Kujiajiri ni wazo zuri sana, siyo rahisi kufanikiwa maishani kwa kutegemea ajira.
Siwezi kusema idea yako kama ni nzuri au laa, watu huwa wana suggest kukopa kuendeleza biashara na siyo kuanzisha biashara.
Ila sometimes mtu huna option hiyo. Hatujui ni biashara gani unataka kuanzisha, au hata wewe una nidhamu kiasi gani kwenye hela, maisha na biashara, so kukwambia ufanye au usifanye ni kubahatisha.
Mimi niliacha kazi mwaka jana mwezi 7 na kuanzisha kampuni yangu. Mwanzo huwa ni mgumu, hasa kwa sababu ya expectations.
Ukiwa una plan biashara huwa tuna assume baada ya muda flani itaanza rudisha hela, mara nyingi haiwi hivyo.
So ushauri wangu, kuwa realistic kwenye expectations na pia like me nilinunua bodaboda kuingiza hela za kula nikiwa napambana na kampuni (ingawa bodaboda nayo inataka dereva mzuri, luck for me, wangu azingui)
All in all, panga, pangua, panga tena, kuwa na plan B na tafuta muda kwa namna yoyoye ile do research. Jifanye mwehu tu, zunguka uliza watu depending na biashara unayotaka kufungua.
Watu wengi wenyeelimu au waajiriwa tuna fail kuingia kwenye biashara kwa sababu tuna overthink. Tunawaza mno, tuna run scenerios nyingi, mara nyingi either zina tukatisha tamaa au tuna poteza interest, unakuja kushtuka darasa la 7 anakupita kimaendeleo.
All the best aisee. Biashara ndo mpango mzima. So far sijutii kuacha kazi.
Sent using
Jamii Forums mobile app