Ushauri: Mke kamalizia kulipa gharama ya kiwanja ambacho mume wake alikuwa anamnunulia mchepuko


Yaani we ndo mwaminifu hivyo???!duh nifundishe na mm kabla niingie kwenye ndoa
 
Mimi niwapongeze tu kwa kujua kutunza wake zenu na michepuko yenu.

Mna nafasi ya pekee huko mbinguni.

Ushauri watakuja kutoa wengine.
Ahsante kwa muongozo.
 
Hivi mnafikiri hizo password hatuzijui eeeh??
 
Hapo cha kufanya

Akaandijishiane

Na akitaka kujikosha aandike jina la mke au aandike watoto.

Akane kabisa kama alikuwa ananunulia mcheps

Ila sheneji hautoaminika tena....ushaingia kwenye kundi la wale wake.

Halafu jamaa yako aogope sana mke anayejifanya hajui kitu. Au unayemdanganya tuuuu anakusikiliza hakujibu au anacheza na beats zako anapokea tu uongo wako.

Ni bomu la nyuklia hilo!!!
 
Katika jambo ambalo huyu mzee hatakiwi kulifanya ni kumdanganya huyu mama tena maana mama anaujua ukweli asilimia 200 ndo maana alileta zile mil 2[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] So asimdanganye ila ambadilishie kibao tuu akomae kiwanja ni mali ya familia.
 
Labda kama una mtoto nae ili ukimjengea nyumba iwe ya mtoto. Kama huna mtoto nae ni upotevu wa bure wa pesa za kutunza watoto wako. Ina maana umeijengea familia ya hawara!!! Acheni hizo!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Story zako kila siku ni mambo ya michepuko tuuu una akili kweli wewe!!!hebu grow up walau kidogo enh
 
Walisema wahenga

1. Hakuna marefu yasiyo na ncha

2. Hakuna siri chini ya jua

3. Kila mchuma janga hula na wa kwao

Halafu wanaharakati wakasema ''Michepuko sio dili''
 
Kwanza, wewe ni sehemu kubwa ya tatizo. Kama jamaa ni rafiki yako wa kweli, unamshaurije amjengee mchepuko nyumba. Ukiwa rafiki wa kweli na ambaye huhusika hata kuwasuluhisha, wewe unategemewa pia kumuongoza rafiki yako kutunza ndoa yake. Kama ana mchepuko ni vizuri usihusike katika maswala ya mchepuko kwa sababu siku za mwizi ni arobaini na itakapobainika si tu unajuwa kila kitu bali wewe ndiyo mshaurui mkuu...utafanyaje! Shame on you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…