Ushauri: Msaada kuhusu tabia ya wizi iliyokubuhu kwa kijana wangu

Ningeweza kujaribu haya mkuu lakini tumechelewa amesharudi kwao tayari
 
acha kujipa umuhimu kwenye maisha ya watu.... kwahiyo ukisifiwa kwrnye harus then nini kinafata..... watu watakusaidia kulea kwa uwezo wao lakini sio ususie watu wengine mzigo wako
 
Wizi ni ugonjwa wa kijenetiki ambao hauna dawa.

Uliposema ukijutia kulea mabao ya watu, umemaliza kila kitu.

Wizi ni roho ya tamaa na ubinafsi anayozaliwa nayo mtu.

Hapo kama ukoo wenu hauna tabia za namna hiyo, basi hiyo tabia ipo umamani kwa wajomba zake.

Tabia hiyo haina ushauri wa mzazi ama ushauri nasaha, inatakiwa ikumbane na adhabu tu za bila maonyo, kumuonya mwizi ni sawa na kumpiga teke chura.

Lazima mwizi apambane na visago mbali mbali ndiyo anaweza kubadilika hata kwa mbinu anazotumia kuiba, lakini si kupona ugonjwa wa wizi.

Huo ugonjwa mtu huwa haponi ni laana, hauoni taifa linavyohangaika na mafisadi bila kuwashinda ama kuwamaliza, hivyo ni vimelea vya tangia utoto wao.

Kabidhi kwa baba yake mzazi akahangaike naye, wewe hautamuweza, siku1 waweza piga ukazidisha ukaua, baadaye ukajikuta upo Kisongo ukipiga stori na mheshimiwa Sabaya.
 
Huyo ana pepo la uwezi humuwezi mludishe kwa baba yake halafu baba yake ampeleke kanisani hilo ni tatizo
 
Wageni ni baraka.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Kabla uzi haujaenda mbali sana mkuu tumia kikao hicho kumkabidhi huyo mtoto kwa baba yake, yaan agenda za kikao ni tatu moja kufungua kikao, mbili kumkabidhi huyo mtoto, tatu kufunga kikao.
Ukiendelea kuwa nae litakukuta Jambo asee
 
Mkuu, uyo dogo muondoe, utakuja kuua. Muondoe mapema, hawezi badilika huyo, baba yake alimlea vibaya, wewe huwezi kumrekebisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We mwenyewe Mkuu utakuwa maji ya baridi,Mitoto kama hiyo unailea Kiscout yaani kama yuko Jeshini mpaka mwenyewe anaomba kwenda kwa Mzee wake.
 
Kumlelea mtoto mzazi mjinga yaani unamwambia mwanae ni mwizi(huyo sio mdokozi tena)alafu anatetea ujinga

Chukua zigo rudisha kwao kama swala ni kusomesha chukua mwingine

Dah,hilo ni jambazi tyari na kuacha hawezi yani
Ukute huyu baba yake dogo ndio alimlea Pancho
 
Komaa nae mpaka abadilike utakuwa shujaa wa familia....wanaume huwa hatukimbii matatatizo tunayatatua kwa njia yeyote afe kipa afe beki.
 
hapo wazaz walishamshindwa wakakuletea wewe! sasa hii tuite nini extend family au? yaan kuzaa wazae wengne kulea alee mwingine!. haya mpe mheshimiwa balozi aende naye Mozambique huyo.
 
Wewe ulichangia kumharibu kipindi anaiba halafu unamwangalia, ila haujachelewa (samaki mkunje angali mbichi). Tembeza adhabu dogo atabadilika.

Ni aibu mzazi kushindwa na mtoto mdogo!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Chunguza katika ukoo wenu alishawahi kuwepo mtu mwenye tabia kama hiyo tena huyo anaiba anauza mimi nnao mfano wa hapa yupo dada yangu ni tena anamaisha ya kawaida hana njaa na kazi anafanya nzuri tu ila baba huyu ana tabia za wizi ambazo amerithi yaani anaiba ile mbaya kesi zake ni za wizi kila anapoenda kufanya kazi basi ukisikia katimuliwa ujie keshaiba huwa namuangalia mpaka najskia nishai nayeye amezaa mtoto nae ni mwizi kama yeye.Huyo msamehe tu pia mpe somo atakuja kupasuka uswahilini.
 
Nashauri mpeleke hospitali, madaktari wa afya ya akili wanaweza kuwa na msaada kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…