Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Lakini pia hali ya hewa ina matter, pengine mm natumia Viscosity ndogo kutokana na weather ya nchi/mkoa wangu
 
Lakini pia hali ya hewa ina matter, pengine mm natumia Viscosity ndogo kutokana na weather ya nchi/mkoa wangu
Yes. Hali ya hewa inachangia sana. Lakini manufacturer akirecommend oil fulani, inakuwa ideal kwa hali zote za hewa. Sababu gari huwa linajaribiwa kwenye mazingira mbalimbali kabla halijaingia sokoni.

Sisi wengi wetu huwa tunajilipua na 20W50 na maisha yanasonga. Ila kiukweli hiyo ni oil nzito balaa.
 
😄😄 Mambo ya Germany Engineering hayo.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
1. Unatakiwa kufahamu gari lake inatumia kidding gani cha oil kwenye gear box
2. Ni mara ya kwanzq kuifanyia Service hiyo gari?
3. Kama ilishafanyiwa Service, ulitumua oil gani, kiasi gani cha oil kilitum8ka na walishauri ufanye service nyingine baada ya km ngapi?
4. Hii Service uiiyoifanya wametumia oil gani?
 
Mag
Magari mengine hayana deep stick, nk
 
Achana na BOT.. Uwe na akili ya kuijua gari yako..!
Kubadilisha oil..
Filter..
Coils na Plugs..
Fuel pump..
Hizo sio kazi za kupeleka gari garage.. Unafanya mwenyewe..!
Ni kweli, ila nyumba zetu sio rafiki. Inatakiwa nyumba yenye gereji na shimo la kuingia kuweza kufanya service ndogondogo kama kubadilisha engine oil.
 
Hiyo ina engine ya N52B25 weka Castrol Oil 5W30 Fully synthetic, Ujazo ni Lita 6.5 na siyo lita 8.
Ebhana eee! Na mi nataka nifikie levo hizi mzee......

At least kwa gari nitakayomiliki niwe na maujuzi niijue kama mke yaani.

Bongo hii ukimsikiliza fundi tu au muuza duka tu anaweza kukupoteza. Wana conflict of interest sana hawa jamaa
 
Ni kweli, ila nyumba zetu sio rafiki. Inatakiwa nyumba yenye gereji na shimo la kuingia kuweza kufanya service ndogondogo kama kubadilisha engine oil.
Au unakua na zile jeki kubwa za kulift.
 
Kwa upande wangu nafaham magari na matengenezo yake plus nina kifaa cha obd2 scan tool...gari yangu ya kwanza kununua ni mjerumani Volkswagen polo bts 2008, nilianza kuisoma gari kabla haijafika bongo thanks kwa tutorials za youtube, nilipata kujua service inavyofanyika plus vifaa vinavyohitajika na kwa kiwango kipi so hata gari ilivyofika bongo sikupata shida nikazama kariakoo nikachukua oil castrol edge 5w30 as recommended nikachukua oil filter ilala pale then nikafanya service after that chumba ikaingia kwa road.

Point muhimu ni kuifaham na kuijui gari yako good newz nowdayz kuna google plus youtube huko kila aina ya maelekezo utakayohitaji.
 
Kwa Volkswagen polo bts 2008 gharama ya kufanya service ikawa hivi mwezi wa August 2022
1) Engine oil castrol edge 5w30, pale kariakoo kuna duka la castrol niliuziwa lita moja kwa elfu 23 x 4 = 92,000/-

2) Oil filter element, pale ilala niliuziwa kwa elfu 30,

Jumla ikawa 122,000/-
 
Safi.. Umefanya service kiuchumi zaidi..
Uwe unanunua oil kwenye gallon kuliko hizo 1lts.. Utasave zaidi..!
 
Safi sana
 
Hii ishu ya Oil bado kuna Changamoto fulani fulani.

Hii Castrol Edge 5W30 kopo la lita 1 bei inachezea kati ya 20k to 30k.

Mfano mimi nmenunua kama week mbili zimepita kwa 30k. Na huko nilikonunua namba nilipewa na Authorized dealer wa Catrol Tz. Yeye Dealer hakuniuzia sababu anauza jumla na mimi nilikuwa nataka rejareja.

Sasa sijui, Huenda wanaouza 20k,25k, hapo kuna feki au Jamaa wa 30k ameoverprice.

Nimenunua tester ya Viscosity za Engine Oils nitaipata this week. Nitafanya test zangu kadhaa kwa Oils za maduka mbalimbali, nitajua mbivu na mbichi.
 
Hapa tutajua alizeti ni ipi na oil ni ipi.. itasaidia watu wengi
 
Castrol changamoto sana (mtaani zipo fake and original), supplier Mkuu haleti, kabadilisha brand anauza Puma Oils. Natumia Atlantic Oil kutoka Kwa authorised supplier.
 
Castrol changamoto sana (mtaani zipo fake and original), supplier Mkuu haleti, kabadilisha brand anauza Puma Oils. Natumia Atlantic Oil kutoka Kwa authorised supplier.
Authorized Supplier wa Castrol Ni Wambi Lubes wapo Nyerere Road ila wao wanauza Jumla.

Ukiwacheck wanakupa namba za mawakala wao.
 
Mkuu umechukua ile hand viscosity tester au ?? Naomba details kama hautojali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…