Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Kwa wazo ulilonalo tu Naomba nikuite "Mdogo wangu"
Mdogo wangu, please USIACHE KAZI...

baki na Kazi yako na omba huo mkopo ufanye biashara, tena omba Mikopo kama hiyo Zaidi ya mmoja Baada ya kuona maendeleo ya kile utakachoanzisha
Tafuta watu 10 walioacha kazi.... Nakwambia waliofanikiwa hawazidi 3.
Usiache kazi tafadhalini, Mimi nimeajiriwa kampuni Binafsi na bado Nina biashara zangu na nimeajiri watu.
Kwenye biashara kuna changamoto nyingi Sana, unaanguka na kusimama, unaanguka, unajikwaa unasimama, wengine wanaanguka jumla...
Baki na Kazi yako na anzisha biashara
HAPA KIYOSAKI HANA NAFASI
 
umejibu vizuri sana japo hujui kwa undani umuhimu wa shule na umri wake. mimi hiyo master sina na sitegemei kwenda kwa sasa lakini naiona changamoto yake huko mbele umuhimu wa shule katika shughuli za kujitegemea. hivyo kwa umri wake anahitaji kufanya hivyo.
msimdanganye mwenzenu millioni kumi sio pesa nyingi katika biashara kuanza nazo anaweza kuanguka vibaya fikiria hana network kubwa na huenda wazo la biashara atafanya nini bado hana uhakika.
kwenda shule ni kupunguza risk na kuongeza mtandao zaidi.
ninaye mshauri naimani ana umri wa kati 24-32 yeye ananielewa msimdanganye kama ninyi mlifanikiwa kiurahisi ni bahati yenu lakini kwa huyu bado anachangamoto nyingi kwanza ndo kwanza kaanza maisha ukilinganisha na kazi aliyonayo.
 
kama nikubebe vile!
ili nichukua zaidi ya miaka mitatu kupata biashara siku niliyoipata nilimpata mteja mmoja mabaye mpaka leo namuhudumia kwa adabu.
 
Watu wengi mmetoa ushauri mzuri sana, naomba niwakumbushe kwamba aliyeleta hii post anaona akiendelea kubaki kwenye ajira, hawezi kuwa hata na huo mtaji mdogo wa kuanzisha biashara ili aone kama itafanikiwa.

Pili, akipata mkopo akaendelea kufanya kazi na biashara wakati huohuo, hataweza kusimamia vizuri biashara yake na matokeo yake hataweza kupata mafanikio kwa usimamizi mbovu. Kwa ufupi ajira yake ndio itakua hiyo biashara kufa na kupona.

Cha msingi ni umakini na utulivu wa kupata wazo na biashara sahihi. Vilevile kama hauna uzoefu wowote wa biashara, kuanza kwa 10M inaweza kuwa changamoto, ungeanza na 3 au 5 M kuona upepo unaendaje.
 
Kwanza consider mambo matatu
1. Unataka kufanya biashara gani
2. Mkopo utaanza kulipa baada ya muda gani
3. Jee una wanaokutegemea na wamekubaliana na uamuzi wako.

Haya mambo matatu ni muhimu sana. Nilipo acha kazi yangu sikujua haya mambo matatu yana umuhimu kiasi gani.

Kujua biashara utakayo fanya nje ndani ni muhimu sana, sababu hutopeteza muda mwingi kujifunza na hutokuwa kwenye risk ya kupoteza sehemu kubwa ya Mtaji.

Lini unaanza kulipa mkopo is very important, sababu kama unaanza kulipa ndani ya week chache basi ujue kabisa inabidi uwekeze kwenye cash cow business.

Familia lazima wasupport to some extent. kama umeowa na mke kila siku atakuwa anasema nilikwambia usiache kazi nilikwambia this and that basi ujue upo kikaaangoni kaka.
 
Hakuna fao la kujitoa??? LAPF wana hilo fao mbona
 
Miaka mitatu kazini midogo mkuu! Ungesubiria angalau kumi,then chukua huo uamuzi.
 
NAONA UNATAKA KUISOMA NAMBA KWA KUJITAKIA.KILA LA HERI MKUU
Watu kama wewe bila kuajiriwa hakuna maisha,kwa hiyo usimkatishe mwenzio tamaa,mwenzio kasoma alama za nyakat na anataman kuwa zaid ya alipo,hakuna ubishi kuajiriwa ni kuminywa akili yako ili ubaki ukimtegemea na kumnyenyekea aliyekuajir siku zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukikopa dhamana yako ni nini,serikalini ukikopa ujue mshahara ni wao,wewe ukisepa unakuja kujikuta wanaidaka pesion yako ila with miaka miiiingi interest kubwa. Biashara ni ngumu mno la msingi omba kazi sekta binafsi ya ofsi unayotaka kufanya.Mfn ukifanya kazi benki unaweza kufungua sacos.Biashara nyiiingi sasa ni kama zimeingiliwa na kilamtu,nothing new...kama ni msomi unajua kwanza inatakiwa ufanye reseach ya biashara hiyo na kuplan mapato na faida. Au shirikiana na vijana waliopo tayari uwe na hisa.
 

Ushauri wangu: Usithubutu kuchukua mkopo kufanya biashara wakati umeacha kazi! Hata kama unafanya kawi masaa mengi chukua mkopo anza biashara unayoitaka polepole, lala hata masaa matano tu kwa siku ikibidi (katika kipindi hicho cha mpto), uache kazi pale tu unapoona biashara inaanza kutoa mwanga. Usiache kazi kijana!
 

Flowery story with no specifics. Kama ushuhuda wa kanisani kabla ya kumpa mchungaji sadaka.
 
Anzisha kwanza biashara ikikolea ndio uzembee kazini usiache kazi kabla hujapata kazi. Mimi nakaribia kuacha baada ya kumaliza haka ka Master kangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani unaacha kazi sababubumepata mastaz au sababu unaenda kufanya biashara zako....ni vip masterz yako inahusiana na biashara unayotaka kufanya na inakupa assuarance ipi ya kufanikiwa katika mambo yako.
take from me .... hizi elimu za shule au vyuo huwa hazina tija katika mapambanobya mtaani...ndio maana mabilionea karibu wote duniani hakuna hata mmoja prof seuse doctor.

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 
....Amekuambia kazini daily anatumia 11- 12 hrs, na pia akirudi hoi bin taabani, vp tena ataweza kusimamia biashara?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawajua wanamshauri kwa nidham ya uoga...hakuana uoga kama umeajiriwa na unafanya biashara zako...zitaendelea kuwa za kawaida tuu na hazitokuwa mpaka siku utakayoacha kazi na kusimamia biashara zako mwenyewe.

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 
Acha kumtia woga...from zero to hero. Haitaji kutafutavkazi wala ajira...anahitaji kufanya biashara zake....zimtoe utumwani mwa ajira isiyolipa wala kumuhakikishia mwisho mzuri wa maisha yake

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 
Acha kumtia uoga na story yako...wewe unatumia masaa 11 kazini bado usafiri na uchovu huo muda hana wa kufanya kazi huku kajiajiri...mzigo mzito mpe mnyamwezi...wewe mzigo wako mwepesi beba mwenyewe ....yeye mnyamwezi atabeba mzigo wake mzito.

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…