Ushauri: Mke kamalizia kulipa gharama ya kiwanja ambacho mume wake alikuwa anamnunulia mchepuko

Ushauri: Mke kamalizia kulipa gharama ya kiwanja ambacho mume wake alikuwa anamnunulia mchepuko

Mkuu!
Ni kweli unashangaa kwanini hajakuambia lolote au umefanya maamuzi ya makusudi kuamua kushangaa!![emoji848]
Sio kawaida yake,
Kukiwa na sintofahamu na mumewe Mimi Ndo HUWA mtu wake wa kwanza kuniletea kesi
 
Kesi ndogo hiyo; akae na mkewe wamalizane, kuhusu mchepuko asijengewe nyumba ila ampe kiasi cha fedha huyo mchepuko akanunue mwenyewe anapojua.
Kukaa nae sio rahisi kiivyo Maana MKE mpk sahv hajasema chochote[emoji4]
 
Mwambie mlitaka kumfanyia suprise ko umefanya haraka kwenda yeye kumalizia huku mkiwa na tabasamu.wewe shemeji na unaharaka kimalizia kabla ujakabidhiwa mali yako
Ila Nadhan mpk yeye atuanze
 
Hahah
Mtani ukijengea nyumba mwanamke, oa kabisa awe mke wa pili au tatu au nne na kuendelea...

Sasa unapambana kujengea mtu nyumba ambaye anakuja kuwa mke wa mtu mwingine baadaye...shabash!!!
Mchepuko anauejengewa nyumba ninmke wa pili unofficial[emoji4]
 
Hii kesi ni balaa!
Inawezekana mchepuko na mke wa jamaa wakawa na Mawasiliano au Kuna mtu wa kati alichoma huo mmchongo! Kama mpaka kiasi kilichobaki amekijua na eneo lililipo amepajua na mwenye eneo amemjua hapo mtajibeba
We jamaa jitoe kabisa kwenye huo mgogoro jifanye hujui chochote isipokuwa ulienda kama shahidi na ulijua ni Mali ya familia hayo ya michepuko hayakuhusu hao mke na mume watamalizana wenyewe
 
Kumbe kuwa mchepuko hakuna tofauti na mke. Huduma kama zote
Michepuko wanaroga hao wanashinda sana kwa waganga kuna rafiki yangu ndo anafanya hayo mambo anasema wateja wake wengi ni wanawake walio kwenye ndoa wanawaroga madanga wasikimbie we chukulia tu mfano majizzo kudata kwa lulu sio akili za kawaida zile mtu katulizwa pale uanaume mateso tu,

Kazini unarongwa
Mke anakuroga
Mchepuko anakuroga
Ndugu wanakuroga ili usiwasahau

Mungu ndio wakutuokoa ndio maana tunakufa mapema.
 
Halafu wakati huo kuna bibi au babu yako mbwinde huko anaishi kwenye nyumba ya nyasi inavuja kinoma...
..ni upuuzi wa hali ya juu. Kuna wakati wanaume tunakuwa wajinga sana kwa maamuzi yasiyo na tija kwa future yetu na ya watoto wetu.
 
Tatizo la watu wanadhan Kumjengea Mchepuko Ni gharama Sana.

Bila kujua umesevu Kias gani kumjengea kutokana na kulipa Kodi mfulurizo ambazo huenda zingetosha kujenga nyumba ndogo ikakamilika kabisa kuishi.

Nitoe mfano:
Kuna Jamaa juz humu katoka kumlipa Mchepuko Kodi ya mil.4.8 kwa mwaka, na bado utaendelea kudaiwa.

Hii pesa ukiilipa miaka 5 sio Chini ya mil.24 ambayo ingetosha kabisa kujenga nyumba na ukaachana kabisa na kulipa kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyumba ya thamani ya mil.24 ? Ni sehemu gani hiyo unaweza kujenga nyumba ya 25mil.
 
Wakuu

MDA SI mrefu nmetoka kupigiwa Simu na rafiki yangu mmoja wa karibu Sana Ni DOKTA hospital moja ya wahindi hapa mjini,Na anamiliki duka moja la dawa za binadamu kubwa Kiasi ambalo suka ilo mkewe ndo muuzaji na msimamizi mkuu wa kila mara. Sasa Jamaa kapigia akinipa taarifa nzito sana khs jambo moja.

Ni kwamba
kile kiwanja nilichosaini Kama shahidi wake kwa ajili ya manunuzi na kumjengea mchepuko wake nyumba tayar kaenda MKE wake na mil 2 cash pesa ilobaki ili kukimalizia kabisa.

