Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Kwani sisi za kwetu tunapikia?

Hicho kinachotoa taarifa kinaweza kuwa na fault pia BMW wanajua Hilo we Ni Nani unakataa
Kwani kuna mahali mimi nimekataa ishu ya sensor kuharibika. Mbona mimi mwenyewe nazibadilisha sana kwenye gari za watu.

Sensor kuharibika ni internal fault ambayo inapelekea sensor itoe wrong signal.

Na siyo kila taa inapowaka sensor inakuwa mbovu, Ndio maana nilisema sensor inatoa taarifa.

Kwenye magari tunapima unapata fault ni sensor fulani, ila mara nyingi sana unakuta sensor ni nzima na tatizo ni kitu tofauti na sensor itself.
 
Oil huwa inaweza kupungua kidogo sababu ya heat lakini huwa kwa kiwango ambacho ni allowable.
Modern cars kuna vitu vingi vya kusubiri sensors zikuambie na siyo kukagua kila siku.
Uwe aina ya engine ndio inakuwa rahisi kupata msaada ukisema tu BMW X3 gari ina variant nyingi sana. Ni ngumu mtu kuguess ni X3 ipi.

Pia oil recommended kwa BMW ni Castrol hata kwenye mfuniko wameandika. Kuhusu grade hapo ndio itategemea na aina ya engine.
Ila wewe jamaa UISHI MILELE....
Huwa unasaidia kwenye mambo mengi....
Maana humu kuna kudanganyana kupita kiasi.......
 
Hahaha inategemea aisee.. Kuna BMW za 20W 50..na oil unabadilisha mwenyewe..!
Jamaa yangu kariakoo anatumia BMW 320i huwa ananunua oil ya BMW yenyewe tena inauzwa Kwa Lita moja Tsh 60,000 × 4,pamoja na filter yake TSH 35,000 na diagnosis 50,000.

Sometimes kama starehe yako duniani ni magari basi sio ishu Sana kutumia laki 3 baada ya miezi 5
 
kama zilikuwa zimebaki 200km, ilitakiwa ipate services. Wapo sahihi kukufanyia service..

Ulitaka uongeze oil mkuu ili iweje ?

Wazee wa toyota wakiona hako ka bei wataongea hapa siku nzima 😅😅😅😅
😀 katoyota hapo nishafanya service ya engine na miguu yote na chenji inabaki ya kununulia wese la kuanzia misele
 
Wakuu nimerudi tena, Nadhani mtakuwa mnaniona hapa mara kwa mara Kila nitakapopata changamoto

Juzi kati nilipata safari ya Dodoma nikaenda na Beamer (BMW X3) na ndio ilikuwa kwa mara ya kwanza naenda safari ndefu na hii gari

Wakati naenda muda wa kulifanyia service ulikuwa Bado haujafika zilibaki kama kilometers 1,200 plus nikaenda Dom nikarudi zikabaki kama kilometers 200+ ili zitimie kilometers 3,000 muda wa kufanya service ufike

Sasa Wakati narudi nilivyofika mbezi Taa ya Engine oil ikaniwakia (yellow) nikafika nyumbani, jana nikalipeleka Mikocheni kwa lengo la kuongezwa oil

Mikocheni Coca-cola Garage ya Atlantic lakini nilivyofika jamaa wakanambia kabla ya kuongeza oil itabidi walicheki kwanza kama kuna leakage wakacheki hawajakuta leakage yoyote ila wakanambia itabidi walifanyie Service kabisa maana oil wameikuta ni nzito tofauti na inavyotakiwa (nikakubali)

Waka change Oil na Oil filter Gari ikakaa sawa, nikapewa invoice total ikaja Tsh 483,800,

Ile Quotation Iko hivi

Oil 8 liters 350,000
Filter 60,000

Subtotal = 410,000/=

Vat 18% 73,800

Total = 483,000/=

Swali langu ni kwamba ukilifanyia Gari service na haina leakage yoyote Oil inatoboa hadi next Service au hapa katikati inabidi uiongezee?

Na je kwa situation yangu ya jana ni kweli ilibidi gari lifanyiwe Service au walivutia upande wao wa kibiashara, Wajuzi naombeni mshee experience zenu
View attachment 2453442
Umesema taa ya oil iliwaka.Je baada ya kuweka oil taa ilizima? na Je km 200 unahisi umepigwa au?
 
Jamaa yangu kariakoo anatumia BMW 320i huwa ananunua oil ya BMW yenyewe tena inauzwa Kwa Lita moja Tsh 60,000 × 4,pamoja na filter yake TSH 35,000 na diagnosis 50,000.

Sometimes kama starehe yako duniani ni magari basi sio ishu Sana kutumia laki 3 baada ya miezi 5
Aisee nahisi wamiliki wapya wa hizi gari wanabambikiwa bei..
Oil ya 60k per litre sio mchezo..!
Mimi 56k nanunua lita 5..na gari inadunda..!
Garage wanafanya janja janja.. Wanauza oil kwa litre wakati bei ya 5litres sio sawa na 1 litre mara 5..!
 
Aisee nahisi wamiliki wapya wa hizi gari wanabambikiwa bei..
Oil ya 60k per litre sio mchezo..!
Mimi 56k nanunua lita 5..na gari inadunda..!
Garage wanafanya janja janja.. Wanauza oil kwa litre wakati bei ya 5litres sio sawa na 1 litre mara 5..!
OIL GANI?
 
Hahahaha 🤣🤣🤣 aisee maisha tumetofautiana Sana maana Sisi akina Toyota ni laki moja Tu unamaliza kila kitu kuanzia service Hadi ufundi alafu uzuri wa Toyota huwa napitiliza kufanya service Hadi km 5000 na gari inadunda tu
Bimmer X3 kwenye Toyota nahisi equivalent yake ni gari kama Rav4.. Vanguard.. Harrier..
Sidhani kama kwa 100k utatoboa service..!
 
Back
Top Bottom