Ushauri: mwanangu ananyang'anywa shamba alilopewa na babu yake

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,583
Reaction score
4,009
Baba mkwe wangu alifariki mwaka 1993 mwanangu akiwa na miaka 9. Alimpa mwanangu shamba kwa sababu alikuwa ni wajina wake. Eneo hilo halikuguswa na yoyote kwa sababu siku zote linajulikana ni la mwanangu.. Pia alimpa mjukuu mwingine mtoto wa mke mwenzangu eneo ambalo pia halikuguswa. Mwaka juzi Bibi yake mwanangu alimwomba alime sehem kidogo ya shamba nae akakubali ili eneo lisikae tu. Sasa mama mkwe wangu amefariki wifi zangu na shemeji yangu wanataka lile eneo ligawanywe kwa wajukuu wengine ambao hata walikuwa hawajazaliwa wenye jina la baba mkwe wangu. Ukoo uliingilia wifi zangu na shemeji yangu wakasema wana karatas ambazo walisaini wao na bibi yangu hayo mabadiliko yafanyike, lakini wameambiwa walete na hawajaleta. Sasa shemeji anamzuia mwanangu kuendeleza eneo lake na karatas ameshimdwa kuzileta..je afanyeje?
 
Kila nikiwaza kujenga kwa babu akili inaniambia ACHA mwaka wa 7 sasa sijafikia muafaka wa akili yangu
 
Baba mkwe wangu alifariki mwaka 1993 mwanangu akiwa na miaka 9. Alimpa mwanangu shamba kwa sababu alikuwa ni wajina wake. Eneo hilo halikuguswa na yoyote kwa sababu siku zote linajulikana ni la mwanangu.. Pia alimpa mjukuu mwingine mtoto wa mke mwenzangu eneo ambalo pia halikuguswa. Mwaka juzi Bibi yake mwanangu alimwomba alime sehem kidogo ya shamba nae akakubali ili eneo lisikae tu. Sasa mama mkwe wangu amefariki wifi zangu na shemeji yangu wanataka lile eneo ligawanywe kwa wajukuu wengine ambao hata walikuwa hawajazaliwa wenye jina la baba mkwe wangu. Ukoo uliingilia wifi zangu na shemeji yangu wakasema wana karatas ambazo walisaini wao na bibi yangu hayo mabadiliko yafanyike, lakini wameambiwa walete na hawajaleta. Sasa shemeji anamzuia mwanangu kuendeleza eneo lake na karatas ameshimdwa kuzileta..je afanyeje?
Kama alipewa na babu yake ni lake. Full stop
 
Yeye alivyopewa na babu yake kuna makaratasi yoyote?
 
kama kuna majirani watu wazima watakaoweza kusimama na nyie kama mashahidi nena ofisi ya kata utapata msaada, ila hata akirudishiwa asijenge hapo hata kaa kwa amani
 
Itisha kikao cha familia.. waaambie shamba ukipewa hakuna anaeingilia..ni lake mjukuuu. Hao tamaa
 
Back
Top Bottom