Ushauri: Mtoto kameza shilingi mia mbili

Ushauri: Mtoto kameza shilingi mia mbili

Hata sisi mtoto wa Jirani yetu kameza shilingi mia wiki sasa imeisha mwanzoni tulimpeleka hospitari maana ilikuwa imegoma kwenye koo anashindwa kumeza chakula madakitari walipojitahidi kutaka kuiitoa ndio kwanza ikawa inashuka mpaka tumboni wakamua kuacha na kushauri apewe vyakula laini ili ikwezekana aitoe hiyo shilingi kwa njia ya haja kubwa mpaka sasa tunasubiria.
 
Kuna zile wanaita goroli na hizo koeni sio nzuri kuwapa watoto wachezee mtakuja kusababisha roho za watoto wenu ziache mwili kisa ujinga wenu.

-Ndumilakuwili-
 
Sasa mnaisubiria mkiwa nyumbani au hospitali?

-Ndumilakuwili-
 
Kuna zile wanaita goroli na hizo koeni sio nzuri kuwapa watoto wachezee mtakuja kusababisha roho za watoto wenu ziache mwili kisa ujinga wenu.

-Ndumilakuwili-
Goroli ni mbaya sana maana zinaweza kuelekea kwenye njia ya hewa.
 
Mtoto kameza Sh mia mbili,je inaeza kutoka au,msaada jamani nifanyejee

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
Ni vema kujua pia umri, poleni. Je hali yake kwa ujumla imebadilika? Anacheza na wenzake? anaonekana kuwa na shida ya kupumua na kutokwa na mate mengi mdomoni? Unaishi umbali gani na hospitali yenye huduma za Xray?
In general kama ana shida ya kupumua ina maana njia ya hewa inahusika kwa namna moja au nyingine, na hivyo hiyo ni dharura awahishwe mara moja hospitalini. Nje ya hapo jiandaeni kumpeleka hospital kwa ajili ya kufuatilia ushukaji wa hiyo coin kwenye mfumo wa chakula kwa Xray.
 
Kama hana maumivu yoyote usiwe na wasiwasi itatoka yenyewe,ili kujihakikishia kuwa imetoka atumie choo cha kukaa au uwe unafuatilia kinyesi chake anapojisaidia kwa muda wa siku tatu itakuwa imetoka.
 
Matatizo ya ki emergency kama hayo si ya kuyaleta kwenye social media ina maana unakaa sehemu ambazo hakuna watu au?
Coz inaonekana tangu imezwe hiyo shilingi ndo unawasubiria wadau wa jf wakwambie cha kufanya wewe na majirani zako hapo hamjui lolote!!!
 
Back
Top Bottom