USHAURI: Nahisi nimerogwa

USHAURI: Nahisi nimerogwa

Shikamoni wakubwa zangu

Mimi ni kijana wa miaka 22, nimekuja mbele yenu kuomba USHAURI kwa haya yanayo ni kumba Katka maisha yangu hasa ya kielimu maana Nahisi Nimerogwa[emoji58] kuna matukio kadhaa yamejitokeza katika harakat zangu za kielimu mpaka Nahisi Nimerogwa. Kuna matukio matatu ambayo mpaka Sasa sielew nimeikuta nimekata tamaa

Tukio la Kwanza nikiwa primary miaka kadhaa iliyopita, shule nilikuwa nasoma ya private iliungua ktk uchunguzi wa walimu katika Tukio Hilo Walifanikiwa kumtambua mtuhumiwa mmoja ambae Katika mahojiano zaidi alinitaja mimi kama mhusika wa tukio hilo ili hali kwamba mimi sikuhusika kwa namna yoyote ile[emoji17] nilijaribu kujitetea lkn wapi, mwisho wa siku nilitimuliwa shule ile

Tukio la pili nikiwa advance shule fulani Kanda ya ziwa, kuna Tukio la kihalifu lilifanywa na baadhi ya wanafunzi hapo shuleni, ambapo wanafunzi walivunja kufuli za locker za wanafunzi wenzao kipindi wanafunzi wengine tukiwa prepo. Lkni baada ya uchunguzi walifanikiwa kutaja wahusika chakushangaza mimi pia nilitajwa na walimu kama mhusika, Aisee nilishangaa sana maana sikuhusika kwa namna yoyote na tukio Hilo. Utetezi wangu haukusaidia mimi kupewa suspension kuanzia mwezi wa 11 mpaka necta hii ilipelekea kufeli mitihani ya kidato cha sita.

Tukio la tatu, ni KIPINDI hichi nikiwa mwanachuo katika chuo cha diploma kada ya afya kozi medical laboratory. Kuna uhalifu umefanyika kwenye hostel za wanafunzi kuibiwa simu na pc. Ijapokuwa mimi nakaa nje ya chuo, lkn kuna mhalifu alikamatwa ambae si mwanachuo ni raia wa mtaani tu hivyo alivyokamatwa ktk mahojiano na Polisi alinitaja mm kwa majina kwamba ndie nimekuwa namsaidia kufanikisha uhalifu huo chuoni. Ilipelekea mm kukamatwa na kuwekwa lockup ilhali mimi sihusiki kabisa na nilitajihidi kujitetea hakuna anayenielewa. Sasa kesi yangu ipo kwenye bodi ya chuo nasubiri maamuzi tu. Na sjui kama nitafanya mitihani ya end of semister2

Nimekuja mbele yenu kuomba USHAURI juu ya haya matukio yanayonikumba maana nahisi kurogwa najiona sina thamani ya kuendelea kuwepo duniani.

Karibuni wakubwa zangu mnishauri nifanyaje mbona mimi tu!!
Embu sahizi sikiliza RADIO Upendo upate maombi 107:7
 
Acha kujiunga na makundi usiyoendana nayo ! Ni ngumu sana mtu kutaja jina lako wakati hakufahamu ! Ni watu unaozunguka wanaona wewe ndo wa kuangushiwa jumba bovu !!
Na server za jamii forum zikipotea tunakutaja chimbo boy we subiri 😀😀😀
khaaa🤣🤣🤣🤭🤭🤭

hebu kalale au kalalwe mkuu
 
Kwanza wewe ni mtu wa aina gani???

Pengine namna ulivyojiweka nirahisi kuhusishwa na matukio ya ajabu na Watu wakaamini.

Kabla hujatafuta mchawi anza nawewe mwenyewe jitathmini matendo na mienendo yako inashabihiana na matukio unayosingiziwa????

