Kwanza unatakiwa ufahamu hiyo LAKI ni mtaji wako ambao hutakiwi upotee kwa namna yeyote ile,kama ni kamba basi wewe umebakisha uzi tu kamba ikatike kwahiyo kuwa makini uzi ni mwembamba muda wowote unaweza kukatika ukatua chini,na ukitua chini omba utue na miguuu unaweza ukatua chini na mgongo au ukabamiza hiyo kichwa kabisa,ok nakuja kama ifuatavyo hapa chini chambua inayokufaa then tembea nayo kwenye utendaji kazi.
1.Uza CD
tengeneza meza yako ya 20,000 ya kuinua kisha 80,000 iliyobaki nenda k.koo kanunue CD za wanyama,katuni,movie za action,kihindi,nk nunua cd zako za 50,000 cd kule zipo kwa bei tofauti,kuna cd zina cover kubwa refu hizo zinauzwa 1000,halafu kuna cd za macover madogo hizo zinauzwa 600-700,kanunue hizo cd za 600 changanya za kila aina,kisha nenda panga kwenye ile meza yako,katege meza yako mahali ambapo watu wanapita pita. cd za 50k ukinunua kwa bei ya 600 utapata cd kama 80 ni cd nyingi sana maana utakua umepoint cd nzuri,wewe utaenda kuuza 2000 kwa CD 1,mteja akikuomba ana 1500 Usikatae chukua,mteja mwngine akija akakulilia ana 2000 ila anataka cd mbili Usimkatalie chukua hela,usiache hata senti ikatize mbele yako.
2.GLASS PROTECTOR + USB + VICHWA VYA CHAJI
ingia pale k.koo glass zinauzwa bei ya jumla 600 kwakua wewe sio mzoefu wa simu gani zinatoka sana jaribu kuwauliza wale wale wauzaji wakusaidie kukupa protector za simu zinazotoka,na siku hizi protector nyingi sana zinaingiliana,proteector 1 inauwezo wa kubandika simu zaidi ya 10 na zote zikafit,mfano protector ya Tecno w3 hi protector inakaa kwenye tecno wx3,wx4,wx4lite,na simu nyingi sana za Itel zina kaa hii protector kwahyo kachukue protector mchanganyiko za 40,000 utapata protector zaidi ya 60,ni nyingi sana sana huwezi maliza siku hujapata mteja wa protector HAIWEZEKANI (nimekuandkia haiwezekani kwa herufi kubwa).
Usb nenda kanunue zile zinauzwa 10,000 zinakaa usb 20 ndani yake,hizi usb 20 wewe Utaziuza 3000 kwa 1 ila wateja wengi watakwambia wana 2000 hivyo usikatae hela,mteja akikwambia nina 1000 Chukua yani haina kuacha hela ilimradi faida inapatkana usjali n kubwa wala ndogo,hesabu utapga jioni.
Vichwa vya chaji vinauzwa 1000 vipo vya 700 pia kwahyo wewe changanya vichwa nunua vya samsung,tecno,infinix,mteja akitaka charge muuzie,Hii biashara yako itakua n ya umachinga,usikae sehemu 1 tembea tembe tembea (nimerudia neno tembea mara 3) zunguka kona zote Najua utachoka ila ikifika jioni utapata tabasamu mwororo sana usoni mwako.
3.MAJI YA KANDORO
Hapa namaanisha maji ya kandoro ya pakti,usitumie chupa zilizotumika (watu hawazipendi siku hizi) jaza weka kwenye friji tembeza maji uza sh 100,hapa unaweza ukaajiri kbsa na kijana/vijana kwa mtaji huo huo wa laki mkawa watatu au hata wanne kila mtu akachukua mzigo wake akapita kona yake,mkimaliza mnafata tena maji,hvyo hvyo..kazi inaenda.
4.Choma mahindi
maelezo ya hii biashara yapo humu humu
5.Uza mishkaki/ndizi mzuzu za kukaanga,
maelezo ya hizo biashara yapo humu humu
Biashara za mtaji huo ni nyingi sana mkuu ila ninachotaka kukwambia biashara zote ni zakutoa jasha/kuhangaika/hamna biashara ya luxury kwa mtaji huo kwahyo kama umedhamiria basi kubali kujitoa sadaka kweli kweli,aibuu weka pembeni pambana hasaaa.
ONYO : nimekushauri biashara nikazipa namba hapo juuu,nakushauri kaza kwenye 1,2 na 3 hizo kuanzia 4 inakubdi uwe extra carefull maana biashara za chakula bwana sio za kubetia hasa kwa wenye mitaji midogo kama wako.
fungua hizo biashara ukiwa unajua unataka kufanya nn,kama hujawahi fanya biashara ndogo sikushauri kbsa ufanye biashara ya chakula,sjui matunda,sjui mihogo sjui nn,utajuta ushke kichwa.