ni wazi huku kubadili kunakofanywa kinyemela, hakuhitaji majibu ila ni uhuni ule ule kufanikisha nia fulani ovu.

6. Kwamba ucheke? Labda kama ni kujichekesha.

7. Majina niliyoyaweka pale sikuyaweka kwa ajali. JF inaweza kiboreshwa zaidi kuondoa uhuni huu.

8. Kumbuka DM baada ya dakika kama 5 hata huwezi ku edit tena message yako.

9. Hapo #8, twitter haina option ya ku edit kilichotumwa.

10. Kujadiliana kwa uwazi kiugwana ni sawa, ila si vinginevyo.
 
Ok sawa umesikika Mwaka huu Mbowe anaachia uwenyekiti, natamani kuona unagombea nafasi hiyo muda huo ukiwadia. Hawezi kujiuzulu bali ataondoka kwa kuamua kutokugombea au agombee na asichaguliwe kwenye nafasi hiyo.
 
Mimi siyo mwananchama kuliko mwingine, kama wewe ni mwanachama kweli iwe ccm au chadema. mwenyekiti hana sababu ya kujiuzulu, anaweza asigombee muda wake ukiisha, au afariki na nafasi iwe wazi.

Subiri muda huo hauko mbali, nafasi zote zitatangazwa na ugombee nafasi uipendayo hasa huo uwenyekiti. Nitafurahi ukishinda kwa sababu nitataka kuona mawazo yako yanakipeleka chama huko mbele unakotaka.
Mimi siwezi kumchoka mtu kwasababu kakalia kiti muda mrefu, nitamchoka kama hatekelezi majukumu ya nafasi yake.

Propaganda ni sehemu ya siasa, lakini nimeoina CCM wengi ndio wakimtaka Mbowe ajiuzuru kuliko CHADEMA, hadi nashindwa kuelewa kulikoni? Nilivyoona bandiko lako nikajua ni wale wale ccm, lakini unakataa wewe sio wao, nami nakubali. Na kwa muktadha huo nakuombea afya njema muda ukifika ugombee nafasi uipendayo, lakini siyo kutaka ajiuzuru, sioni sababu ya yeye kufanya hivyo, alichaguliwa na anatekeleza majukumu yake, kwanini ajiuzuru hasa ajiuzuru?

Kama ni mawazo mapya unaweza kuyawasilisha chamani kwa utaratibu, au ugombee uje nayo.

Mimi namtetea Mbowe kwa sababu tu ya wingi wa lawama ninazoziona hazina maana yoyote, huyu mtu alichaguliwa kwenye nafasi hiyo, kwa mujibu wa katiba yao, muda wake haujaisha, na hajavunja katiba kwa matendo na anafanya kazi yake.

Wewe huoni hayo unataka ajiuzuru, kwanini usifuate utaratibu mliojiwekea, usisubiri muda unadi sera uchaguliwe?
 
Unaandika vibaya mpaka nahisi kutapika
 

Mmiliki wa shamba (cdm) lake ajiuzulu kumiliki. Sijawahi kupata kusikia. Labda afanye kuliuza.
 
Kwa kadiri ninavyo ona mimi mchoma mkaa wa mkata:
Lengo kuu la Maldive's queen ilikuwa kuua uwezekano wa muungano kati ya timu reform na timu ya mwamba ulioanguka dhidi ya the great wanamtandao. Hivyo, ukabuniwa mkakati wa kutengeneza mazingira yatakayofanya uwepo mvutano na chuki kubwa kati ya timu ya Wanamageuzi na wafuasi wa mwamba ulioanguka.

Timu reform ikaingia kwenye mtego pengine bila kujua na wakatumika kama wakala wa kumdhoofisha adui wa Adui yao Mkuu, a big mistake kwenye game.