Kuna wakati matendo yako ndio mchawi wako.
 
aisee, israeli yupo mwaisela....kaa kitaalamu...wanajuaje jina lako kamili mkuu ?
 
Kiujumla tukuo la Kwanza alie nitaja namfahamu, lapili niliitwa tu na walimu.. Lkn hili la tatu nimestaajabu sana mtuhumumiwa ananitaja tena mbele yangu anakiri waz ku husika na Tukio na mm eti ndio mshirika wake.. Sura yake ni mara ya kwanza naiona
Niliwai kuwa katika viatu vyako mara 1.
Jamaa simjui, ndiyo mara ya kwanza ninakutanishwa nae mbele ya umati mkuu wa watu Alichokuwa akikisema jamaa ni the same na kesi yako.
Suluba zote, kipigo chote jibu langu ni SIJUI CHOCHOTE wakati huo nina miaka 17 tu na homu hawajui niko wapi.
Jamaa aliyeniingiza katika msala alikuwa ananizidi umri lakini alikuwa analia kama mtoto.
Niliteseka siku hiyo!! ni moja ya siku zangu mbaya, mauti niliyaona, walipiga wakachoka na jibu langu ni lile lile!!! baada ya wiki 1 hivi Bro mmoja simjui pia nikabumiana nae tu mtaani, akanivuta pembeni akaniambia:, BWANA MDOGO SIKU ILE NILIKUKUBALI , WEWE NI MTU SAHIHI WA KUFANYA NAE KAZI , MAADAM BADO UKO HAPA HAPA NITAKUTAFUTA BAADA YA SIKU MBILI. Ananiambia hivyo mimi nina tiket tayari ya kurudi skonga.
 
Kuna jamaa alikuwa anasimulia kwny kipind cha sitasahau RFA........aliwahi sema kuwa alikubwa na hicho Kitu ...

Inakuwaje
Nikwamba akiwa kazin copy yake inatoka then inarudi home na kuanza kuleta vurugu kitaa......mfano kusumbua watoto wa watu n.k
But mshkaji akirudi home anashangaa kesi ni nyingi mtaani

Dunia Ni Zaid ya tuijuavyo[emoji23][emoji23]
Mkuu hichi ndo kilichokua akilini mwangu nakiwaza baada ya kuusoma huu uzi. Jamaa wa RFA alikua anakiita kivuli. Kilikua kinamuharibia kila aendapo.

Mleta uzi bila shaka nawe una kivuli chako ambacho ndo kinatenda hayo yote.

Ushauri: Tafuta mtu wa dini haswa akuombee. Ikishindikana tafuta mganga haswa akufanyie tiba.
 
Acha kuvuta bangi na huo usela mavi, mtu unajiita chimbo boy maana yake nini?

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Sivuti bangi.. Jina chimbo boy, kipind nasoma Nlikua na utaratibu wa kujichimbia kusoma peke yangu(bila discussions na wenzangu) ndio mwanzo wa Hilo jina chimbo boy
 
Nenda Kwa mganga isije ikawa una copy yako inafanya kazi, au huwa unatoka nje ya mwili bila kujijua
Kwa mganga Tena? Shetani kwa shetani wanashtakiana? Nakushauri uokoke then roho mtakatifu atakusaidia kushinda yote hayo in Jesus Christ name!
 
Achana na marafiki wahuni, Vibaka wanajuaje official names zako? Chimbo siyo kuzuri!
 
Nenfa kanisani onana na mchungaji mwelezee hiyo shida inakuandama na pia funga na kusali kwa MOYO WAKO WOTE Mungu atakuweka huru
 
Sivuti bangi.. Jina chimbo boy, kipind nasoma Nlikua na utaratibu wa kujichimbia kusoma peke yangu(bila discussions na wenzangu) ndio mwanzo wa Hilo jina chimbo boy
wengine achana nao usiwajibu watakusumbua kichwa, anza kuzingatia ushauri wa kidini ulioshauriwa na watu ktk comments...
Ila kamwe usijichanganye ukaenda kwa mganga, ni sawa na mbuzi kufia kwa muuza supu...
 
