Ushauri: Msaada kuhusu tabia ya wizi iliyokubuhu kwa kijana wangu

Ushauri: Msaada kuhusu tabia ya wizi iliyokubuhu kwa kijana wangu

New gay nakubaliana nawe, dna ipo kazini maana mtoa lawama kaelezwa ampeleke dogo polisi cha ajabu jibu lake ni hili ( nikimpeleka polisi nitamuharibu zaidi ). Inaonyesha wazi yeye ni muhusika wa ukufunzi wa huwo wizi endelevu.
 
Kumlelea mtoto mzazi mjinga yaani unamwambia mwanae ni mwizi(huyo sio mdokozi tena)alafu anatetea ujinga

Chukua zigo rudisha kwao kama swala ni kusomesha chukua mwingine

Dah,hilo ni jambazi tyari na kuacha hawezi yani
Uamuzi huu inategemea mkuu. Huwenda baba yake ndiye kamsomesha kwa hiyo kaamua alive fadhila

Hilo ni pepo tu limempitia dogo. Vinginevyo hata karogewa kuiba. Aulizie mchungaji wa ukweli ampeleke dogo atapona

Binafsi haya ya mtoa mada yalinitokea lakini kwa mwanangu. Tena wa kwanza na alikuwa na akili ya darasani ya kutisha. Ajabu akawa Mlevi na mwizi wa kutisha. Nilielekezwa kwa mganga wa kienyeji nikampeleka maana sikuwa na namna . Akamtibu alivyoweza na kweli dogo aliacha tabia zote mbovu. Tena akawa anajishangaa kwa tabia aliyokuwa nayo ya WIZI na ulevi.

Waganga wa siku hizi wengi ni matapeli simshauri ampeleke huko. Bali wachungaji watamsaidia.
 
Wakuu,

Naamini kila mtu huwa anakosea, lakini linapokuja swala la kukosea mara kwa mara huwa linatia hasira sana.

Huyu mtoto wangu anasoma darasa la 6 ,ni mtoto wa Kaka yangu alimleta hapa kwangu ili asome,

Sasa kinachozidi kunipa wasiwasi ni tabia yake ya wizi uliokubuhu!

Yaani kwa umri wake na vitu anavyoiba nabaki mdomo wazi kabisa.

Sijawahi hata kumuadhibu lakini jana imenipasa baada ya yeye kuuza simu tatu kwa bodaboda tatu wakuu!

Bora hata angeuza bei kauza elfu 7.

Alishasema mara nyingi harudii lakini ni yale yale nimempiga na leo hawezi kutembea wa kwenda shule amelala tu.

Alishaiba hela sana ndani huwa nina tabia ya kuweka noti ndogo ndogo kwenye dressing table pale, so anapokuja asubuhi kuomba hela ya kula shule namwambia achukue buku yeye anapita nazo zote huwa nanyamaza tu.

Alishaiba baiskeli ya wenzie shule wakamfuata mpaka huku nyumbani kwangu niliskia aibu sana nilipoambiwa hilo.

Aliiba laptop ya mwalimu! Najiuliza aliwezaje nayo pia walimdaka nayo.

Vingine ndani vitu anauza mfano aliingia Store akauza pampu, aliuza charge ya simu, flash disk yangu pia yenye documents muhimu sanaa aliuza!

Sasa chai anakunywa asubuhi, pesa ya kula shule ninampa, lakini bado anaiba nimekosea wapi? Nikimwambia kaka yangu huko kwake ananilaumu na ndugu wengine kuwa nimemuharibu mtoto wake.

Kuna jirani alisema nimpeleke dogo polisi, hili haliingii akilini polisi kufanyeje sasa kwa mtoto mdogo kama huyu? Si nitamuharibu zaidi?

Mbaya zaidi na kanisani huwa anaenda kila Jumapili.

Nahofia kanisani atakuja kuiba sadaka.

Aliwahi pia kuiba pesa za wageni wangu 65k nikamsachi na kumkuta nazo, imagine aibu niliyoipata!

