Ushauri: Mke wangu anawasiliana na X wake

Ushauri: Mke wangu anawasiliana na X wake

Nimegundua kwamba mke wangu wanawasiliana na ex wake. Niligundua baada ya kuchunguza nikamkataza, Ila nikachunguza nikagundua bado wana mawasiliano mana meseg zinaonekana ni za kimapenzi, isitoshe mke wangu ana mimba ya miezi miwili.

Ushauri wenu wadau, niko juu ya mawe.
Una hela?
Una piga show za uhakika?
 
Hivi wanaume siku hizi tumekuwaje au tunerogwa?
Yaani na hili ni la kuja kuomba ushauri kweli?

Acha tu na ndio maana huwa nawaza hawa ni Game Changer and Spin Doctors ,wanaleta mada zenye hisia kuteka watu humu na kuwahamisha kwenye mijadala yao.

Swala kama hili ni kweli unataka ushauri? Ushamkataza wife wako asichat na x wake then anarudia na mimeseji ya kimapenzi then anataka tumshauri.
 
Ndio shida ya mapenzi....

Kumuacha unatamani lakini unazidiwa na penzi..

Asali chungu!

Mfate huyo ex .. ..ukiwa na ushahidi na mtu mwengine.. yaani muwe wawili.. muweke mtu Kati.. muonyeshe upupu wake anaotumiana na mkeo! ..

Usimuonye Wala kumkataza ... ..ondokeni tu kimya kimya..

Niamini..atakoma !

Au muonyeshe mkeo kwamba unajua kinacho endelea ... Wasubirie majibu..
Bi dada atajinyoosha mwenyewe ..kukaa au kuondoka!

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Hivi wanaume siku hizi tumekuwaje au tunerogwa?
Yaani na hili ni la kuja kuomba ushauri kweli?
Kabisa, hiyo si Iko wazi kabisa jamaa ameoa mke wa mtu?

Atafute mke wake, huyo sio mke wake.

Wanawake wanaelewa sana kuhusu hii kitu.
 
Duh pole sana kijana nina wasi wasi ata mimba ikawa ya uyo mwamba
 
Nimegundua kwamba mke wangu wanawasiliana na ex wake. Niligundua baada ya kuchunguza nikamkataza, Ila nikachunguza nikagundua bado wana mawasiliano mana meseg zinaonekana ni za kimapenzi, isitoshe mke wangu ana mimba ya miezi miwili.

Ushauri wenu wadau, niko juu ya mawe.
Sasa broo tukushauri nini, subiri ulee watoto wa mwanaume mwezio, au umbukizwe ukimwi.
 
Hivi wanaume siku hizi tumekuwaje au tunerogwa?
Yaani na hili ni la kuja kuomba ushauri kweli?
Unaropokaa maana hajakukutaa

Siku yakikukutaaa utajinyongaa nivyokujuaaa.

TUTAIMBA RIP
 
Ushauri wangu Mkuu

Usiwe na papara kaa naye uongee naye kwa undani ujue kwanini

Anafanya hivyo shida iko wapi

And uwe makini maana wanawake wajawazito wana vimbwanga anaweza kukujibu lolotee.
Kama ni mke wako hali wa ndoa
Mtishe muambie ntakurudisha kwenuuu
 
Unataka ushauri tena, vipi tukwambie umsindikize lodge akatafunwe kabisa au!! 😡😠

Wanaume siku hizi tuna matatizo gani, umekataza hasikii piga chini,
Ama tega mtego uwakamate uwale viboga, kisha mpe mkeo talaka akakae na mwanamke mwenzie.
 
Back
Top Bottom