Ushauri; Nashindwa kujikubali

Ushauri; Nashindwa kujikubali

Habari zenu , mim n binti wa miaka 27, jamani mwenzenu nashindwa kabisa kujikubali na kujiamini kutokana na umbo langu na watu wananisema Sana Jambo linalonifanya nizidi kujiona sipo vizuri.

Ni mwembamba yaani sina hipsi hata kidogo ,nina mapaja madogo Sana ,pia nina maziwa makubwa , nilikuwa nikijiona vizuri tuu na kujikubali hapo awali lakini kutokana na watu kunisema ovyo ,najiskia vibaya mno.

Ilifikia wakati nikawa nasemwa na watu kuwa Mimi ni magonjwa wa gonjwa fulani ,niliumia sana baada ya kupata habari hizo ,lakini sina ugonjwa wa aina yoyoye ile , Jambo hili linanifanya nikose ujasiri kabisa ,.

Nina boyfriend lakini nakosa hata ujasiri wa kuwa nae mala kwa mala hadi kuna muda nawaza nivae nguo za aina gani labda nitaonekana vizur,Kuna muda hadi boyfriend aliniambia kuwa anahitaji ninenepe , wakati sijajiumba Mimi.

Nahitaji faraja yenu wana jf ,au nivae mavazi gani, au nifanye nini nami niwe na muonekano mzuri na wa kuvutia?
Tafuta washauri nasaha

Hakuna binadamu aliyekamilika

Lakini hiyo maLa Kwa maLa siyo sawa, ni mara Kwa mara
 
Unasikitisha sana...

Ila unaongea kama dume...
 
I am sorry you are going through this but hao watu hawatoacha kusema hata kama ukija kunenepa wataanza tena maneno,wapotezee fanya yako don’t allow them to control you,keep yourself busy,fanya mazoezi,talk to someone you love,,,,,,,,wishing you well.
 
Mwenyezi Mungu hajawah kosea katika kuumba kwake. Kila mtu ana uzuri wake, hata wewe lazima utakua mzuri, jikubali dear kuwa hivyo ni deal.
 
Habari zenu, mim ni binti wa miaka 27, jamani mwenzenu nashindwa kabisa kujikubali na kujiamini kutokana na umbo langu na watu wananisema sana, jambo linalonifanya nizidi kujiona sipo vizuri.

Ni mwembamba yaani sina hips hata kidogo, nina mapaja madogo sana, pia nina maziwa makubwa, nilikuwa nikijiona vizuri tu na kujikubali hapo awali lakini kutokana na watu kunisema ovyo, najisikia vibaya mno.

Ilifikia wakati nikawa nasemwa na watu kuwa mimi ni magonjwa wa gonjwa fulani, niliumia sana baada ya kupata habari hizo, lakini sina ugonjwa wa aina yoyoye ile, jambo hili linanifanya nikose ujasiri kabisa.

Nina boyfriend lakini nakosa hata ujasiri wa kuwa nae mara kwa mara hadi kuna muda nawaza nivae nguo za aina gani labda nitaonekana vizuri, kuna muda hadi boyfriend aliniambia kuwa anahitaji ninenepe, wakati sijajiumba mimi.

Nahitaji faraja yenu wana JF, au nivae mavazi gani, au nifanye nini nami niwe na muonekano mzuri na wa kuvutia?

Fanya mazoezi ya kuongeza shape, kula vyakula vya protein utapendeza sana
 
Dada wewe binafsi ni zaidi ya hipsi na ni zaidi ya huo unene unaoutaka.. Thamani ya utu wa mtu haipimwi kwa muonekano wako unapimwa kwa unachokimiliki ndani yako... utashi wako,upendo wako,utu wema wako,uvumilivu na nk.hutakiwi wewe kujinyanyapaa hata siku moja,

Hivi umeshaona watu wana viwiliwili tu lakini wapo happy huko mtaani au mitandaoni?sembuse wewe Dada umepewa viungo vyote?

Hujitendei haki.... kila siku kumbuka huwezi kupendwa na kila mtu wewe sio pesa.... Mabadiliko yanaanza na wewe,Jipende,jithamini, hii itakuongezea confidence hutaamini hao wanaokusema wataacha.
 
kama mungu mungu hajakujaalia wowowo ni ngumu mwanamke kujikubali kwa dunia ya leo...wowowo ni muhimu kuliko kila kitu
 
Dada wewe binafsi ni zaidi ya hipsi na ni zaidi ya huo unene unaoutaka.. Thamani ya utu wa mtu haipimwi kwa muonekano wako unapimwa kwa unachokimiliki ndani yako... utashi wako,upendo wako,utu wema wako,uvumilivu na nk.hutakiwi wewe kujinyanyapaa hata siku moja,Hivi umeshaona watu wana viwiliwili tu lakini wapo happy huko mtaani au mitandaoni?sembuse wewe Dada umepewa viungo vyote?hujitendei haki.... kila siku kumbuka huwezi kupendwa na kila mtu wewe sio pesa.... Mabadiliko yanaanza na wewe,Jipende,jithamini, hii itakuongezea confidence hutaamini hao wanaokusema wataacha.
Tatizo wowowo
 
Back
Top Bottom