Nilimnunulia mpira na viatu vya kuchezea soka, lakini cha ajabu aliuza huo mpira, viatu mpaka kijazio!

Hii shida ya kulea mabao ya watu ni ushenzi sana!

Nishauri wakubwa.

UPDATE :
Leo kutakuwa na kikao hapa kwangu ndugu wengi wamekuja wengine hawajafika akiwemo baba wa huyu dogo.
Lengo lao likiwa ni kujadili namna ya kumsaidia lakini mimi binafsi nimenyoosha mikono juu niko radhi kuwaambia ukweli kwamba amenishinda hivyo baba yake aondoke naye mpaka mwisho wa kikao tutajua.
Ngoja tumvizie huku mtaani kwetu, ole wake tumkamate....mimavi ya kesho atakunya leo hii. Wewe si amakushinda, basi huku tutamshinda tu na akitoka hai atakuheshimu baba yake mzazi.
 
Huyo mtoto anakipaji kikubwa cha wizi ,mpeleke chuo cha wizi bariadi ....atakuja kuwa na mafanikio zaidi kwenye wizi mkuu ....!
 
Ushauri mzuri Sana na nimeupokea lakini polisi huyu dogo Sana hatoumia Huko kweli
Usimpeleke zungumza nae mara nyingi malezi magumu acha,wakati nasoma msingi mwanafunzi mwenzetu alikuja na pesa nyingi alitununulia mavitu acha kumbe kaiba mshahara mzima nyumbani tulikuja pigwa wote tulinunuliwa vitu mstarini chini ya babaake,alisumbua na huu wizi ila sasa ni mtu mzima ana kazi ila ukimkopesha hakurudishii ngodo
 
Uamuzi huu inategemea mkuu. Huwenda baba yake ndiye kamsomesha kwa hiyo kaamua alive fadhila

Hilo ni pepo tu limempitia dogo. Vinginevyo hata karogewa kuiba. Aulizie mchungaji wa ukweli ampeleke dogo atapona

Binafsi haya ya mtoa mada yalinitokea lakini kwa mwanangu. Tena wa kwanza na alikuwa na akili ya darasani ya kutisha. Ajabu akawa Mlevi na mwizi wa kutisha. Nilielekezwa kwa mganga wa kienyeji nikampeleka maana sikuwa na namna . Akamtibu alivyoweza na kweli dogo aliacha tabia zote mbovu. Tena akawa anajishangaa kwa tabia aliyokuwa nayo ya WIZI na ulevi.

Waganga wa siku hizi wengi ni matapeli simshauri ampeleke huko. Bali wachungaji watamsaidia.
Mkuu tatizo hapa ni mtoto wa mtu ni bora akiwa mwanao huyo utakufa naye,hapa shida iko hivi
Akimuacha anavyozidi kukua ndivyo wazazi wake watajivua na kusema dogo wizi kajifunzia kwa baba yake mdogo kwakua amekulia hukohuko,hapo ajiandae kubeba lawama zote ikiwa ni pamoja na malezi mabaya hata kama wanajua kwao alikuwa mdokozi
Pili ikitokea la kutokea bahati mbaya dogo akajeruhiwa au kuuwawa kwenye harakati zake,anaweza kutengwa mpaka na ukoo mzima,wanadamu waone hivihvi
 
Nimejiskia kusikitika, Nimejiskia kucheka, Nimepata mixture of feelings,Mtoa mada nakufananisha na Mama Yangu mzazi alienitoa tumboni mwake,Huyo mtoto najifananisha na mimi,halafu sasa huyo mtoto mimi ni clone wangu

mimi ndie ORIGINALY yani huyo ni COPY enzi za utoto wangu mimi ndie nilikua OG Kuna kitu hujakijua kuhusu huyo mtoto,fimbo haitomsaidia wala kumbadilisha,mimi mwenzako nilishaloekwa hadi kwenye Beseni na Biblia,nishafungiwa Room kwangu Likizo nzima ya Mwezi wa 6 na December no kutoka nnje,ndani sijaekewa godoro zaidi ya Poti (lile la mtoto).