Mkakati uliotumika baada ya Machi 17 ni kutumia utaratibu wa kumpepea na kumchelewesha mpinzani kwa kujenga matumaini ya uongo kwa mpinzani wako, kumfanya mpinzani akusifu kwa matarajio yasiyokuwepo, kumpa short and personal benefit mtu huru, kumchagulia adui mpya mpinzani wako, na hatimaye kufichua udhaifu huo wa mpinzani wako kwa umma ili kumfanya aonekane ana fikra fupi na asiyeaminika.

Baada ya mpambano mkali wa madaraka kati ya Malkia wa Maldive na wanamtandao, na baada ya kubainika kuwa Team the Fallen Rock ina nguvu zaidi ya Wanamtandao, kulifanyika mapinduzi baridi ambapo wanamtandao walipigwa chini. hatimaye The Maldive's Queen akaamua kuungana na Team grey hair pamoja na Team mwamba.

Hivyo, kinachoonekana sasa ni matokeo ya mchezo. Kimsingi, Team Mageuzi ilifanya kosa kubwa la kimkakati kwa kukumbatia maumivu ya siku za nyuma bila kuona fursa waliyoipata kutokana na machungu husika. Kanuni kuu ya mchezo sio kuangalia machungu ya zamani bali fursa inayoletwa na machungu hayo. Mifano: Mandela Vs. Frederik W. de Klerk; Odinga +Rutho vs Kibaki, kisha Kinyatta+Rutho vs Odinga, kisha Kinyatta+Odinga vs Rutho. Ruto alikuwa ni asset ambayo wenzake walikuwa waki Utilize kufika kileleni, na siku alipojitambua kuwa yeye ni asset akajikusanya na kufika kileleni mwenyewe.

Hata hivyo, bado kuna fursa ya Timu mageuzi, lakini wanapaswa kutoa sadaka kubwa ya kisiasa. Waondoe mapenzi ya watu binafsi na waweke maslahi ya kudumu mbele (Prof Mwesiga Baregu angekuwepo angewaleza vema kuhusu hili kimkakati). Pia wakubali kumpa kijana wao wa kipekee na mwana kindakindaki wao aipeleke Timu kwenye mtanange. Wajikite katika kunyakua kila fursa zilizo mbele yao ili kupata matokeo chanya. wamemlea vema kijana lakini wanaogopa kumpa fursa ya kuwavusha kutokana na kile kinachodhaniwa kuwa maslahi binafsi na kikabila.

mtazamo wa mchoma mkaa wa Mkata ambaye anakubali kupingwa na kukosolewa.
 
Nakubaliana nawe kuwa Matukio yana nafasi katika kuingia madarakani, lakini ni mchezo hatari sana kwa ustawi na sustainability ya chama na sera zake. assume Jamaa angeshinda, nini unafikili kingetokea? Jamaa alijipanga kukiteka chama na kubadili sera ya chama jambo ambalo lingekuwa disappointment kubwa kwa umma na wanachama. Kumbuka, Ma-mvi alikuwa ni Taasisi yenye malengo na falsafa yake na ambayo mwenyekiti wake hakuwa Ma-mvi. Mbaya zaidi falsafa ya timu Ma-Mvi ilikuwa inapingana sana na matarajio ya chama.
 
Bila Lowasa upinzani ungepata wabunge zaidi na heshima yao ingebaki palepale, sasa hivi unashangilia wabunge ambao wote walikuja kuunga mkono juhudi
Ili la kupata wabunge wengi zaidi sina hakika sana, ila definitely ubora na heshima ya Chama ingeimarika sana na pengine wangeweza kuchukua kirahisi 2025.
 
Ok sawa umesikika Mwaka huu Mbowe anaachia uwenyekiti, natamani kuona unagombea nafasi hiyo muda huo ukiwadia. Hawezi kujiuzulu bali ataondoka kwa kuamua kutokugombea au agombee na asichaguliwe kwenye nafasi hiyo.

1. Sina hakika ni wapi umeona nimetamka neno kujiuzulu au kumhimiza yeyote kujiuzulu.

2. Sina hakika ni wapi popote nimemtaja Mbowe.

3. Kulikoni kutaka kuniwekea maneno yako mdomoni?

4. Nikukumbushe post yangu ya kwanza kwenye uzi huu ni #4 na ya pili ni #6 (nikiamini hayupo wa ignore list aliyekuwa ka comment kabla).

