Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Naomba nifafanulie namba 3 halafu hiyo namba 4 naomba nisaidie na link tafadhali kama unaweza
OBD II Scanner ni kale kamashine ka kukuambia matatizo mbalimbali ya gari ata kabla taa ya njano haijawaka kwenye dashboard yako.

Unaweza ukanunua au ukawa unaenda kupima.

Kwa kuanza nakushauri anza kwenda kupima kwa mtu mfano JituMirabaMinne anakupa full report. Maana inakupa summary sana.

Kuhusu namba 4, nakutumia namba za admins inbox.

 
Mkuu Oil Gani ni recommended kwa BMW X3 ya 2008 kwa hali ya hewa ya Dar ambayo inaweza kutoboa hizo Kilometers 5,000
Maximum 10000km Kilometer ila badilisha at 8000 to 9000km.

Castrol oil angalia na gauge number gani engine inataka. Mashine ni ya kisayansi fata maelezo
 
Kwani Unamwaga oil kwa wiki au km?
Kwa km Ni uongo


Oil inapoteza utelezi wake kwa joto Kali inapotea haraka

Hiace inayotembea route ndefu inaenda 130 ikifika inarudi jumla 260km kwa siku ..Hadi ifikishe kilometa 7000 Ni siku 26

Na hiace ingne route za town inaenda na kusimama kila baada ya do ukiweka oil siku moja baada ya week mbili utagundua Kuna moja oil yake imechoka mapema haswa ile ya route ndefu inakaa na joto Kali muda mrefu oil inapoteza utelezi wake mapema sana

Hata Bajaj TV's king

Huwezi sema ubadili oil kulingana na dumu la oil lilivoandikwa

Jiulize kwanini route za town hata baada ya week mbili km huwa zinasoma Kati ya 1500km Hadi 1600 bado oil inakuwa inadai ila oil hio hio ukitembea route ndefu kwa siku tu mfano 300km ukifika uendapo ile oil huwezi kurudi nayo? Hadi ubadili na umetembea 300km tu


Au hao wanaosema oil Ni 10k km means gari inaweza toka dar kwenda kahama ikarudi ikaenda Tena kesho yake ikarudi jumla iende kahama Mara tano na oil ile ile? Waambie wajarbu Kama hujachinja gari kwa bei ya mchicha
 
Okey boss, ila Still bado unachofanya ni kwa km sema hufati km zilizoandikwa unazipunguza na km 10,000 mbona tunafanya sana tu. Labda useme kwa mazingira kama hayo ya gari ipo safarini muda wote au kazini inaweza kuwa sawa. Ila kwa mazingira yetu ya kawaida km 8000 elf tisa kujisahau mpka 11000 inafanyika sana tu.
 
Shukrani mkuu nasubiria namba

JituMirabaMinne unapatikana wapi kwani?
 
Bro unajua kazi ya sensor wewe?

Unajua maana ya Fault?

Kwa hiyo tairi kupungua upepo halafu TPMS sensor ikakuambia low pressure hiyo siyo fault?
Sensor enyewe inaeza kuwa na fault na fault isilete fault yenye fault kwenye fault ...tuna dizain saket mbali mbali za umeme na sensor za kupima vitu mbali mbali naelewa nachosema hata bmw wanafahamu Hilo sijui wewe Ni Nani unakataa
 
Sensor enyewe inaeza kuwa na fault na fault isilete fault yenye fault kwenye fault ...tuna dizain saket mbali mbali za umeme na sensor za kupima vitu mbali mbali naelewa nachosema hata bmw wanafahamu Hilo sijui wewe Ni Nani unakataa
Kazi ya sensor ni kutoa taarifa tu. Hakuna kazi nyingine.

Nazungumza kwa muktadha wa magari.

Kwenye gari, Hizo taarifa zinapewa modules then modules ndio zinaleta message kwenye dashboard. mfano low tyre pressure, low coolant, low oil level, service engine soon, n.k. Wenye hayo magari wapo kwenye huu uzi waseme kama magari yao hayawapi hizo taarifa.

Taarifa zingine haziji kwa mtumiaji module inafanya decision yenyewe. Mfano gari imeua kifaa fulani, Module inaengage limp mode. Gari inakuwa haina nguvu mpaka urekebishe kifaa kilichozingua.

Sijui wewe unazungumzia sensor zipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…