Adhabu gani mimi sijapewa? ila sikia nikwambie the more mnamuadhibu huyo mtto the more mnamuongezea tabia ya wizi,nina uhakika 100% mtoto sampuli hiyo nikikaa nae mwezi 1 tu, Akirudia kuiba hata sh 50 mimi sio CONTROLA.

Una haki ya kumchoka kwasababu si mwanao wa kumzaaa una haki 100%, mimi mama yangu tu alienibeba tumboni miezi 9 na akapata uchungu alidiriki ilaani siku aliyopata mimba siku aliyonileta duniani, (unaweza ukapata picha)

Mtoto wa namna hiyo hakuna anaeweza mvumilia wala kumkubali,naelewa unachokiongelea mkuu nakielewa kwasababu unamuongelea COPY yangu so naelewa hasara nilizokua nazitoa kwa wote waliokua around.

Nime endesha Gari nikiwa darasa la 5,Narudi nyumbani na Gari wazazi wangu hata baiskeli hawana Naingia getini nikabadilisha nguo nikarud kwenye gari huyooo nikasepa zangu, kama ushawahi ona katuni ya ZOOTOPIA yule dogo anaendesha ile gari namna alivyokua, mwanzo kbsa ikianza. Nimetoa wapi GARI hilo tuachane nalo.

Naishi DAR kama unaishi DAR ongea na mzazi wa huyo mtoto mnikabidhi mimi nikae nae Mwezi 1 tu halafu ntawarudshia mtoto wenu (akirudi akiwa hajabadilika Uje unifungulie THREAD hapa JF).

Si rahisi lakini amini nakwambia Huyo mtoto atakuja kuwa Nyota imeremetayo ambayo kila mtu ataitamani Ule mzoga wa simba uliotoa Asali huyo mtoto anaonekana kama mzoga sasa (ni haki yenu kabisa kumuona hivyo) ila siku 1 itatoka asali kupitia mtoto huyo.

Si rahisi kulea aina hiyo ya mtoto kama kuna maisha hujayapitia, yani kila kitu kwako ni kama kipya Aina hiyo ya watoto tupewe vichaa tulio staafu ukichaaa, its not late halafu kabla sijamuona nimejikuta natamani ungekua n ndugu yangu unanisimulia hayo unaniomba ushauri uone ningekwambia ufanye nini.

NOTE:

Hata mumkate miguu yote sasa hivi atembelee magongo akipona atarudia tabia yake ya wizi,Unapo deal na mtoto type hii ni lazima ufahamu kuongea na yule mtu wa ndani sio wa nnje, Huyo mtoto ana Part Mbili ya nnje na ya Ndani, uktaka abadilike Komaeni na huyo mtu wa ndani Asie onekana, si rahisi kunielewa (utaweza sema ushafanya yote hayo) lakini mimi najua jambo 1 TU, Hakuna MTOTO anaezaliwa ni mwizi au ana Tabia mbaya au Mtukutu HAKUNA, kila mnachokiona kwa mtoto ni Matokeo ya malezi ya Wazazi FULL STOP.
 
Wakuu.
Kwenye kikao jana ndugu wote walikuwepo akiwemo kaka yangu (baba wa huyu mtoto)
Niliwaeleza mengi kuhusu ilivyo licha ya wao kunilaumu kama kawaida.
Tulifikia hata kukwaruzana kabisa kwamba wanasema wizi amejifunzia hapa kwangu , kitu ambacho naweza nikakubali au kukataa, sababu ninampa mahitaji yote.

Hivyo muafaka uliopatikana ni kuwa dogo arudi kwa baba yake lakini nitatuma pesa Za shule na mambo mengine kama kawaida.

Amelia Sana na kujutia pia kuomba msamaha lakini nilipofikia inatosha kabisa tena Sana,

Pia wakati wa kikao dogo alidai kuna mwanafunzi mkubwa shuleni kwao huwa anamtuma hela asipoleta anapigwa..!

