USHAURI: Mke wangu anamatumizi makubwa ya fedha yanayosababisha tuwe tunagombana sana

USHAURI: Mke wangu anamatumizi makubwa ya fedha yanayosababisha tuwe tunagombana sana

Wanaume wanao taka ushauri kuhusu wake zao ni wengi
kuliko wanawake ambao wanakuja kuomb ushauri kuhusu waume zao dah!
sasa sisi ambao bado hatuja oa sijui kama tutaoa,
kuna brother moja aliwahi kunambia 'asinge kua ameoa asingeoa.' mpaka leo sijawahi kuielewa kauli yake
 
Mimi nimeoa na naishi ya familia yangu, wote tumeajiriwa ila wife ndiye aliyenifuata mahali ninafanyia kazi. Tumegombana na huwa tunagombana mara Kwa mara shida kubwa mwenzangu Huwa anamatumizi makubwa kuzidi kipato chetu.

Na mara nyingi nimekuwa nikimwelewesha anakuwa mbishi mpaka anakopa halafu mwisho wa siku mlipaji ni mimi, juzi aliniudhi nilikuwa na safari yangu nikiondoka home bila ya kumweleza napokwenda, ila kesho yake usiku nikawa nimerudi.

Sasa mwenzangu naona amefura anataka kuomba kuhama kmya kmya nibaki peke yangu, Wala haongei na mimi chochote tokea juzi, Sasa kwenye mazingira ya namna hii nifanyeje?
Piga chini ana mtu anaempa jeuri hata hayo matumizi
 
Kwahiyo mkeo akiwa na matumizi ndio unaondoka nyumbani unalala huko huko bila kuaga???
 
Mimi nimeoa na naishi ya familia yangu, wote tumeajiriwa ila wife ndiye aliyenifuata mahali ninafanyia kazi. Tumegombana na huwa tunagombana mara Kwa mara shida kubwa mwenzangu Huwa anamatumizi makubwa kuzidi kipato chetu.

Na mara nyingi nimekuwa nikimwelewesha anakuwa mbishi mpaka anakopa halafu mwisho wa siku mlipaji ni mimi, juzi aliniudhi nilikuwa na safari yangu nikiondoka home bila ya kumweleza napokwenda, ila kesho yake usiku nikawa nimerudi.

Sasa mwenzangu naona amefura anataka kuomba kuhama kmya kmya nibaki peke yangu, Wala haongei na mimi chochote tokea juzi, Sasa kwenye mazingira ya namna hii nifanyeje?
Mwanamke akishakuwa na matumizi makubwa,simply ni kwamba anatamaa,na mwanamke mwenye tamaa huwa haoni kazi kufanya uovu kuitimiza tamaa yake ,huo ni mtihani,huyo sio mwanamke ni kibaraka wa ndoa,"" Tunaishi na wake za watu ambao wapo katika sura nafiki ya wake zetu,akikuzingua mzingue,akikusumbua mpumzishe"
 
Muache aondoke uishi kwa amani furaha baraka na kuinjoi maisha... Ukimuendekeza utakufa kwa presha utuachie wahuni mke na mali zako
 
Hakuna kubembeleza mwanamke

Fukuza huyo akajifunze adabu kwanza.
Afukuze kama alivyofanya mfalme Ahasuero kwa mrembo Vashti na kuopoa mrembo mpya Ester. Hakuna jipya chini ya jua, kumbe yale yaliyokuwepo ndio yaliyopo.
 
Back
Top Bottom