Kama kwenye ukoo wenu kuna asili ya mizimu ongea na wazazi wako mkafanye jambo,mi mwenyewe nimekumbana nayo sana
 
Kama kwenye ukoo wenu kuna asili ya mizimu ongea na wazazi wako mkafanye jambo,mi mwenyewe nimekumbana nayo sana
 
Unaroho ya kukataliwa...

Maombi ndio njia pekee...

YESU KRISTO ndio njia, anajua mwisho wetu kabla ya mwanzo.
 
Ogea chumvi ya mawe kwa siku mara mbili ndani ya siku saba....itakusaidia kuondoa kimavimavi au mikosi na nuksi zilizojaa divi la mkazuzu au divi la mkamwamba usiposhtuka mapema jamii itakuja kukuona ni kinyago cha mpapule
 
Shikamoni wakubwa zangu

Mimi ni kijana wa miaka 22, nimekuja mbele yenu kuomba USHAURI kwa haya yanayo ni kumba Katka maisha yangu hasa ya kielimu maana Nahisi Nimerogwa😑 kuna matukio kadhaa yamejitokeza katika harakat zangu za kielimu mpaka Nahisi Nimerogwa. Kuna matukio matatu ambayo mpaka Sasa sielew nimeikuta nimekata tamaa

Tukio la Kwanza nikiwa primary miaka kadhaa iliyopita, shule nilikuwa nasoma ya private iliungua ktk uchunguzi wa walimu katika Tukio Hilo Walifanikiwa kumtambua mtuhumiwa mmoja ambae Katika mahojiano zaidi alinitaja mimi kama mhusika wa tukio hilo ili hali kwamba mimi sikuhusika kwa namna yoyote ile😔 nilijaribu kujitetea lkn wapi, mwisho wa siku nilitimuliwa shule ile

Tukio la pili nikiwa advance shule fulani Kanda ya ziwa, kuna Tukio la kihalifu lilifanywa na baadhi ya wanafunzi hapo shuleni, ambapo wanafunzi walivunja kufuli za locker za wanafunzi wenzao kipindi wanafunzi wengine tukiwa prepo. Lkni baada ya uchunguzi walifanikiwa kutaja wahusika chakushangaza mimi pia nilitajwa na walimu kama mhusika, Aisee nilishangaa sana maana sikuhusika kwa namna yoyote na tukio Hilo. Utetezi wangu haukusaidia mimi kupewa suspension kuanzia mwezi wa 11 mpaka necta hii ilipelekea kufeli mitihani ya kidato cha sita.

Tukio la tatu, ni KIPINDI hichi nikiwa mwanachuo katika chuo cha diploma kada ya afya kozi medical laboratory. Kuna uhalifu umefanyika kwenye hostel za wanafunzi kuibiwa simu na pc. Ijapokuwa mimi nakaa nje ya chuo, lkn kuna mhalifu alikamatwa ambae si mwanachuo ni raia wa mtaani tu hivyo alivyokamatwa ktk mahojiano na Polisi alinitaja mm kwa majina kwamba ndie nimekuwa namsaidia kufanikisha uhalifu huo chuoni. Ilipelekea mm kukamatwa na kuwekwa lockup ilhali mimi sihusiki kabisa na nilitajihidi kujitetea hakuna anayenielewa. Sasa kesi yangu ipo kwenye bodi ya chuo nasubiri maamuzi tu. Na sjui kama nitafanya mitihani ya end of semister2

Nimekuja mbele yenu kuomba USHAURI juu ya haya matukio yanayonikumba maana nahisi kurogwa najiona sina thamani ya kuendelea kuwepo duniani.

Karibuni wakubwa zangu mnishauri nifanyaje mbona mimi tu!!
Kuwa makini sana, unapoelekea atafanya kosa mwingine hapa JF kisha wewe utapigwa ban.
 
Back
Top Bottom