Tukasema mtaje twende shuleni kwa mwalimu mkuu ili tumuwajibishe, dogo akaruka kiunzi kwamba amedanganya?

Ni hayo tu wakuu ninawashukuru Sana kwa michango yenu iliyotukuka nyote kabisa hakika mmenisaidia Sana...
 
Ahsante kwa mrejesho ndugu mjumbe.
Maamuzi sahihi na yenye afya kwa ustawi wa jamii inayokuzunguka.
 
Ahsante kwa mrejesho ndugu mjumbe.
Maamuzi sahihi na yenye afya kwa ustawi wa jamii inayokuzunguka.
Nashukuru sana mkuu anyway twende ukanisimulie uzalo sasa sijacheki Week yote hii 😁
 
Wakuu,

Naamini kila mtu huwa anakosea, lakini linapokuja swala la kukosea mara kwa mara huwa linatia hasira sana.

Huyu mtoto wangu anasoma darasa la 6 ,ni mtoto wa Kaka yangu alimleta hapa kwangu ili asome,

Sasa kinachozidi kunipa wasiwasi ni tabia yake ya wizi uliokubuhu!

Yaani kwa umri wake na vitu anavyoiba nabaki mdomo wazi kabisa.

Sijawahi hata kumuadhibu lakini jana imenipasa baada ya yeye kuuza simu tatu kwa bodaboda tatu wakuu!

Bora hata angeuza bei kauza elfu 7.

Alishasema mara nyingi harudii lakini ni yale yale nimempiga na leo hawezi kutembea wa kwenda shule amelala tu.

Alishaiba hela sana ndani huwa nina tabia ya kuweka noti ndogo ndogo kwenye dressing table pale, so anapokuja asubuhi kuomba hela ya kula shule namwambia achukue buku yeye anapita nazo zote huwa nanyamaza tu.

Alishaiba baiskeli ya wenzie shule wakamfuata mpaka huku nyumbani kwangu niliskia aibu sana nilipoambiwa hilo.

Aliiba laptop ya mwalimu! Najiuliza aliwezaje nayo pia walimdaka nayo.

Vingine ndani vitu anauza mfano aliingia Store akauza pampu, aliuza charge ya simu, flash disk yangu pia yenye documents muhimu sanaa aliuza!

Sasa chai anakunywa asubuhi, pesa ya kula shule ninampa, lakini bado anaiba nimekosea wapi? Nikimwambia kaka yangu huko kwake ananilaumu na ndugu wengine kuwa nimemuharibu mtoto wake.

Kuna jirani alisema nimpeleke dogo polisi, hili haliingii akilini polisi kufanyeje sasa kwa mtoto mdogo kama huyu? Si nitamuharibu zaidi?

Mbaya zaidi na kanisani huwa anaenda kila Jumapili.

Nahofia kanisani atakuja kuiba sadaka.

Aliwahi pia kuiba pesa za wageni wangu 65k nikamsachi na kumkuta nazo, imagine aibu niliyoipata!

Nilimnunulia mpira na viatu vya kuchezea soka, lakini cha ajabu aliuza huo mpira, viatu mpaka kijazio!

Hii shida ya kulea mabao ya watu ni ushenzi sana!

Nishauri wakubwa.

UPDATE :
Leo kutakuwa na kikao hapa kwangu ndugu wengi wamekuja wengine hawajafika akiwemo baba wa huyu dogo.
Lengo lao likiwa ni kujadili namna ya kumsaidia lakini mimi binafsi nimenyoosha mikono juu niko radhi kuwaambia ukweli kwamba amenishinda hivyo baba yake aondoke naye mpaka mwisho wa kikao tutajua.
Dah pole sana,
Tabia ya wizi ni kama addiction

Mtu mwenye tabia hiyo huweza kuiba hata pale anapokuwa hana sababu ya kufanya hivyo

