Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Mp##zi wewe,labda wewe ndo slave

great thinker
Pole sana kwa changamoto unazopitia lakini ongera kwa kutafuta freedom. Wengi wa watu waliokushauri wanakwambia mtaji huo ni bora unge make mwenyewe alafu ukanzia biashara then badaye ndo uchukuwe mkopo ili kudevelop business ni lakini option mbili ni muhimu hasa ikijuwa unachotaka kufanya.Ngoja nikupe story yangu labda uka learn kitu.
Mimi nilianza kazi mwaka 2014 mkoani mtwara,katika maisha yangu ya kazi sikuwa kufurahia kazi yangu hata siku moja nilikuwa na ndoto in my life so nikaona nikitegemea kazi siwezi kufikia ndoto zangu.Nikaamuwa kuchukuwa loan 2015 nikanunuwa shamba la mikorosho ile kufika 2016 soko la korosho likacheuwa nikapiga pesa nzuri tu naweza sema nilichanga karata zangu vzr.Nilikamata 10mil kupitia shamba zile pesa nikafunguwa beiber shop.Thanks God mambo yanaenda powa nimewekeza sehemu nyingine ya kuuza juice ya miwa na matunda mengine.Pia this year nalimia shamba langu la korosho kama kawaida.Sijawahi juta since nimechukuwa loan. Nimeweza kujenga nyumba within 3yrs nina usafiri(ndinga) +viwanja 3.Mshahara wangu nautumia kwa kusaidia ndugu zangu na matumizi madogo tu.
Mytake .Use you're salary kama mtaji wa kuanzia biashara lakini nakuomba usiache kazi kwa haraka hadi uweze kusimama vzr.Mimi sijaacha kazi ila sitafikisha ten yrs kazini.Anza sasa usisubiri kesho

great thinker
 
Kwanza nikupe hongera mkuu kwa wazo lako maana hata huo mshahara unaopata ni kama zawadi tu ya kukufanya uendelee kufanya kazi na si kutimiza malengo yako bali malengo yao.
~Ni vizuri kujiwekezea hela ili uje kutumia kama mtaji na si kukopa maana mkopo unasaidia kuendeleza na kukuza biashara.
~Usitishike kua mtaani kugumu kwani kufeli ni mojawapo ya kujifunza, bila kufeli utajifunza lini?? Kumbuka: watu wengi walio na malengo wanawafanyia kazi watu wenye malengo, utaendelea kua mtumwa hadi lini? Better be a risk taker
~ Fanya research kuhusu biashara unayotaka kufanya na pia tafuta ushauri kwa watu mbalimbali.
Start with commitment finish with consistence




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habari za majukumu.

Natambua JamiiForums ni kijiwe cha wasomi na mchanganyiko wa watu wenye busara zao.

Najitokeza mbele yenu mnipe ushauri kidogo, kwa ufupi mimi ni muajiriwa katika serikali yetu hapa Tanzania, kutokana na changamoto za kazi na hali halisi ya maisha nina plan kukopa fedha kiasi cha 10m kisha nianzishe miradi yangu binafsi ili nijiajiri niachane na kuajiriwa maana naona napelekeshwa ilihali maslahi ni duni sana.

Kazi ni nyingi mno na maslahi ni kiduchu sana, nilitamani kuanzisha miradi nikiwa katika ajira lakini muda ninaoingia na kutoka kazini ni wastani wa masaa 11 mpaka 12 kwa siku, hali hii inanichosha sana kiasi kwamba hata nikifika home akili inakua imechoka sana naishia kulala tu.

Kwa mantiki hiyo naona umaskini wangu unaweza kua wa kudumu maana hata nikiwatazama walionitangulia naona hawana kitu kikubwa sana walichofanya maishani.

Nina dreams nyingi na kubwa, napenda kua mtu huru na mwenye mafanikio makubwa kupitia biashara na kilimo, naiona ajira kama kifungo cha kunifanya niwe maskini. Sasa kwakua nimekaa kwenye system kwa takribani miaka mitatu naona ni vema nijilipue nikafanye yangu.

Naomba ushauri na mapendekezo yenu, watu hatulingani akili endapo unaona niko wrong basi naomba unishauri namna ya kuboresha hili wazo.

Kejeli na matusi sio mahala pake hapa, mimi ni kijana kama ulivyo kijana pengine nikawa sawa na mwanao ni vema unishauri kwa kujua unamshauri ndugu yako na mwana JF mwenzako.

Natanguliza shukrani.
Kosa kubwa ulilo fanya ni kuja kuomba ushauri wafanya kazi. Ukitaka kujiajiri tafuta watu walio kwenye hiyo sekita wakupe ushauri. Huku utatiwa uoga hadi ukimbie.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara siyo lazima ufanye mwenyewe., while Ukiwa kwenye ajira anzisha biashara muajiri mtu wa kusimamia. Milioni kumi ni hela ndogo sana ambayo inaweza kuanzishia biashara usiyoijua from zero. Ila ungekuwa na experience na biashara yeyote ningekuwa wa kwanza kukushauri uache kazi, this is from real experience I have.
Endelea na kazi mkuu at the same time anzisha biashara after atleast two years baada ya kupita misimu mbali mbali ya biashara yako acha kazi.
Ni ushauri tuu
Biashara ikiwa changa inamuhitaji sana mwenye nayo au mwenye Idea.
Kosa kubwa sana ambalo watu hufanya ni hili.

Biashara inakuhitaji wewe. Mengi hakukabizi Mke wake au Shemeji yake biashara ya kutengeneza Kalamu bali alianza mwenyewe.

