Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Next time do a lot of research about your car.

Utapunguza hata kupigwa au kuwekewa vitu vya hovyo.

Na hata ukitaka kununua kitu, fanya research.

Mpaka sasa ulitakiwa ujue recommended oil for your car. Na ujue unaipata wapi na kwa bei gani.

Wengine ni mawakala wanalazimisha kukuwekea oil mradi wao wauze.

Nilishawahi fukuzwa garage ya mtu kwa kumkatalia kuniwekea hiyo hiyo Atlantic. Nilienda na oil yangu ya Castrol na filter yeye anataka kuweka yake ya Atlantic na aniwekee filter zake tena za bei ya juu zaidi.

Gharama ingekuja almost 250k ila ningeenda kichwa kichwa ingefika almost 400k.

Bro. I do tonnes of research before i do anything serious.
Wewe Service huwa unafanya wapi mkuu?
 
Kanuni za Udereva hutakiw KUWASHA gari bila kufanya UKAGUZI.

Ukaguzi upo wa ndani na upo wa nje

Ukaguzi wa Ndani unahusu Gari kwa ujumla mpk Injini. Hapo ndio utapima na Oil kulingana na Deep stick ya oil, maji (Coolant) hydraulic mpk brake fluid.. etc.

Ukaguzi wa Nje ni ENVIRONMENTAL based, unaangalia Uvunguni.. Nyuma au mbele ya matairi kuna sharp objects? Je kuna Mtoto au Mnyama Kalala?

Hiyo ndio maana ya daily follow up
🙌
 
Kwa hio kuchekiwa ukapewa mkeka wa milion kwamba ndo ukaona wako vizuri ,, je ningekupeleka sehemu likachekiwa wakakwambia au kukupa mkeka wa Bei ghali zaidi means ungeona huko pa Bei ghali ndo mafundi😁 we bado mshamba na utapigwa sana

Ushamba wa watu wengine wenye pesa na akili zipo down ndo inafanya wajanja tuishi mjini just kwa kujua ongea tu
💪Ahsantee
 
Hizi ni kanuni za udereva wa gari za miaka ya zamani na gari za kijapani.

Gari za kijerumani washa gari, kagua dashboard, piga gear.

Mambo ya kukagua oil na kuangalia upepo kwenye matairi, siyo saaana. Hata taa ikiungua huitaji mtu kukuambia taa imeungua. Cheza tu na dashboard.
Huo Ni uongo hakuna

Jifunze tofautisha fault na kitu ambacho kitaleta fault . BMW inaonesha fault tu
 
Thanks, Kuna mtu hapo juu ameniambia nikutafute kuhusu OBD scanner, ebu naomba ufafanuzi kwanza nikijue
Hiyo ni tool ambayo inawezabkukusaidia kujua baadhi ya matatizo ya gari yako. Lakini pia inaweza kukusaidia kufanya baadhi ya reset kwenye gari yako.

Kuna taa zitawaka utarekebisha tatizo, taa haitazima utatakiwa kufanya reset.

Ni hivo tu,
 
kama gari haina leakage yoyote inatoboa hadi service nyingine na mara nyingi inategemea na oil unayotumia kwenye gari lako zipo oil hadi 5000km ndo unabadili. Ikitokea gari lako oil inapungua ujue kuna shida kwenye gari lako mana gari lenye mfumo mzuri uwezi ongeza oil ni service hadi service.
Rotary engines huwa zinakula oil bila ya kuwa na leakage wala kuua oil ring. Na hata baadhi ya engine za Subaru zina mchezo huo.
 
Back
Top Bottom