Yani akiona kitu kuzuri ambacho si chake, anasisimka

Mwili unamsisimka kuwa aibe, achukue kiwe chake

Ni kama madawa ya kulevya

Dawa yake,
. Dawa namba moja:

Ni kufumwa akiiba ama kugundulika kuwa kaiba,
Msisimko anaojisikia akiona kitu kizuri ni mkubwa mno mwenyewe hawezi kujizuia, inahitaji mtu mwengine (hasa mtu mzima) amfume au agundue kosa lake kisha amkanye na amuonye, maana yeye mwenyewe hamu ya kuiba imemzidia hawezi kujicontrol

Yani akifumwa anaiba reaction anayopewa ndio mwanzo wa tiba, hapo lazima aoneshwe kwa maneno na vitendo kuwa afanyacho sio sahihi. Ikiwemo kumtandika

Hapo ndio atajifunza hamu yake ya kuiba sio kitu sahihi

Na mlazimishe Kuomba msamaha na kuahidi kutokufanya tena, na aahidi akiiba tena umpe adhabu gani

Unasema yuko darasa la sita, ni kwamba huyo bado mdogo anafundishika, anachohitaji ni mtu mzima wa kufuatilia nyendo zake

Hakikisha, hana kitu chochote usichofahamu kakipataje

Kila alichonacho Hakikisha unamfahamu kakipataje, tena ajue kuwa una fuatilia kila anachomiliki,

Kama ana marafiki wenye tabia zinafanana muonye akae nao mbali

Kama ana rafiki wana vitu ambavyo hawezi yeye kuwa navyo, mueleze kuwa hawezi kuwa na vitu kama hivyo kama wezake

Chunguza kama anakosa mahitaji ya msingi, maana isije ikawa kukosa vitu vya msingi nyumbani kuna mfundisha wizi

Itachukua muda ila ndio maana ya kulea hiyo

Kashakumbwa na hisia za wizi (maana wizi ni hisia na msisimko), ila bado mdogo ananyoosheka
 
Anahitaji tiba za kiroho Ili ile roho ya wizi imtoke. Yaani ashachukuliwa nafsi yake na shetani so anaitumia. Inatakiwa apate ukombozi wa kurejesha nafsi yake.
 
muwekee sumu kwenye chakula
We jamaa umepinda kabisa
JamiiForums1852391034.jpg
 
Tiba ni nyingi tu bro km kwenu mnafuga mbwa mpikie vhakula kwenye sufuria hilo ale bila kujali hataiba tena wala usilioshe pika hivyo hivyo
 
Tatizo kaka zangu hawawezi na hawataki kusikia ili wanaamini nina uwezo wa kumtunza huyu dogo,
sijui nifanyeje?
Kuwa na uwezo haimaanishi ni jukumu lako ni bora umrudishe kwa baba yake usiangalie watafikiria nini, huyo dogo anahitaji msaada wa wataalamu wa afya ya akili.
 
Kumlelea mtoto mzazi mjinga yaani unamwambia mwanae ni mwizi(huyo sio mdokozi tena)alafu anatetea ujinga

Chukua zigo rudisha kwao kama swala ni kusomesha chukua mwingine

Dah,hilo ni jambazi tyari na kuacha hawezi yani
Usitamkie vijana wadogo maneno makali kiasi hicho

Huko ni kumkatia tamaa na sio sahihi

Huyo bado mdogo anafundishika.
Maneno makali yasije kumletea laana akajikuta ana haribika zaidi.

Maneno yanaumba hivyo sio vizuri kuropokea watu mambo hasi na kuharibu mustakabali wao.
 
rudisha kwa baba ake ....
Kauli za walezi wa kizazi hiki!!!!

Kulea ni majukumu makubwa

Msione mnaenda katika maharusi ama tukio fulani mtu anasimama anasema "namshukuru fulani, bila yeye nisingekuwa hapa", yani mkiona hivyo mjue mtu alibeba majukumu, pengine hata hayakuwa yake, ikiwemo kama haya ya kunyoosha kijana tabia
 
Back
Top Bottom