Ushauri: Msaada kuhusu tabia ya wizi iliyokubuhu kwa kijana wangu

Nenda polisi kaongee nao, ili baadae uende na mtoto wampige mjwara mzito
 
Wakuu.
Kwenye kikao jana ndugu wote walikuwepo akiwemo kaka yangu (baba wa huyu mtoto)
Niliwaeleza mengi kuhusu ilivyo licha ya wao kunilaumu kama kawaida.
Tulifikia hata kukwaruzana kabisa kwamba wanasema wizi amejifunzia hapa kwangu , kitu ambacho naweza nikakubali au kukataa, sababu ninampa mahitaji yote.

Hivyo muafaka uliopatikana ni kuwa dogo arudi kwa baba yake lakini nitatuma pesa Za shule na mambo mengine kama kawaida.

Amelia Sana na kujutia pia kuomba msamaha lakini nilipofikia inatosha kabisa tena Sana,

Pia wakati wa kikao dogo alidai kuna mwanafunzi mkubwa shuleni kwao huwa anamtuma hela asipoleta anapigwa..!

Tukasema mtaje twende shuleni kwa mwalimu mkuu ili tumuwajibishe, dogo akaruka kiunzi kwamba amedanganya?

Ni hayo tu wakuu ninawashukuru Sana kwa michango yenu iliyotukuka nyote kabisa hakika mmenisaidia Sana...
Pole Sana atabadilika tu Kuna wakt nilikuwa na tabia za hvyo vya udokoz udokoz Ila iliisha automatically Bila kujua na Wala sipendi na siwapendi wezi kbsa
 
Mkuu tatizo hapa ni mtoto wa mtu ni bora akiwa mwanao huyo utakufa naye,hapa shida iko hivi
Akimuacha anavyozidi kukua ndivyo wazazi wake watajivua na kusema dogo wizi kajifunzia kwa baba yake mdogo kwakua amekulia hukohuko,hapo ajiandae kubeba lawama zote ikiwa ni pamoja na malezi mabaya hata kama wanajua kwao alikuwa mdokozi
Pili ikitokea la kutokea bahati mbaya dogo akajeruhiwa au kuuwawa kwenye harakati zake,anaweza kutengwa mpaka na ukoo mzima,wanadamu waone hivihvi
Ndiyo maana nasema ajalibu kwa kila namna kumrekebisha tabia ikiwa ni pamoja na kufanyiwa maombi. Kamwe lawama hataziepuka. Akimrudisha atalaumiwa kuwa hataki kusaidia au kuishi na ndugu. Akipatwa na matatizo kutokana na tabia yake atalaumiwa kuwa ameshindwa kumsimamia. Hivyo lawama haziepukiki.
 
Wakuu,

Naamini kila mtu huwa anakosea, lakini linapokuja swala la kukosea mara kwa mara huwa linatia hasira sana.

Huyu mtoto wangu anasoma darasa la 6 ,ni mtoto wa Kaka yangu alimleta hapa kwangu ili asome,

Sasa kinachozidi kunipa wasiwasi ni tabia yake ya wizi uliokubuhu!

Yaani kwa umri wake na vitu anavyoiba nabaki mdomo wazi kabisa.

Sijawahi hata kumuadhibu lakini jana imenipasa baada ya yeye kuuza simu tatu kwa bodaboda tatu wakuu!

Bora hata angeuza bei kauza elfu 7.

Alishasema mara nyingi harudii lakini ni yale yale nimempiga na leo hawezi kutembea wa kwenda shule amelala tu.

Alishaiba hela sana ndani huwa nina tabia ya kuweka noti ndogo ndogo kwenye dressing table pale, so anapokuja asubuhi kuomba hela ya kula shule namwambia achukue buku yeye anapita nazo zote huwa nanyamaza tu.

Alishaiba baiskeli ya wenzie shule wakamfuata mpaka huku nyumbani kwangu niliskia aibu sana nilipoambiwa hilo.

Aliiba laptop ya mwalimu! Najiuliza aliwezaje nayo pia walimdaka nayo.

Vingine ndani vitu anauza mfano aliingia Store akauza pampu, aliuza charge ya simu, flash disk yangu pia yenye documents muhimu sanaa aliuza!

Sasa chai anakunywa asubuhi, pesa ya kula shule ninampa, lakini bado anaiba nimekosea wapi? Nikimwambia kaka yangu huko kwake ananilaumu na ndugu wengine kuwa nimemuharibu mtoto wake.

Kuna jirani alisema nimpeleke dogo polisi, hili haliingii akilini polisi kufanyeje sasa kwa mtoto mdogo kama huyu? Si nitamuharibu zaidi?

Mbaya zaidi na kanisani huwa anaenda kila Jumapili.

Nahofia kanisani atakuja kuiba sadaka.

Aliwahi pia kuiba pesa za wageni wangu 65k nikamsachi na kumkuta nazo, imagine aibu niliyoipata!

Nilimnunulia mpira na viatu vya kuchezea soka, lakini cha ajabu aliuza huo mpira, viatu mpaka kijazio!

