Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umaskini ni laana! Kumpa TAL chama, ni kukiuza kwa Robert Amsterda....Tundu Lissu kaiba nini na umasikini wake?
Hilo ndilo janga ninaloimaliza CCM!Hii hoja ya masikini wasiongoze uliwahi kuwaambia wenzio wa ccm?
Jamani huyo abdul si ndiye mfadhir wa huyo unaemnadi hapa au unadhani unajadir na mbulula wa kijaniMkapa .... Mama Anna Mkap... fisadi
JK.....Riziwan... fisadi
Saa100 .... ABDUL fisadi
Hizo ni siasa,uhalisia ni kuwa tumepigwa.Jamani huyo abdul si ndiye mfadhir wa huyo unaemnadi hapa au unadhani unajadir na mbulula wa kijani
Duh... Mambo ya kulinganisha mlima na kichuguu, lazima mlima utashinda, mgombea mmoja ataukacha huo mdahalo Je, CHADEMA wakubali au wasikubali Mdahalo wa Uenyekiti wa chama? Wenzenu CCM huwa hawakubali MidahaloUtangulizi
Mdahalo wa wagombea uenyekiti wa Chadema Taifa unatarajiwa kufanyika tarehe 18/01/2025, na ni tukio muhimu linalohitaji maandalizi makini ili kuhakikisha kwamba wagombea wanajitambulisha vyema kwa wajumbe na wapiga kura.
Katika muktadha huu, tunatoa ushauri kwa Chief Odemba ili kuwezesha mdahalo huu kuwa wa mafanikio.
ya jamii na kuhakikisha kwamba wagombea wanawakilisha maslahi ya wanachama na wananchi kwa ujumla.
Wasio kubali mdahalo ni wabakaji wa Demokrasia!Duh... Mambo ya kulinganisha mlima na kichuguu, lazima mlima utashinda, mgombea mmoja ataukacha huo mdahalo Je, CHADEMA wakubali au wasikubali Mdahalo wa Uenyekiti wa chama? Wenzenu CCM huwa hawakubali Midahalo
P
Ikungi haitaki kumsikia TAL.Kama anashida ya kujua maendeleo husika amtafute SAASISHA MAFUE mbunge wa hai na ndugu miraji mtaturu wa ikungi maana ndo wenye majimbo yao
Na ubongo pia.Kwa hiyo twende Butiama kule nyumbani kwa Mwl Nyerere tupime maendeleo ya huko ndo tuyathaminishe na uwezo wa mwl ktk kulitumikia taifa la tanzania? Hakika Lissu atawabomoa mapafu
Kwa hiyo Kwame Nkuruma, Mandela, Patrick Lumumba walikuwa matajiri ?Ni hatari sana kumchagua mtu maskin.... kuwa Kiongozi!
Trump mungu ambariki
Kwa namna ulivyoleta hoja zako unaonekana unamtetea Mbowe na humtaki Lissu sasa wewe mtetee mbowe nami nimtetee Lissu hapa JF tushuke nondo hapa kwa faida ya watz waliomo humu na hata wale wapitao (visitors)Hizo ni siasa,uhalisia ni kuwa tumepigwa.
Kwani alikuwa anakusanya kodi?Ikungi haitaki kumsikia TAL.
Kwenye uongozi wake ikungi,Kila mtu aligombana na mwingine.miaka mitano,hakuna Barbara,hakuna maji,hakuna shule,hakuna vituo vya afya na zahanati, hakuna umeme.
Utaelewa baada ya mwaka 2030, bibi akituacha mbuzi,Abdul anagombea urais anamteua Riziwan..kuwa waziri mkuuKwa hiyo Kwame Nkuruma, Mandela, Patrick Lumumba walikuwa matajiri ?
Sifa za uongozi ni kuwa tajiri?
Chawa siku zote huwaza kichawachawa tu,ajipendekeze kwa tajiri ili ajaze utumbo wake mpana.
Siku ya kupigiwa kura,atuambie kama ulivyosemaKwani alikuwa anakusanya kodi?
Wenye akili tulizijua fitna za ccm.
