Wakuu nimerudi tena, Nadhani mtakuwa mnaniona hapa mara kwa mara Kila nitakapopata changamoto
Juzi kati nilipata safari ya Dodoma nikaenda na Beamer (BMW X3) na ndio ilikuwa kwa mara ya kwanza naenda safari ndefu na hii gari
Wakati naenda muda wa kulifanyia service ulikuwa Bado haujafika zilibaki kama kilometers 1,200 plus nikaenda Dom nikarudi zikabaki kama kilometers 200+ ili zitimie kilometers 3,000 muda wa kufanya service ufike
Sasa Wakati narudi nilivyofika mbezi Taa ya Engine oil ikaniwakia (yellow) nikafika nyumbani, jana nikalipeleka Mikocheni kwa lengo la kuongezwa oil
Mikocheni Coca-cola Garage ya Atlantic lakini nilivyofika jamaa wakanambia kabla ya kuongeza oil itabidi walicheki kwanza kama kuna leakage wakacheki hawajakuta leakage yoyote ila wakanambia itabidi walifanyie Service kabisa maana oil wameikuta ni nzito tofauti na inavyotakiwa (nikakubali)
Waka change Oil na Oil filter Gari ikakaa sawa, nikapewa invoice total ikaja Tsh 483,800,
Ile Quotation Iko hivi
Oil 8 liters 350,000
Filter 60,000
Subtotal = 410,000/=
Vat 18% 73,800
Total = 483,000/=
Swali langu ni kwamba ukilifanyia Gari service na haina leakage yoyote Oil inatoboa hadi next Service au hapa katikati inabidi uiongezee?
Na je kwa situation yangu ya jana ni kweli ilibidi gari lifanyiwe Service au walivutia upande wao wa kibiashara, Wajuzi naombeni mshee experience zenu
View attachment 2453442