1. Ikumbukwe kina Putin, Medvedev na sasa Trump (yuko njia moja) waliwahi kushika hatamu wakatoka na baadaye kurudi.
2. Mtu unaweza ukatoka ukarudi ukipenda ukiwa fresh na mawazo mapya. Ndiyo maana kuna likizo, rest and recuperation, sabbatical leave, nk.
3. Kukaa kiti kile kile muda mrefu inaweza kumpa mtu chronic fatigue na bila kujitambua akabweteka.
4. Leo chadema ina chawa na vijana wa hovyo kama wale wengine.
5. Hapo #4 hata nidhamu na heshima imekuwa changamoto.
6. Hapo #5 si ajabu illiterates na hata vijiweni na mitandaoni kuwakuta wanamzodoa Shivji, Nyerere, Mandela, Tutu, Lissu nk kiboya boya, kwa uchawa wao tu bila kujali jitihada, michango au mafanikio ya watu kama hao duniani, kwa jina la chama.
7. Kina
Nanye Go na wenzao wengi ni mfano wa watu hao ambao bila ya uhalali wowote, si nadra kuwaona na kujinadi kwa kudhani wao ni wanachama zaidi kuliko wengine, wakiwaitisha hata kama vipi kuondoka isipokuwa wao!
8. Kwamba hapo #7, vijana wa hovyo hawa, chama kimeshindwa hata kuwakemea hadharani? Ukiwa ni mwendelezo wa mapungufu ya yasiyo na afya ya yatokanayo na haya tunayoyaoigia kelele Kila leo kwa maslahi ya chama:
"
Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama"
9. Hapo #8, ni hali isiyoweza kuwavutia wenye kujitambua au akili zao chamani. Kwa hakika ni ujasiri wa kutokuwa tayari kuwasusia fisi bucha kuendelea kukomaa nao.
10. Hatuwezi kuendekeza ujinga, wajinga au kuwAendekeza watu wasiojua wanataka au hawataki nini kwenye mapambano yasiyohitaji ajizi kuwatia CCM madarakani.
11. Wanasema mjini kwa mwendo huu hatuwezi kutoboa!
12. Siyo siri, tunahitaji mwanzo mpya wa mawazo. Tulipo tumegonga mwamba.
13. Waungwana wanasema, "retreat is no surrender."