Ushauri: Miaka 6 kazini, mishahara haikutani

Ushauri: Miaka 6 kazini, mishahara haikutani

Wakuu nina miaka 6 kazini, lakini naona hata nikiacha kazi leo sina future wala hela ya kula mwezi mmoja.

Nilianza na mshahara wa laki 6 leo nina mshahara wa 2.9M lakini hadi leo sina project wala uwekezaji wowote.
Nimeishia kujenga nyumba mbili tu moja kijijini nyingine mjini na zote hazijakamilika yaani zimepauliwa tu zikaishia hapo hapo.

Sijui nakosea wapi mshahara ukitoka haumalizi siku moja unakatika...madeni, bills na changamoto za ndugu.
Nilianzisha kibiashara ya consultation niliishia kupata mteja mmoja tu hadi leo hamna.

Wakuu nifanyaje maana sioni mbele na familia inazidi kukua...
Sina gari, sinywi pombe na sina uraibu wa aina yoyote hata mademu pia...ila pesa ndo hamna muda wote
Mbona mshahara mkubwa sana huo mkuu, mimi nina 1.2 na Mishahara hukutana.. Ningekuwa na huo wako nazani nisengekuwa naendesha Crown Athlete bali Mercedes Benz au BMW
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] malalamiko ya.mishahara imekuwa mingi sana mkuu.
Pole sana kwa unalopitia na nikuhakikishie kabisa hauko peke yako ni mtego ambao waajiriwa wengi wamenasa.
Hapo namba 1 ni kwamba una matumizi makubwa kuliko pesa uipatayo na kadri upatavyo pesa nyingi basi unakuta inakulazimisha kufanya matumizi makubwa pia.
Mengine unakuwa hata huna umuhimu nayo ila tu kwa kuwa pesa ipo basi wakuta umefanya.
Ku solve.
Hakikisha unapanga kabla matumizi ya mwezi.
Tenga kiasi kwa ajili ya dharura(kukopesha kutoa kwa rafiki na ndugu). Kiwe fixed hapa mtu atakayekuja baada ya hiyo hela kuishi hapati kitu.
Then jizoeshe kufanya matumizi ya kawaida ndipo utaona pesa yako inabaki.
Hakikisha wewe ndio una i control pesa na si pesa ina ku control wewe.
Pesa ni kama mpira wa miguu ule.Vile unaona mtu anauchezea na ku u control vile atakavyo wakati mwingine anashindwa hata dana dana moja unakuwa umemtoka mguuni.Tatizo linakuwa ni mchezaji na si mpira kwakuwa mpira hauna akili bali mchezaji ambaye anaweza tumia akili yake akaufanya anavyotaka ukatii.
Nb: Nidhamu ya pesa ni muhimu mno hapo
Hii coment naiscreenshot isiije kunipotea. Nilipoona huu uzi nilidhani nimeandika mimi kwa uwezo wa roho mtakatifu.
 
Mleta mada mkeo ni jobless? unaishi kwa sifa na kujitutumua kwa watu wakuone boss?
Kama huwezi fanya saving kwa salary hiyo hata ukilipwa 100M kwa mwezi bado utakuja kuomba ushauri humu ndani.
Hiyo consultation firm yako inajihusisha na nini?
Ukijibu hayo nakupa way forward!!
 
Back
Top Bottom