5. Ninakuwekea hapa post yangu hiyo #4 kama ni nia yako kujadili kwa hoja:



Angalizo:

Wala sikuwa nimefahamu uwepo wa uzi huu kabla ya kuitwa kwa heshima na taadhima na boss wako bwanq Proved ninayeamini anaithamini sana michango ya waungwana wasioendekeza uchawa popote.

6. Hapo kwenye angalizo, mabosi wako wengine waandamizi JokaKuu, Economist na wengine watafute faragha, sitashangaa kama watakwambia:

"kijana umekurupuka, tena big time."

7. Kuondoka au kutoondoka Kwa yeyote wapi unayasoma hayo? Kugombea au kutokugombea ni haki ya mtu yeyote isiyoweza kuchagizwa popote na awaye yote.

8. Hapo #7, ikiwa na maana kuwa umepoteza wakati kuandika mambo yako yasiyokuwa na maana kwa yeyote.

9. Suala la msingi ni kujikita kwenye mada. Hoja hujibiwa kwa hoja. Kulikoni kuja na mabo yako mfukoni kunishutumu nayo, nisiyoyatamka mimi?

10. Uzi huu uliotajwa pia pale post #4, uliwaangazia sana watu kama nyie wenye kudhani ni wapiganaji kweli kweli:

"Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM."

11. Hapo #10 ni kuwa hamjui kuwa mnaicheza ngoma ya CCM bila kujua. Misahafu inasema:

"Si kila aniitaye bwana bwana atauona ufalme wa mbinguni."

Pascal Mayalla kuna kijana wenu mwingine huku, hajijui tu. Anadhani u CCM ni rangi.
 

1. Sina hakika kwa nini kuhangaika kote kujaribu kuniwekea maneno yako mdomoni?
Nilivyoona bandiko lako nikajua ni wale wale ccm

Ni bandiko lipi uliloliona nisilolijua mimi? Tafadhali lilete hapa au unipe rejea ya bandiko hilo.

2. Ninakazia hakuna popote nilipojadili mtu au watu kama wao; kila siku ninajadili ninayoamini yanastahili kujadiliwa tena kwa uwazi na uaminifu wote.

3. Dhana ya kuwaingiza CCM kwenye nani wangetaka kuondoka au kubaki bila shaka ni tamu sana kwa chawa na labda hata CCM yenyewe.

"Hudhani kuwa CCM kumbe wakitaka mtu aondoke wanaweza kusema 'abaki,'' ili watu kama wewe waseme, atoke?"

4. Kwa mawazo kama yako ya kuendekeza kujadili watu badala ya hoja; bila shaka CCM wataendelea kutamalaki kwa muda mrefu sana!

5. Hata hivyo nielewe vyema, "tutabanana hapa hapa."

Jifunzeni kusoma hoja za watu kuelewa; acheni uvivu wa kusoma, kama mnadhani muingie kwenye mijadala. Acheni kukurupuka; msipoelewa ulizeni kupewa ufafanuzi kwa wahusika badala ya kuja na yenu yasiyokuwa kuwapo kuwahusu wao.

6. Ramli chonganishi hazilipi, hakuna aliye supernatural; kudhani unayajua ya mtu bila yeye kuyasema ni ujinga uliopitiliza.

"Kama ni kushukiana kiboya boya tu, kwa nini wewe usiwe hayo ma CCM? Kwa usiwe kuwa ndiyo uko kwenye agenda yao au yenu ki rasmi kabisa hapa sasa?"

Kushukiana shukiana huku ni mfano halisi wa mtu kujidhania yeye ni mwanachama zaidi kuliko wengine.

7. Tumeshauri mara kadhaa ni makosa ya msingi kwa CHADEMA, John Mnyika kuwaachia watu wasiokuwa na uelewa wa kutosha kukisemea chama na bila ridhaa yake.

