Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Kanuni za Udereva hutakiw KUWASHA gari bila kufanya UKAGUZI.

Ukaguzi upo wa ndani na upo wa nje

Ukaguzi wa Ndani unahusu Gari kwa ujumla mpk Injini. Hapo ndio utapima na Oil kulingana na Deep stick ya oil, maji (Coolant) hydraulic mpk brake fluid.. etc.

Ukaguzi wa Nje ni ENVIRONMENTAL based, unaangalia Uvunguni.. Nyuma au mbele ya matairi kuna sharp objects? Je kuna Mtoto au Mnyama Kalala?

Hiyo ndio maana ya daily follow up
BM hawana dipstick.. Oiii
 
Hivi kilometa elf 10 unazijua

Acheni Soma ujinga unaoandikwa kwenye oil

Vyombo vyangu vya biashara week mbili natoa oil Tena kwa kusimamia mwenyewe

Oil za Mjerumani ni 10kkm wanazoshauri sasa kusema oil 3k km kubadilisha. Napata ukakasi ila sio big deal. Kimfaacho mtu chake na mimi sio fundi makanika
 
Next time fanya hivi:

1. BM E90 3 Series na E83 X3 zinatabia ya kunywa oil (oil burn) kwahiyo make sure una lita 1 kwenye buti always. Tatizo linasolvika kwa kubadirisha seals.

2. Kukwepa gharama zisizo rasmi, kanunue mwenye oil Liqui Molly hapo ungetumia jumla kama laki 3 na nusu hivi.

3. Tafuta OBD scanner. Jitu la Miraba Minne atakushauri zaidi

4. Jiunge magroup ya BMW Tanzania WhatsApp na Telegram.

5. Umezingua sana kuwakiwa kale kabirika ka oil.

6. Jiandae kwa makubwa zaidi kila sekunde..
 
Wakuu nimerudi tena, Nadhani mtakuwa mnaniona hapa mara kwa mara Kila nitakapopata changamoto

Juzi kati nilipata safari ya Dodoma nikaenda na Beamer (BMW X3) na ndio ilikuwa kwa mara ya kwanza naenda safari ndefu na hii gari

Wakati naenda muda wa kulifanyia service ulikuwa Bado haujafika zilibaki kama kilometers 1,200 plus nikaenda Dom nikarudi zikabaki kama kilometers 200+ ili zitimie kilometers 3,000 muda wa kufanya service ufike

Sasa Wakati narudi nilivyofika mbezi Taa ya Engine oil ikaniwakia (yellow) nikafika nyumbani, jana nikalipeleka Mikocheni kwa lengo la kuongezwa oil

Mikocheni Coca-cola Garage ya Atlantic lakini nilivyofika jamaa wakanambia kabla ya kuongeza oil itabidi walicheki kwanza kama kuna leakage wakacheki hawajakuta leakage yoyote ila wakanambia itabidi walifanyie Service kabisa maana oil wameikuta ni nzito tofauti na inavyotakiwa (nikakubali)

Waka change Oil na Oil filter Gari ikakaa sawa, nikapewa invoice total ikaja Tsh 483,800,

Ile Quotation Iko hivi

Oil 8 liters 350,000
Filter 60,000

Subtotal = 410,000/=

Vat 18% 73,800

Total = 483,000/=

Swali langu ni kwamba ukilifanyia Gari service na haina leakage yoyote Oil inatoboa hadi next Service au hapa katikati inabidi uiongezee?

Na je kwa situation yangu ya jana ni kweli ilibidi gari lifanyiwe Service au walivutia upande wao wa kibiashara, Wajuzi naombeni mshee experience zenu
View attachment 2453442
Kama uneweka oil nzuri as recommended. Unatakuwa kufanya next service at least baada ya 7500Km mpaka 10000km
 
kama gari haina leakage yoyote inatoboa hadi service nyingine na mara nyingi inategemea na oil unayotumia kwenye gari lako zipo oil hadi 5000km ndo unabadili. Ikitokea gari lako oil inapungua ujue kuna shida kwenye gari lako mana gari lenye mfumo mzuri uwezi ongeza oil ni service hadi service.
Oil huwa inaweza kupungua kidogo sababu ya heat lakini huwa kwa kiwango ambacho ni allowable.
 
Kanuni za Udereva hutakiw KUWASHA gari bila kufanya UKAGUZI.

Ukaguzi upo wa ndani na upo wa nje

Ukaguzi wa Ndani unahusu Gari kwa ujumla mpk Injini. Hapo ndio utapima na Oil kulingana na Deep stick ya oil, maji (Coolant) hydraulic mpk brake fluid.. etc.