Hii shida ya kulea mabao ya watu ni ushenzi sana!

Nishauri wakubwa.

UPDATE :
Leo kutakuwa na kikao hapa kwangu ndugu wengi wamekuja wengine hawajafika akiwemo baba wa huyu dogo.
Lengo lao likiwa ni kujadili namna ya kumsaidia lakini mimi binafsi nimenyoosha mikono juu niko radhi kuwaambia ukweli kwamba amenishinda hivyo baba yake aondoke naye mpaka mwisho wa kikao tutajua.
Hana shida, ni tatizo la kiroho zaidi. Dozi iliyopo kanisani kwenu bado haimtoshi. Jaribu kumpeleka kwenye makanisa ya Walokole akaombewe. Popote pale. Kwa kuanzia, unaweza ukampeleka kwa Bull dozer Mwamposa au kwa Nabii Suguye
Usipofanya hivyo inabidi ukae standby siku moja kufikishwa Polisi ukiwa una kesi, wewe kama mtuhumiwa! Mpeleke kwa Walokole. Mimi ni mmoja wao, naelewa ninachokueleza hapa
 
Mkuu swali ni je akiiba pesa anafanya nayo nini?Ukiweza kujua matumizi yake ya pesa unaweza jua uanze kumsaidia vipi.
 
Pole Sana atabadilika tu Kuna wakt nilikuwa na tabia za hvyo vya udokoz udokoz Ila iliisha automatically Bila kujua na Wala sipendi na siwapendi wezi kbsa
Kubeba laptop, simu nafikiri dogo, kahama kwenye udokozi kawa wa next level!
Kuchukua buku buku 2 ni tofauti na kudondoka na simu za watu unaziuza bei chee!
Yaani kapitiliza!
 
Ana baba ake muondoe angekua wako ningekushauri kitu ila huyo utapata lawama
 
Nimeongea na dogo hapa sasa hivi nimemwambia nimrudishe kwa baba amekataa kabisa analia anadai nimsamehe harudii tena lakini alishaomba msamaha mara nyingi Sana

naumia Sana nampenda huyu ni damu yangu kabisa.
Huruma inakuponza mrudisheeee utajutaa kanafiki hakoo
 
Wakuu.
Kwenye kikao jana ndugu wote walikuwepo akiwemo kaka yangu (baba wa huyu mtoto)
Niliwaeleza mengi kuhusu ilivyo licha ya wao kunilaumu kama kawaida.
Tulifikia hata kukwaruzana kabisa kwamba wanasema wizi amejifunzia hapa kwangu , kitu ambacho naweza nikakubali au kukataa, sababu ninampa mahitaji yote.

Hivyo muafaka uliopatikana ni kuwa dogo arudi kwa baba yake lakini nitatuma pesa Za shule na mambo mengine kama kawaida.

Amelia Sana na kujutia pia kuomba msamaha lakini nilipofikia inatosha kabisa tena Sana,

Pia wakati wa kikao dogo alidai kuna mwanafunzi mkubwa shuleni kwao huwa anamtuma hela asipoleta anapigwa..!

Tukasema mtaje twende shuleni kwa mwalimu mkuu ili tumuwajibishe, dogo akaruka kiunzi kwamba amedanganya?

Ni hayo tu wakuu ninawashukuru Sana kwa michango yenu iliyotukuka nyote kabisa hakika mmenisaidia Sana...
Ameen ameen afadhali bora lawama kuliko fedheha
 
Nimejiskia kusikitika, Nimejiskia kucheka, Nimepata mixture of feelings,Mtoa mada nakufananisha na Mama Yangu mzazi alienitoa tumboni mwake,Huyo mtoto najifananisha na mimi,halafu sasa huyo mtoto mimi ni clone wangu

mimi ndie ORIGINALY yani huyo ni COPY enzi za utoto wangu mimi ndie nilikua OG Kuna kitu hujakijua kuhusu huyo mtoto,fimbo haitomsaidia wala kumbadilisha,mimi mwenzako nilishaloekwa hadi kwenye Beseni na Biblia,nishafungiwa Room kwangu Likizo nzima ya Mwezi wa 6 na December no kutoka nnje,ndani sijaekewa godoro zaidi ya Poti (lile la mtoto).

Adhabu gani mimi sijapewa? ila sikia nikwambie the more mnamuadhibu huyo mtto the more mnamuongezea tabia ya wizi,nina uhakika 100% mtoto sampuli hiyo nikikaa nae mwezi 1 tu, Akirudia kuiba hata sh 50 mimi sio CONTROLA.

Una haki ya kumchoka kwasababu si mwanao wa kumzaaa una haki 100%, mimi mama yangu tu alienibeba tumboni miezi 9 na akapata uchungu alidiriki ilaani siku aliyopata mimba siku aliyonileta duniani, (unaweza ukapata picha)

Mtoto wa namna hiyo hakuna anaeweza mvumilia wala kumkubali,naelewa unachokiongelea mkuu nakielewa kwasababu unamuongelea COPY yangu so naelewa hasara nilizokua nazitoa kwa wote waliokua around.