CCM imeleta ujinga mwingi kwa watz wasiofiki sawasawa
Kwa hiyo ukipewa hela ya kula na tajir tayari anafaa kuwa kiongpzi? Hivi upo sawa ndugu au ndo upo kibaruaniMkapa .... Mama Anna Mkap... fisadi
JK.....Riziwan... fisadi
Saa100 .... ABDUL fisadi
Dogo umeitoa mawazo mazuri ila nakuonea huruma maana kundi la wafuasi Tundu Antipass Lissu halitakuacha salama!Utangulizi
Mdahalo wa wagombea uenyekiti wa Chadema Taifa unatarajiwa kufanyika tarehe 18/01/2025, na ni tukio muhimu linalohitaji maandalizi makini ili kuhakikisha kwamba wagombea wanajitambulisha vyema kwa wajumbe na wapiga kura.
Katika muktadha huu, tunatoa ushauri kwa Chief Odemba ili kuwezesha mdahalo huu kuwa wa mafanikio.
Ushauri kwa Chief Odemba
1. Tembelea Majimbo ya Wahusika
Kabla ya mdahalo, ni muhimu kwa Chief Odemba kutembelea majimbo ya wagombea. Hii itasaidia kujiridhisha kuhusu kazi za maendeleo ambazo wagombea wamefanya katika jamii zao. Kwa mfano, Jimbo la Ikungi na Hai ni maeneo muhimu ya kutembelea. Kutembelea majimbo haya kutampa picha halisi ya mchango wa wagombea katika maendeleo ya jamii.
2. Kuweka Msingi wa Uelewa
Katika kutembelea majimbo, Chief Odemba atapata fursa ya kuzungumza na wananchi na wajumbe kuhusu maono na mikakati ya wagombea. Hii itasaidia katika kuelewa jinsi wagombea wanavyochukuliwa na jamii na pia kuweza kusimulia hadithi za mafanikio na changamoto walizokutana nazo.
3. Kutembelea Makazi ya Wagombea
Ni muhimu kwa Chief Odemba kutembelea makazi ya wagombea, hasa katika maeneo kama Ikungi na Hai. Hii itampa fursa ya kuona hali halisi ya maisha ya wagombea na kujua mazingira wanayoishi. Kutembelea makazi yao pia kutasaidia wajumbe kujua ni wapi watakapoweza kumtembelea mwenyekiti iwapo atachaguliwa.
4. Uhakiki wa Uraia wa Wagombea
Kabla ya mdahalo, ni muhimu kuhakikisha kwamba wagombea ni raia wa Tanzania. Chief Odemba anapaswa kufanya uchunguzi kupitia ofisi za uhamiaji na NIDA ili kuzuia uwezekano wa kumchagua mkimbizi kuwa mwenyekiti wa chama. Hii ni muhimu ili kudumisha uaminifu na usalama wa chama.
5. Mazungumzo na Familia za Wagombea
Chief Odemba anashauriwa kufanya mazungumzo na wake na watoto wa wagombea. Hii itasaidia kuelewa mtazamo wa familia kuhusu mgombea kugombea uenyekiti. Uwepo wa ridha ya familia ni muhimu katika kusaidia mgombea kuwa na nguvu na kujiamini.
6. Kujua Mchango wa Wagombea kwa Chama
Ni muhimu kwa Chief Odemba kupata mawazo kutoka kwa wagombea kuhusu mchango wao kwa chama katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Hii itasaidia wajumbe kuelewa historia ya wagombea na jinsi walivyoweza kuathiri chama katika nyanja tofauti.
Hitimisho
Mdahalo huu ni fursa muhimu kwa Chadema kuweza kuwasilisha viongozi wazoefu na wenye uwezo. Kwa kufuata ushauri huu, Chief Odemba atachangia kwa kiasi kikubwa katika upeo wa wagombea na kuimarisha demokrasia ndani ya chama.
Ni muhimu kuzingatia maoni ya jamii na kuhakikisha kwamba wagombea wanawakilisha maslahi ya wanachama na wananchi kwa ujumla.