Kuna mwanamke nilikuwa naye kwenye mahusiano, ni mtu ambae alinipenda na mimi nilimpenda sana, kuna kipindi niliumwa sana kama miezi mitatu, alipambania uhai wangu hadi dakika ya mwisho maana ilikuwa nusu nife!
Ila Dini zikaja kututenganisha, hatuwezi kuoana, familia yangu ikaleta vita kali niachane naye sababu muda unaenda, kwa maamuzi ya busara tukatengana ila yeye hakutaka na hilo suala, lilimuumiza ila hakuwa na namna.
Japokuwa kwenye suala la maisha mimi ndio nilikuwa nampambania, maana kwenye moja ya ofisi zangu anafanya kazi na ndugu zangu wanataka nimfukuze ili nikate ile line ya uhusiano.
Sasa nimejiuliza sana ile ni Rizki na ni mtu aliyepigania misha yangu sana, nawezaje kumfukuza pale? Je, ni sawa.