Nime endesha Gari nikiwa darasa la 5,Narudi nyumbani na Gari wazazi wangu hata baiskeli hawana Naingia getini nikabadilisha nguo nikarud kwenye gari huyooo nikasepa zangu, kama ushawahi ona katuni ya ZOOTOPIA yule dogo anaendesha ile gari namna alivyokua, mwanzo kbsa ikianza. Nimetoa wapi GARI hilo tuachane nalo.

Naishi DAR kama unaishi DAR ongea na mzazi wa huyo mtoto mnikabidhi mimi nikae nae Mwezi 1 tu halafu ntawarudshia mtoto wenu (akirudi akiwa hajabadilika Uje unifungulie THREAD hapa JF).

Si rahisi lakini amini nakwambia Huyo mtoto atakuja kuwa Nyota imeremetayo ambayo kila mtu ataitamani Ule mzoga wa simba uliotoa Asali huyo mtoto anaonekana kama mzoga sasa (ni haki yenu kabisa kumuona hivyo) ila siku 1 itatoka asali kupitia mtoto huyo.

Si rahisi kulea aina hiyo ya mtoto kama kuna maisha hujayapitia, yani kila kitu kwako ni kama kipya Aina hiyo ya watoto tupewe vichaa tulio staafu ukichaaa, its not late halafu kabla sijamuona nimejikuta natamani ungekua n ndugu yangu unanisimulia hayo unaniomba ushauri uone ningekwambia ufanye nini.

NOTE:

Hata mumkate miguu yote sasa hivi atembelee magongo akipona atarudia tabia yake ya wizi,Unapo deal na mtoto type hii ni lazima ufahamu kuongea na yule mtu wa ndani sio wa nnje, Huyo mtoto ana Part Mbili ya nnje na ya Ndani, uktaka abadilike Komaeni na huyo mtu wa ndani Asie onekana, si rahisi kunielewa (utaweza sema ushafanya yote hayo) lakini mimi najua jambo 1 TU, Hakuna MTOTO anaezaliwa ni mwizi au ana Tabia mbaya au Mtukutu HAKUNA, kila mnachokiona kwa mtoto ni Matokeo ya malezi ya Wazazi FULL STOP.
Tupe mbinuaana bado tunazaa hatujui tutabeba nini matumboni
 
Wakuu.
Kwenye kikao jana ndugu wote walikuwepo akiwemo kaka yangu (baba wa huyu mtoto)
Niliwaeleza mengi kuhusu ilivyo licha ya wao kunilaumu kama kawaida.
Tulifikia hata kukwaruzana kabisa kwamba wanasema wizi amejifunzia hapa kwangu , kitu ambacho naweza nikakubali au kukataa, sababu ninampa mahitaji yote.

Hivyo muafaka uliopatikana ni kuwa dogo arudi kwa baba yake lakini nitatuma pesa Za shule na mambo mengine kama kawaida.

Amelia Sana na kujutia pia kuomba msamaha lakini nilipofikia inatosha kabisa tena Sana,

Pia wakati wa kikao dogo alidai kuna mwanafunzi mkubwa shuleni kwao huwa anamtuma hela asipoleta anapigwa..!

Tukasema mtaje twende shuleni kwa mwalimu mkuu ili tumuwajibishe, dogo akaruka kiunzi kwamba amedanganya?

Ni hayo tu wakuu ninawashukuru Sana kwa michango yenu iliyotukuka nyote kabisa hakika mmenisaidia Sana...
Pole sana
 
Mkuu swali ni je akiiba pesa anafanya nayo nini?Ukiweza kujua matumizi yake ya pesa unaweza jua uanze kumsaidia vipi.
Alisema huwa anaenda kula chips sijui soda na vitu vingine.
Ilihali nyumbani nilikuwa nampa vyote.
 
Hana shida, ni tatizo la kiroho zaidi. Dozi iliyopo kanisani kwenu bado haimtoshi. Jaribu kumpeleka kwenye makanisa ya Walokole akaombewe. Popote pale. Kwa kuanzia, unaweza ukampeleka kwa Bull dozer Mwamposa au kwa Nabii Suguye
Usipofanya hivyo inabidi ukae standby siku moja kufikishwa Polisi ukiwa una kesi, wewe kama mtuhumiwa! Mpeleke kwa Walokole. Mimi ni mmoja wao, naelewa ninachokueleza hapa
Tayari nilishampeleka kwao
 
Alisema huwa anaenda kula chips sijui soda na vitu vingine.
Ilihali nyumbani nilikuwa nampa vyote.
Good sasa kwa kuanza,mwambie akitaka chipsi akwambie au uwe na tabia ya kutoka nae na kwenda sehemu ya chipsi unamnunulia mnakula mnashiba then akija nyumbani unampa tena chakula.Mfanye awe rafiki yako kwa kuanza ili ufahamu kama ana tatizo la kleptomaniac au ni tattizo la malezi huko kwa ndugu yako kwani kwa assessment yangu mpaka ndugu yako amemleta kwako kuna shida kwenye mji wake. so do what you can.
 
Back
Top Bottom