Ni Hivi wakuu,
Katika harakati za hapa na pale, jamaa yangu uyu nilimshaur Bora amjengee TU mchepuko wake maana Kodi anakokaa anayomlipia kubwa Sana na inamuumiza (double ya nnayomlipia mchepuko wangu mimi).Jamaa kweli akakubali.

Kiwanja kimetafutwa kimepatikana na maafikiano yamefikiwa kilipiwe pesa mil. 8 cash ila iwe ni kwa installment 3 ndani ya miez 3 tu.
Yaani [emoji117]January tulipoenda wote kililipiwa mil 3 cash- Tukasainishana awamu ya kwanza tukaondoka.

[emoji117]February, - Jamaa akamuingizia TU mzee Ela mil.3 kwenye bank. Akanipa taarifa tu ila Hatukwenda kule saiti kusaini. Mzee akasema tutakuja kusainishana mwishoni kabisa tukimaliza biashara.

[emoji117]Jana anasema kapigiwa na mzee mwenye kiwanja kwamba mkataba uko tayar Mbona haji wakakabidhiane na viongozi wa serikali. Kila Siku anapiga kalenda.

Jamaa akajitetea mzee amvumilie kwanza mpk amalizane na TRA tar 30 March kwenye maswala ya Kodi ya mapato. Mzee akamjibu kwamba mbona ela iliyobaki tayar ishalipwa, ililetwa na mama (yaani mkewe).

Mzee Anasema Kuna mmama alimpigia akijitambulisha kwamba mme wake DOKTA flani kampa maelekezo pesa ilobaki mil.2 cash aje aimalizie, sasa wakutane wapi akabidhiwe?

Mzee kamjibu kwamba wakutane saiti maana Hakua mbali na pale. Akasema mama mwnyw alikuja na gari yake ile ile jamaa aliyokuja nayo siku ya mwanzo pale saiti kwake Akiwa Yuko na mtoto mdogo na binti mmoja kafunga nywele kwa juu kuja kumalizia Ela.

Na kuondoka zake kwamba mkataba watakuja jumapili ijayo.Jumapili imefika hawajaja Ndo ikabd ampigie jamaa. Sasa Jamaa akasema kwa maelezo yake akahisi labda mzee yule anamjaribu. Ila Kama ni gari Huenda iwe imetumika wikendi TU maana ndo humuachia mkewe apeleke Watoto wake kanisani, yeye ubaki nyumbani kupumzika.

Sasa Leo jion kaenda kumhoji binti wa kazi kama Kuna sehem yoyote alienda na mama ake, binti kweli kakiri Kuna mahali jumapili moja walienda na mama ake baada ya kutoka misa nje ya mji kidg.

Ila yeye alibaki kwenye gari mama akaenda kuongea na wazee flani, baadae mzee mmoja akawa anamsindikiza mpk kwny Gari wakasalimiana ila yeye akujua walienda kufanya Nini kule Maana mama akumwambia kilichompeleka mpk wanarudi.

Sasa Jamaa kachanganyikiwa apa kaniomba ushaur afanyeje kulimaliza hili.Nmemwambia nipe muda nitafakari Kwanza tunafanyaje.

Kiukweli
Mimi mwnyw hata Cha kumshaur sahii Ni kipi nmekosa.

Maana Kama kweli yule MAMA alijua nilikua shahidi tayar nishajijengea chuki kwamba nmehusika kwenye dhambi ya mmewe. Mimi na mmewe Ni wale wale.

Afu kibaya zaidi Mimi Ndo huwa msuluhishi wao kila Mara pale wanapogombana, shemej huja kushtakia kwangu Nawasuluhisha.

Sasa kwahili nashangaa shemej yangu hajaja kunambia chochote.

Yaan Shemej yangu uyu huwa ananiamini Sana kias kwamba ata jamaa akienda kwenye Mambo yake akimwambia TU kua Yuko namimi, mkewe anakua na amani KABISA mmewe Yuko sehem salama.

Kwenye ugomvi shemej anamshaur kila mara kufuata nyayo zangu jins nilivotulia na familia yangu bila mambo mengi ya michepuko michepuko.

Sasa
Nishaurini vema niweze kumshaur vizur uyu jamaa yangu ili kuokoa ndoa yake.

Pili nishaurini namuingia vipi uyu shemej yang Kama kweli akija kujua nmehusika kwny kile kiwanja kwenye dhambi ya mmewe. Napangua vipi mapigo.

NAWASILISHA[emoji120]
Kiwanja mliandika jina la nani? Tuanzie kwanza kaka
 
Back
Top Bottom