8. Hapo #7, ni muhimu Chadema kama chama tena kwa dharura mno kuyafanya haya mapema iwezekanavyo:

CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

9. Wakisemee chama watu rasmi wenye weledi unaostahili. Wengine wote ni kujadili mambo "at the same level."

10. Tushindane hoja, si mahaba!

11. Proved, JokaKuu, Economist ikiwapendeza fundeni vijana hawa kama waheshimiwa hawa wanatingwa na yaliyo nyeti zaidi:

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama
 
Bado huoni kuwa amejustify alternative plan unayoipigia kelele!?
Ukumbuke vile vile kwenye maridhiano hakuanzisha yeye ila Samia na sasa anaongea fucken 4Rs!
Ukumbuke alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi wakati wanapanga huo mbadala kule Moshi?
Ameshamaliza zile njia zote za kidiplomasia na sasa ana haki ya kutangaza njia mbadala "maandamano"
Nadhani ungeweka msisitizo kwenye maandamano hayo badala ya kuja na mambo ya utumbo mpana ya kujiuzulu ambayo yatapoteza/yatachelewesha dira yote ya kisiasa.
Umeona Kuhaha kwa CCM hasa kupitia vyama vijikombi sasa eti wanapinga maandamano. Vimefadhiliwa na CCM. AU wewe ni mmojawao!!??
 
Umesahau ule msemo usemao "Mwonja Asali Huchonga Mzinga".

Je, twazifahamu "terms" za maridhiano?

Upinzani Tanzania haupo hili nimelisema mara nyingi huhu JF.

Wapo wasindikizaji na si wapinzani, na hiyo ni tokea mwaka 1992 siasa zinoitwa za upinzani na vyama vingi vilipoanzishwa.
 
Iko hiv, Kwa namna watu tukivyokua tumechoka na utawala wa sisiemu, ufusadi Kila Kona, ushikaji Kila Kona, ilikua ni yeyote kati ya wale vinara wa UKAWA kushika kijiti Cha urais. Wananchi hasa vijana wangeunga mkono Kwa nguvu zote. Kumleta Lowasa Kwa kua et atakuja na watu wengine, atakuja na pesa na blaa blaa zingine iliwagawa watu. UKAWA walipoteza mvuto Hadi hiv Leo.

CHADEMA ya enzi za 2007 Hadi 2014 huwez ilinganisha na CHADEMA hii ya Sasa. CCM hutumia akili kubwa katika ku execute plan zake. Ninyi mnaweza ona mmeokota dodo kumbe deep in, mejipiga wenyewe bila kujua.

Saiz Mbowe anaitisha maandamano, watu hawana mzuka na hayo maandamano. Trust me, mwaka 2015 immediately baada ya uchaguz, na CCM wasingemsimamisha ngosha wangempa mtu kma Maembe, then UKAWA Kwa pamoja wangeitisga maandamano, hayo maandamano yangekua na nguvu kubwa sana. CCM walikiona Hilo ambalo mtu kama wewe huwez liona. Ni simple but you need to go deepdown ndio utaelewa karata za CCM.
 

Nisaidie kumwambia pia kuna chama ambacho Mwenyekiti alikuwa Raisi wa nchi.
Mke wake yuko bungeni.[Mbunge]
Mtoto wake yuko bungeni. [Mbunge]

Je, CCM ni chama cha ukoo?
_________________________________________
Na chama hicho hicho CCM Kuna aliyekuwa Raisi wa nchi hapo zamani kule Zanzibar na badae JMT.[]
Mtoto wake nae ni rais wa Zanzibar.
Mtoto mwengine NI Balozi.
Mtoto mwingine ni mbunge.

Je, CCM ni chama cha u-koo?

Ila pia MWAMBIE mwenyekiti wa CCM taifa ambae kwasasa ni Raisi wa JMT ana mtoto ambae kule zanzibar ni mbunge

Je, CCM ni chama cha ukoo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…