Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Ni wazi mashabiki wengi wa Yanga wanaamini kazi imeisha, kilichobaki ni kumaliza kazi Dar.
Mimi niko kinyume, kazi ndio imeanza, mpaka sasa hatuna deni na wachezaji wetu na benchi la ufundi kwa sababu wameshavuka malengo yaliyowekwa kuingia kwenye makundi, wanachotupa kwa sasa ni bonus tu.
Sasa kwakuwa wachezaji wametimiza majukumu yao kwa zaidi ya asilimia 100, huu ni wakati sasa wa mashabiki kuwapa nguvu wachezaji.
Tujaze uwanja full house kwa Mkapa mechi ya marudiano na Rivers, tuwaheshimu na tuingie kama sisi ndio tulipoteza mchezo Nigeria.
Ni wazi wengi mnakumbuka Simba ilishinda ugenini bao 2 kwa bila dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Namibia lakini walipokuja uwanja wa Mkapa Simba ikatolewa on aggregate.
Haya makosa yasijirudie kwa Yanga, wananchi wana kiu ya mafanikio, lakini pamoja na Kiu hiyo naomba tujifunze kwa Morocco, mechi yao na Simba tiketi zote zimeisha ni full house.
Tunahitaji full house mechi ya marudiano na Rivers, hamasa ianze sasa, full house tayari ni goli kabla ya mechi.
Nimemaliza.