Thomas Edson baada ya kuwa na wazo alianza hakumtafuta Mjomba wake au shemeji yake au mke wake.

Mawazo yako ni mawazo ya watu waoga.

Hapo tegemea mshahara wako ndo ukalipe vijana wa kazi mshahara tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jambo jema Sana kujiajiri ila nakushauri uanze hiyo biashara uliyopanga hata Kwa mtaji kidogo ili ukiona biashara yako imesimama ndio ukope kuongezea mtaji na ndio taratibu nyingine za kuacha kazi uzifanye Kwa sababu ukisema ukope hiyo pesa huku umeacha kazi alafu na biashara ikute ndo Mara yako ya kwanza kufanya, mkuu utayamani kukimbia nchi maana Kwa hali iliyopo inahitaji uweze kusoma soko kwanza kabla ya kujilipua kuweka pesa yote huko.

Yangu ni hayo tu
Inawezekana pia. Kuna kitu inaitwa Burn the boat.

Some time unatakiwa kuchukua maamuzi.Magumu sana ambayo ni ya maumivu makubwa sana na katika hayo maamuzi kuna pain process

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi ningekushauri uache kazi kama hela ingekuwa ya kwako ume save.. na biashara unayoenda kufanya unaijua kwa experience sio za kuhadithiwa na watu....

kukimbia deni sio njia sahihi siku hizi kuna credit reference utakuwa kwenye backlist na itakuharibia sana kukopa mbeleni maana hata biashara isimame kama mengi kukopa hakuishagiiii...

njia sahihi ni fanya ufanyavyo upate experiwnce ya biashara wakati upo kazini tayariiiiiii...
Atapataje experience akiwa kazini? au atakuwa anaifanyia kazini kwake?

Biashara ikiwa changa inamihitaji sana Initiotor wa Idea. ni sawa na.mtoto mchanga kumuhitaji sana mama yake kwa miezi 3 ya mwanzo na ndo maana ya likizo ya miezi 3 ya uzazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anzisha kwanza biashara ikikolea ndio uzembee kazini usiache kazi kabla hujapata kazi. Mimi nakaribia kuacha baada ya kumaliza haka ka Master kangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Anatakiwa kusimamia Idea yake mwenyewe. sasa unataka nani asimamie Idea yake?

Yaani Idea yake then Shemeji yake asimamie au mke wake?

Haya ndo mambo yanatufabya tubakia kama tulivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKIKOPA na KUACHA KAZI huo mkopo utaulipaje? Si unatafuta kuolewa wewe?
Fanya hivi kama unakopa kwa kutumia mshahara hilo ni ruksa. Hiyo pesa iwekeze kwenye biashara. Ukifanikiwa kuendesha hiyo biashara baada ya mwaka mmoja bila kuyumba yumba ndipo ufikirie kuacha kazi. Kujiajiri sio rahisi kama watu wanavyosema...
Kuajiriwa ndo rahisi? kutumwa na kupelekesshwa ndo unaona Dili? nitajie rist ya Mfanya kazi tajiri hata mmoja.

Acha uoga Kuajiriwa ni ufala na ni kubinasifisha muda wako kwa mwanaume mwingine.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanzako leo alikuwa analilia kazi hiyo hiyo anase.ma anawatoto

Sent using Jamii Forums mobile app
Unasumbiwa na uoga na kuona kuajiriwa ndo Dili sana. Wewe huna kazi na muda wako? maana ya kuajiriwa ni kwamba wewe Muda ulio pewa na Mungu huna kazi nao bali inabidi uwapatie vichwa ambao ni risk taker wafanyaie kazi.

Endelea kubinasifisha muda wako kama Madini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka Nina mengi ya kukushauri lkn sina mda wa kutosha kuandika hapa pia nina uvivu sana wa kutype. Labda nikukumbushe jambo, kaka ni ngumu kuacha kazi ili ukatafute kazi, tafuta kazi ndiyo uache kazi. Anza shughuli ndogo ndogo kwanza za kiabiashara ndiyo ujue nini ufanye

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngumu kivipi? yeye si anajiajiri? Ujue tuna tujmnatumia back graoud za ajabu sana na hizi ndo zinatugharimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
So.kumbe mikopo hulipwa na mishahara? unajua principal za mikopo?

au unazania ni ilenakopaga kununua Magari then mnakatwa the rest ya maisha yenu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu angalia maelezo yake ni kama anatumia Mshahara kukopa kama ndivyo achukuapo hela mwezi huo huo wanaanza kukata pia kumbuka amesema ndio anaenda kuanza biashara so ktk hicho kipindi utaulipa vipi huo mkopo?
 
Kwa uwelewa wangu nihivi usikope mkopo kwa ajili ya kuanzisha biashara ila kopa mkopo kwaajili ya kuendeleza biashara,,mkuu usiache kazi mpaka uhakikishe umeanzisha biashara na kumudu changamoto zake kisha ukiona hapa sasa sinashaka na hich nnachokifanya ilikutafuta mianya zaidi yakibiashara ndo ujilipue na uingie kusimamia biashara zako.Sababu hiyo milion 10 unaweza ukaiona kubwa ukaacha kazi kutokana na bado huna na hujapata changamoto za kibiashara ukaiona ikiteketea bila kujua,na nyumban pesa hakuna aisee utamtafuta mchawi nani wakati ni wewe mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Asiache kazi sasa biashara aanzishe vipi? apateje vipi uzoefu?
Au kwa kupiga simu kuulizia kama leo wateja wamefika wangapi?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom