LLB ina soko sana ndugu, ila inahitaji watu wenye akili za kutosha, akili ya kuelewa na kupambanua mambo na kutetea hoja. hii itakufanya ufanye kazi hadi utakapofariki ukiwa mzee kabisa, kwasababu hata ukistaafu bado utaendelea kufanya sheria kwenye law firm yako popote pale tz tena ukijicontrol mwenyewe bila kuwa chini ya mtu. the more unavyozidi kupractice shere, the more unavyopata uzoefu ivyo utakuja kujikuta kazi ya hela nyingi unafanya kwa muda kidogo sana.
kama wewe ni mzembe, umefaulu kwa kukariri shuleni sio kuelewa, mtu wa kubebwa tu, akili yako imekalia kuajiriwa tu tangu ulivyoanza darasa la kwanza, HAUNA NAFASI KUWA MWANASHERIA, kwasababu hautatengeneza hela, utakuwa unashindwa kesi kila siku. sheria inahitaji watu waelewa sana, kuhusu kuwa na soko, kama mtu unajiamini, hauwezi kutegemea kuajiriwa, wengi wa wanasheria ninaowafahamu hawataki kuajiriwa, wengi wameacha kazi za kuajiriwa
Nimeipenda hii, good clarification. Watu wasikariri kuajiriwa!