Ushauri: Mwanamke amenipigania sana nilipoumwa lakini dini imekuwa kikwazo kwetu kuoana, ndugu zangu wanataka pia nimfukuze sehemu ya kazi! Nifanyeje?

dini ipi, kuwa wazi.
 
Ni vizuri kutoa credit kwa Mungu aliyekukutanisha na mwanamke sahihi .

Mungu wetu hapatikani katika dini ,bali matendo mema yenye utu na ubinadamu.
 
You are In-charge of your destiny..., nyingine huwa ni excuses tu za justification ya unachofanya / ulichofaya...; Makes one Sleep better at Night...

My Motto; Huwa nafanya nachotaka kufanya binafsi.., hence nikilikoroga no one to blame but myself..... Ukiwa na misimamo hio hata ndugu watakuelewa from the get go kwamba jamaa huwa yupo jinsi alivyo...
 
Hujataja wewe ni wa dini gani ila ukiwa na ndugu wa kichawi kama wa kwako ni tabu sana
 
Una umri gan mpaka sasa familia ukuamulie maamuzi ya maisha yako...
Dini hakuna wa kukupangia
Wa kumwoa hakuna wa kukupangia labda uwe goigoi..
 
Inaonyesha wewe ni Last Born, unakosaje maamuzi kwa suala dogo kama hilo?
Nisikilize sasa; katika maisha yako kaa ukijua kuwa suala lolote linalohusisha hisia (Kupenda/kutopenda) halimuhusu mtu mwengine yeyote ispokuwa wewe mwenyewe, maana hata ikifikia nyakati za maumivu hayatompata yeyote ispokuwa wewe mwenyewe.
Kaa ukijua kuwa wewe ndiye derev wa maisha yako na hisia zako, na sio mzazi wala ndugu yeyote. Zaidi utasikiliza ushauri wao na utautafakari mazur utayachukua na yasiyofaa utayaacha. Huezi kumuacha mtu unayempenda naye akupenda kisa eti ni ndugu, kwani wao ktk familia zao walizojenga (walioolewa/waliooa) wewe walishawahi kukushirikisha kuwachagulia? Iweje wao wakuchagulie?, Sikia ushasikiaga ile kauli ya ADUI YAKO HATOKI MBALI?, MCHAWI HATOKI MBALI?, ushaitafakari hiyo MBALI? nadhan ushanielewa had hapo.
Unaacha mwanamke aliyekuwa bega kwa bega naww kipind ambacho huenda wengine hao walikaa kando wakisikilizia halafu baada ya kupona unaacha kusikiliza hisia zako unasikiliza hisia za wengine?, UNAZINGUA. Rudisha akili yako na ikikuoendeza hyo Mwanamke OA, masuala ya dini itabaki kuwa maridhiano yenu ninyi wawili tu, nimeandika hili nikiwa na hasira sana MWANAUME UNATAKIWA UWE NA MISIMAMO, unakosa kujisimamia utaweza kusimamia Familia yako kweli Jamaa? SHENZ
 
Kosa langu nn
Kosa lako liko hapa; Kwanza sijui umri wako, pili wewe ni dini ipi?

Kosa ni kuamriwa na ndugu zako badala ya kukupa ushauri lakini pia kama mwanamke ni mkiristu ana haki kutokana na imani yake na kama ni muislamu same like ila nendeni bomani kaunganeni maisha yaende.
 
Alikupambania kwa sababu ananufaika na wewe. Kama ana tabia nzuri na hofu ya Mungu mtafute muangalie mna-solve vipi hicho kipengere cha dini lakini usidanganyike na wema aliokufanyia. Wanawake ni opportunistics, hakuna mwanamke mwema kwa mwanaume ambae hana masilahi nae.
 
Brother hao ndugu zako we unawasingizia tu,sema unatafuta ushauri ili uhalalishe uharamia unaotaka kumfanyia huyo manzi
 
Hukupaswa kumuacha kabisa, kama kweli unampenda muoe huyo Binti maisha ni yako wewe kama wewe.
 
Hizi bahati mbona sisi hatupati.. 😭
 
wewe ni she au he? usikute tunapoteza muda wetu kwa mwanaume ke.
 
Shauri yako,mwanaume unakosa uamuzi kwenye masuala madogo kama hayo.Umemuacha haijatosha bado unaendelea kumuadhibu,litakukuta jambo
 
Ingekuwa ni mtu wangu wa karibu halafu ananieleza huu upumbavu ningempiga vibao, na nisingemsemesha chochote.
Umeniudhi sana.

Dini ni kitu gani? Eti unasema kwa maamuzi ya busara mkatengana? Huyo dada Mungu amsaidie apate mwanaume bora wa kuwa mumewe wewe huna msimamo utamsumbua sana.
 
Mzee mjinga, kwani unaoa Dini au mtu? Hizi stories zilizoletwa Kwa jahazi na mitubwi zisikufanye utengane na Manzi yako.
 
Kwenye biblia kuna kitabu kinaitwa Ruth kitafte ukisome. In short kinaeleza story ya binti aliebadili dini Kwa ajili ya upendo. Kama huyo mpenzi wako yuko tayari kuifata imani yako zungumza Kwa hekima na ndugu zako muyaweke sawa umuoe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…