Ushauri: Nataka nioe Binti wa Kishua

Ushauri: Nataka nioe Binti wa Kishua

mwache abaki kama mchepuko wako ukijiingiza apoo ili swala litakuumiza sana hutaweza kujenga familia yenye furaha na kujaliana tafuta mwanamke mnayeendana anayekupenda jinsi ulivyo c kwakile ulichonacho
Bonge la wazo.. Nilishawaza kama hivi kiongozi.. Ngoja muda ufike nitafanya implementation!
 
kama unampenda pambana umchukue hata kwa kumjaza kibendi....Maisha yanabadilika any time alafu kaza na huyo huyo .Usikubali kushidwa kirahisirahisi.
Asante sana kaka Mkubwa hii ni Bonge la Comfort.. Do or Die!
 
Uyo anakupotezea mda yy hana nia ya kuolewa na ww kama mnaachana maranyingi hivyo mnarudiana tena. Na akishapata wa kuendana nae anakuacha kbsaa......
Mkuu umeona mbali aisee..Najua ipo siku kama hiyo ila ndo ile tayari ushampenda aisee..
 
Huyo binti na wewe either of you ni watoto. Kuweni mkifika walau 27 years ndio muanze kuongelea hizo habari.
What i feel its like 2 teenagers thinking of getting married and having kids. Things dont work like that. Mwanamke lazma awe na msimamo juu ya nini anataka.
Somehow true..
 
Mkuu kwa umri wako bado una nafasi usitumie nguvu sana katika mapenzi. Huo ushuwa wake huyo binti ndio unaokutatiza, you waste your time bro. Huyo teyari kashaandaliwa maisha na wazazi wake, nawe tengeneza maisha yako. Kama ipo ipo tu usiumize kichwa chako

.
 
Piga mimba mkuuu ata usipomuoa mtt wako atakuja kua wakishua hatateseka kama ww

Sent using boeing 737 max8
 
Dogo chukua shauri huu huyo mwanamke anakufaa sababu ya kwanza mnahitajiana ndio maana mpaka leo hamjaachana hiyo ni ishara kwamba mtavumiliana kwa kila jambo wenzenu hawamalizi hata week pili maamuzi unayo wewe mwanamke hana maamuzi siku zote wewe ndio dira ya familia hivyo kua imara na fanya maamuzi sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za siku ndugu wanafamilia wa JF!, Poleni na Majukumu Mazito ya kifamilia na ya kutafuta Mkate wa Kila siku hasa kwa awamu hii ngumu ya 5.


Naomba nianzie hapa..
Unauhakika humpendei ushua wake?


Hili ndilo kubwa.
 
Habari za siku ndugu wanafamilia wa JF!, Poleni na Majukumu Mazito ya kifamilia na ya kutafuta Mkate wa Kila siku hasa kwa awamu hii ngumu ya 5.


Naomba nianzie hapa..

Kwanza kabisa mimi ni kijana wa Miaka 28 mwenye elimu ya shahada moja, katika harakati za maisha nilifanikiwa kukutana na binti mmoja miaka takribani 6 iliyopita, Nilitokea kupendana naye sana..


Tafuta wa size yako mkuu
 
OA nasema OA huyo, maisha yasasa hayataki kujizuga.... Yeye akikuletea kauli sijui yeye mambo Safi mkrashi jifanye kama vile uuoni ushua wao mwambie pesa zamadafu hizo....,akiregeza piga mimba tuliaaaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za siku ndugu wanafamilia wa JF!, Poleni na Majukumu Mazito ya kifamilia na ya kutafuta Mkate wa Kila siku hasa kwa awamu hii ngumu ya 5.

Naomba nianzie hapa..

Kwanza kabisa mimi ni kijana wa Miaka 28 mwenye elimu ya shahada moja, katika harakati za maisha nilifanikiwa kukutana na binti mmoja miaka takribani 6 iliyopita, Nilitokea kupendana naye sana..

Huyu binti ni mtoto wa kishua ukilinganisha na familia yetu.. mara nyingi amekuwa akinisumbua katika mahusiano yetu(Hakuwahi kuonesha kunicheat).. hasa kwa kutaka breakup za ghafla ambazo anadai mzee wake anamshinikiza aachane na mimi.. huwa natulia anajiachisha kisha anajirudisha (Mapenzi yake kwangu hayakupungua mpaka hivi sasa naandika uzi huu).

sasa kwa kipindi chote tumekuwa tukipanga kuoana.. ila ninachogundua ni kwamba binti yupo tayari kishingo upande.. yaani ananipenda ila akifikiria status ya familia yangu haifanani na ya kwao anarudisha moyo wake nyuma ghafla na hata kutaka kubreakup.. akijisahau hurudisha mapenzi na ananipenda kama kawaida.

Kwa sasa imefika wakati ambao hata mimi nimeanza kuchoka na mwanamke ambaye hatabiriki..leo hivi kesho vile.. nataka nioe, Japo favorite option ni yeye.. Nampenda huyu mwanamke.. ila kigezo cha yeye kuwa kishua na kuonekana kutoridhika na hali ya kwetu kinanipa wasiwasi endapo kama huyu binti ataweza kunivumilia au la..(i'm sure of being financialy free)

Kuna wakati akipitiwa hujisahu na kuropoka kabisa kuwa baba yake hapendi aolewe na mimi na mara kadhaa amemsihi asiwe hata na mahusiano na mimi.. nikiwa naye haya maneno najifanya kuchukulia kirahisi but kiukweli ni maneno mazito..

Ndugu zangu.. mimi kama mtu mzima sasa.. nina uwezo wa kufanya mbinu zozote(Hata kwa Figisu) za kumuoa tu awe mke wangu.. ila je madhara ya kuwa na mke wa aina hii itakuwaje? ..kwa maana sitaki familia isiyo na Amani ...mtu ambaye mzazi wake hataki awe nami.. na kwa kiasi kikubwa hata kama ananipenda ameonesha kumsapoti mzee wake..

Ndugu zangu wanafamilia wa JF tumetofatiana uzoefu achilia mbali kuzidiana mitazamo.. ni matumaini yangu kuna watu wenye uzoefu na matukio ya aina hii.. naombeni mnipe ushauri kwa nyinyi wenye uzoefu..je kuna madhara gani kumuoa mwanamke mwenye situation kama hiyo?.. Je unashauri nimuoe au Niache?.. Je una maoni gani ya kudeal na situation ya aina hii?..

Asanteni Sana!

Khan
Hayaa mambo sio kwa matajiri hata kwa watu wa hali ya kawaida, eti mzazi anaongea mkwe hasiye na hela simtaki......... wanaweka presha kwa watoto mwisho wa siku wanakuwa single mother.
 
Hayaa mambo sio kwa matajiri hata kwa watu wa hali ya kawaida, eti mzazi anaongea mkwe hasiye na hela simtaki......... wanaweka presha kwa watoto mwisho wa siku wanakuwa single mother.
Good newz ni kwamba tulishindwana mapema..
 
Achana nae huyo hata ukiforce ndoa atakuwa kakuoa yeye.
 
Back
Top Bottom