Ukaguzi wa Nje ni ENVIRONMENTAL based, unaangalia Uvunguni.. Nyuma au mbele ya matairi kuna sharp objects? Je kuna Mtoto au Mnyama Kalala?

Hiyo ndio maana ya daily follow up
Hizi ni kanuni za udereva wa gari za miaka ya zamani na gari za kijapani.

Gari za kijerumani washa gari, kagua dashboard, piga gear.

Mambo ya kukagua oil na kuangalia upepo kwenye matairi, siyo saaana. Hata taa ikiungua huitaji mtu kukuambia taa imeungua. Cheza tu na dashboard.
 
Next time fanya hivi:

1. BM E90 3 Series na E83 X3 zinatabia ya kunywa oil (oil burn) kwahiyo make sure una lita 1 kwenye buti always. Tatizo linasolvika kwa kubadirisha seals.

2. Kukwepa gharama zisizo rasmi, kanunue mwenye oil Liqui Molly hapo ungetumia jumla kama laki 3 na nusu hivi.

3. Tafuta OBD scanner. Jitu la Miraba Minne atakushauri zaidi

4. Jiunge magroup ya BMW Tanzania WhatsApp na Telegram.

5. Umezingua sana kuwakiwa kale kabirika ka oil.

6. Jiandae kwa makubwa zaidi kila sekunde..
Hiyo namba 5 na 6 una maana gani? Kwamba hutakiwi kuruhusu hiyo taa kuwaka? Na ikiwaka ni kosa kwamba itasababisha ubovu?
 
Ndio maana mnaua Magari bila kujijua. Gari zinawaka Moto kwa makosa madogo tu unawz kuta Bonnet cover imesogea au imeachia je utajua ktk Dashboard? Je deep stick imepanda juu na kuruhus Oil kuvuja na kufata exhaust pipe utajua? Unajua madhara yake?.. Gari kila siku ikague na kama muda upo Pima/hakikisha bolt za matairi zimekazwa vzr at least kila baada ya wiki unafanya Uhakiki
Modern cars kuna vitu vingi vya kusubiri sensors zikuambie na siyo kukagua kila siku.
 
Next time fanya hivi:

1. BM E90 3 Series na E83 X3 zinatabia ya kunywa oil (oil burn) kwahiyo make sure una lita 1 kwenye buti always. Tatizo linasolvika kwa kubadirisha seals.

2. Kukwepa gharama zisizo rasmi, kanunue mwenye oil Liqui Molly hapo ungetumia jumla kama laki 3 na nusu hivi.

3. Tafuta OBD scanner. Jitu la Miraba Minne atakushauri zaidi

4. Jiunge magroup ya BMW Tanzania WhatsApp na Telegram.

5. Umezingua sana kuwakiwa kale kabirika ka oil.

6. Jiandae kwa makubwa zaidi kila sekunde..
Naomba nifafanulie namba 3 halafu hiyo namba 4 naomba nisaidie na link tafadhali kama unaweza
 
Mkuu Oil Gani ni recommended kwa BMW X3 ya 2008 kwa hali ya hewa ya Dar ambayo inaweza kutoboa hizo Kilometers 5,000
Uwe aina ya engine ndio inakuwa rahisi kupata msaada ukisema tu BMW X3 gari ina variant nyingi sana. Ni ngumu mtu kuguess ni X3 ipi.

Pia oil recommended kwa BMW ni Castrol hata kwenye mfuniko wameandika. Kuhusu grade hapo ndio itategemea na aina ya engine.
 
Inauzwaje mkuu, na Manufacturer wanashauri oil gani?
Next time do a lot of research about your car.

Utapunguza hata kupigwa au kuwekewa vitu vya hovyo.

Na hata ukitaka kununua kitu, fanya research.

Mpaka sasa ulitakiwa ujue recommended oil for your car. Na ujue unaipata wapi na kwa bei gani.

Wengine ni mawakala wanalazimisha kukuwekea oil mradi wao wauze.

Nilishawahi fukuzwa garage ya mtu kwa kumkatalia kuniwekea hiyo hiyo Atlantic. Nilienda na oil yangu ya Castrol na filter yeye anataka kuweka yake ya Atlantic na aniwekee filter zake tena za bei ya juu zaidi.

Gharama ingekuja almost 250k ila ningeenda kichwa kichwa ingefika almost 400k.

Bro. I do tonnes of research before i do anything serious.
 
Back
Top Bottom